Kwa Kamanda IGP na RPC Dodoma

Kisampido

Senior Member
Jun 19, 2013
157
63
Nianze kwa kuwapa Pole na ujenzi wa taifa, naomba niweke wazi kwamba Kuna jambo nimelishuhudia hapa kwa jirani yangu siamini kama utendaji wa jeshi la polisi umefikiwa viwango hivi ama ni wale Maaskari walikuwa wakifanya vile kwa matakwa Yao binafsi.

Ilikuwa majira ya saa Saba mchana Askari alifika kwa jirani yangu kwa lengo la kumuhitaji mke kwa lengo la kumkamata na kwenda naye polisi kwa bahati mbaya hawakumkuta kwani alikuwa kazini.

Nilisikia akimuuliza jiani mke wako Yuko Mimi ni Askari, jirani yangu akamjibu ni vema ukanionyesha kitambulisho chako kama kweli ni Askari Ili tuendelee na mazungumzo ghafra yule Askari akamjibu ngoja nikuonyeshe kitambulisho angiza mkono mfukoni na kutoa pingu na kumfunga jirani yangu.

Baada kumfunga pingu akaanza kumshambulia kwa ngumu mateke vichwa huku jirani yangu akihoji kuomba kitambulisho ni kosa? Wakati huo gari no STM 5771 land cruiser double cabin ya rangi ya kijivu ikiwa imepaki karibu na kwangu hapa kukiwa na Askari mmoja na mtumishi wa Gmicrofinance ambayo IPO karibu na Magorofa ya Mpwapwa Frats.

Kwa bahati nzuri yule mwanyakazi wa Gmicrofinance namfahamu anaitwa Andrew lakini Moja ya wale Askari huwa namuona sana pale kwenye kituo kidago kinaitwa Ndashi kwenye mataa njia ya kwenda Dodoma in walimpakia jirani yangu na kutokomea naye kusikojulikana.

Mimi niliendelea na mjukumu yangu mpaka naondoka majira ya saa tisa hakurudi. Sasa Kuna maswali najiuliza ni kwanini askari atumie nguvu kubwa namna Ile kisa kaulizwa kitambulisho cha kazi?

Pili ni kwanini taasisi binafsi ya Gmicrofinance (kausha damu) itumie gari la serikali kupitia mtaani kukamata wadeni wake na askari ambao hawana uniform Wala vitambulisho lakini pia hii ni hatari kwa usalama wa Askari kwani muda mfupi tayari majirani walisha jaa, pengine ingeleta uvunjifu wa amani
 
Kwahiyo imekuwa ni mtindo,

Dah nchi inapelekwa wapi hii Ina maana magari ya serikali yanatumika kwenye mishe za watu binafsi mala kubebea wahamiaji haramu mala mihadarati kweli kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake maana STM 5771 hii gari ni mali ya serikali sasa na kausha damu wapi na wapi!? Matumizi mabovu ya Mali za serikali kwahiyo Kodi ya wananchi ndiyo matumizi yake.!!?
 
Ifike wakati hata nyinyi majirani muwe na akili timamu vichwani mwenu. Kwa Askari Polisi yoyote yule anayekuja kumkamata mtu kwa utaratibu kama huo ulioeleza huyo atakuwa ni Mhalifu, wala siyo Askari Polisi. Utaratibu wa kukamata Watuhumiwa upo wazi umeelezwa ktk Sheria za nchi.

Majirani mlipaswa kutoa ushirikiano kwa Mwananchi mwenzenu, mlipaswa kumkabili vilivyo huyo Askari Polisi kwa sababu alikuwa ni mhalifu kama Wahalifu wengine, ni jambazi au mtekaji.

