Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,493
- 11,486
Alfajiri ya kuamkia leo jeshi la Israel kwa kutumia vifaru na mashambulizi ya anga wamefanikiwa kufikia kituo cha mpaka wa Gaza na Misri na kukishikilia kituo hicho kutokea upande wa Gaza.
Mara baada ya kufanikiwa kukishika kituo hicho jeshi la Israel limezuia uingizwaji wa misaada ndani ya Gaza ikitoa visingizio kuwa ina taarifa ya kutumiwa kituo hicho kwa vitendo vya kigaidi.
Kwa sasa njia zote za ardhini za kuingia Gaza ambazo huwa zinatumiwa na mashirika ya misaada kuwafikishiwa wapalestina chakula na mahitaji mengine zitakuwa zinashikiliwa na jeshi hilo la Israel
Upande wa kaskazini ya Gaza eneo la Erez kwa muda mrefu limekuwa likishikiliwa na jeshi hilo ambapo kiasi kinachoruhusiwa ni kile cha kuwafanya wakazi wa eneo hilo wasife tu kwa njaa lakini wasishibe na kuishi kama binadamu wengine.
Umoja wa mataifa na mashirika mengi ya misaada yamekuwa yakiilalamikia Israel kuwa kiasi wanachoruhusu kuingia Gaza ni kama tone tu la mahitaji kwenye bahari.Hata hivyo lawama hizo hazijaifanya Israel kulegeza kamba