Kwa jinsi namba E inavyokimbiza kuna kitu hakipo sawa mahali

Kwa takwimu rasmi za benki kuu.. Kipindi cha miezi nane pekee January mpaka August 2022 watanzania wamenunua/wameagiza magari nje ya nchi yenye thamani ya mamilioni ya dola Hii tafsiri yake ninini kuna kitu hakipo sawa ama kwa uzuri au kwa ubaya

Inawezekana kabisa nchi imefunguka na pesa imerudi kwenye mzunguko kwakuwa hata kwenye ujenzi mambo ni moto licha ya vifaa vya ujenzi kupanda bei maradufu
Ama inawezekana kabisa kuna umakini umepata dhoruba kwenye mapato ya serikali hivyo kutengeneza mianya mingi ya upigaji
Ama pengine uwekezaji umeongezeka na watu sasa wanapiga kazi kufa na kupona.

Yoyote kati ya hayo yanaweza kuwa sahihi ama vinginevyo.. Tafakuri yangu ni hii kwamba kama kwa robotatu tu ya mwaka tumeweza kupeleka nje ya nchi bilion 400 kasoro kwenye manunuzi ya magari tuu, achana na manunuzi ya serikali na wakandarasi wageni na manunuzi ya vifaa vya ujenzi.. Hatuoni kama tunaidhoofisha hakiba yetu ya fedha za kigeni? Je tuna uwiano kwenye kuuza?

Kwa kununua magari yote hayo kwa kipindi kifupi hivyo kuna tafsiri moja tuu, kuzidi kuzineemesha nchi husika miaka ijayo kwenye vipuri na chochote kinachohusika na magari

Kwa takwimu hizi kama serikali yetu ina maono basi ianze kuangalia namna ya kuanzisha viwanda vya vipuri na vitu vyote vinavyohusika na hayo magari
Kwa kufanya hivyo
. Itakuwa ni mwanzo wa maandalizi ya kuwa na viwanda vyetu wenyewe vya magari
. Tutaokoa pesa nyingi za kigeni ambazo zingetumika kuagiza vitu husika
. Tungetengeneza ajira nyingi
. Mzunguko wa pesa ungeongezeka
Na mengine mengi mazuri.. Wizara ya biashara na washika dau wengine walione hili kama fursa
View attachment 2397068
ushauri mzuri sana
 
Kwa takwimu rasmi za benki kuu.. Kipindi cha miezi nane pekee January mpaka August 2022 watanzania wamenunua/wameagiza magari nje ya nchi yenye thamani ya mamilioni ya dola Hii tafsiri yake ninini kuna kitu hakipo sawa ama kwa uzuri au kwa ubaya
...
Yeni ya Japan imepoteza mpaka 30% ya thamani yake (ukilinganisha na Dola ya Marekani). Pia angalia JPYTZS, kutoka Tsh. 20 March mpaka Tsh. 15 October. Kwa hiyo, kwa uchumi rahisi tu, pesa ya nchi ikishuka wanunuzi wa nje wanapata bidhaa kwa bei poa. Kwa hiyo wakati mzuri wa kununua magari Japan ni sasa, wakati Yeni imeporomoka.
 
Yeni ya Japan imepoteza mpaka 30% ya thamani yake (ukilinganisha na Dola ya Marekani). Pia angalia JPYTZS, kutoka Tsh. 20 March mpaka Tsh. 15 October. Kwa hiyo, kwa uchumi rahisi tu, pesa ya nchi ikishuka wanunuzi wa nje wanapata bidhaa kwa bei poa. Kwa hiyo wakati mzuri wa kununua magari Japan ni sasa, wakati Yeni imeporomoka.
Mbona magari hayajashuka bei kwetu huku mkuu
 
Baadhi ya spare zitengenezwe hapa hapa, kwa kuanzia tungeanza na Brake shoe,brake pad,clutch plate. Kuna watu wanafanya utengezaji wa brake na clutch bonding wangewezeshwa kwa kupata mashine za kisasa ambazo wanazalisha kwa wingi.

Gasket zote za karatasi, hapa mchawi ni kuagiza gasket paper material kisha zinakuja kuchongwa kulingana na parts za engine na aina ya gari.
 
Manzoni nilivokua nasoma andiko lako kwamba magari yananunuliwa mengi nikajua unapinga watu wasinunue magari nikawa najiuliza kwann wakati ni dalili njema ya maendeleo

Ila ulivyomalizia na suggestion ya kuanzishwa viwanda vya spare parts ndo nikaelewa the whole story

Kiufupi umeupiga mwingi
Je mjapan atakubali hili ama zake ni kuendelea kutuletea misaada ya miundombinu na ujenzi wa vyoo?
 
Ndio maana pamoja na kufanya biashara nasi kwa miongo mitatu na ushee hajawahi hata maramoja kusema atujengee walau kiwanda kimoja cha vipuri
Vipuri vina hati miliki

Ukiiga tu umekwisha

Ndio maana hata matajiri wakubwa hawajengi viwanda vya vipuri

Gari atengeneze mjapani halafu wewe uibuke kutengeneza kipuri cha gari yake haiwezekani.Utakitengebeza exactly kama kilivyo hapo tayari uneshavunja sheria ya hati miliki
 
Ni kipindi cha kurudisha hazina pesa ambayo haikutumika kama sheria inavyoyaka
Sasa hapa wengi huwa hawarudishi na hiyo pesa iliyobakk hutafutiwa matumizi ya lazima ili isirudi, hapa ndio watu hupiga hasa..
Je ni kama haya matumizi ujenzi wa 'karavati'
=
1666692070262.png
 
Back
Top Bottom