But all in all, Sheria za Umiliki wa Silaha hapa Tanzania zinatakiwa kubadilishwa, kumiliki bunduki iwe ni HAKI ya kila raia mwenye akili timamu hapa nchini.
 
hukupata hata mwanya wakuwasha camera yako kisirisiri kwa mbali
Mkuu sikuwa na simu kubwa ila nilijitahidi kuandika namba za gari STM 5771 Land cruiser double cabin ya rangi ya kijivu Mpya dereva Mzee hivi amevaa miwani pia polisi walikuwa wababe walikuwa wanamshambulia jamaa uku wamemfunga pingu yaani kama jambazi mateke vichwa ngumi ni hatari
 
Haya maelezo bila kaushahidi cha unyama tutaishia kumpa pole tu, au wewe unaweza kushuhudia?
 
Mkuu ungerekodi ukamtumia kigogo au mange watusaidie kutupostia hao watu pale NEW YORK BOARD SQUARE.
 
Maelezo yanatosheleza kabisa. Usajili wa gari hizonamba ni utambulisho tosha wakuanzia. Kwakuwa inajulikana gari ni mali ya nani na siku hiyo muda huo alikuwa nayo nani so huyo dereva atasaidia kusema aliokuwa nao kwenye hilo tukio.
Sahihi kabisa pia huyo Andrew wa hiyo Gmicrofinance anafahamika pia itasaidia maana jamaa kataja mpaka eneo ilipo ofisi hata huyo Askari ambaye kituo chake cha kazi kinafahamika
 
Haya maelezo bila kaushahidi cha unyama tutaishia kumpa pole tu, au wewe unaweza kushuhudia?
Nafkiri kama uchunguzi utafanyika upo ushahidi wa mazingira kwasababu tukio limetokea mchana na kuna baadhi ya vielelezo vimeonekana kwanza dereva wa hiyo gari ni shahidi tosha
 
Nianze kwa kuwapa Pole na ujenzi wa taifa, naomba niweke wazi kwamba Kuna jambo nimelishuhudia hapa kwa jirani yangu siamini kama utendaji wa jeshi la polisi umefikiwa viwango hivi ama ni wale Maaskari walikuwa wakifanya vile kwa matakwa Yao binafsi.

Ilikuwa majira ya saa Saba mchana Askari alifika kwa jirani yangu kwa lengo la kumuhitaji mke kwa lengo la kumkamata na kwenda naye polisi kwa bahati mbaya hawakumkuta kwani alikuwa kazini.

Nilisikia akimuuliza jiani mke wako Yuko Mimi ni Askari, jirani yangu akamjibu ni vema ukanionyesha kitambulisho chako kama kweli ni Askari Ili tuendelee na mazungumzo ghafra yule Askari akamjibu ngoja nikuonyeshe kitambulisho angiza mkono mfukoni na kutoa pingu na kumfunga jirani yangu.

Baada kumfunga pingu akaanza kumshambulia kwa ngumu mateke vichwa huku jirani yangu akihoji kuomba kitambulisho ni kosa? Wakati huo gari no STM 5771 land cruiser double cabin ya rangi ya kijivu ikiwa imepaki karibu na kwangu hapa kukiwa na Askari mmoja na mtumishi wa Gmicrofinance ambayo IPO karibu na Magorofa ya Mpwapwa Frats.

Kwa bahati nzuri yule mwanyakazi wa Gmicrofinance namfahamu anaitwa Andrew lakini Moja ya wale Askari huwa namuona sana pale kwenye kituo kidago kinaitwa Ndashi kwenye mataa njia ya kwenda Dodoma in walimpakia jirani yangu na kutokomea naye kusikojulikana.

Mimi niliendelea na mjukumu yangu mpaka naondoka majira ya saa tisa hakurudi. Sasa Kuna maswali najiuliza ni kwanini askari atumie nguvu kubwa namna Ile kisa kaulizwa kitambulisho cha kazi?

Pili ni kwanini taasisi binafsi ya Gmicrofinance (kausha damu) itumie gari la serikali kupitia mtaani kukamata wadeni wake na askari ambao hawana uniform Wala vitambulisho lakini pia hii ni hatari kwa usalama wa Askari kwani muda mfupi tayari majirani walisha jaa, pengine ingeleta uvunjifu wa amani
Jirani yako akirudi mwambie akavunje chungu hakuna namna
 
Back
Top Bottom