SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,150
- 7,916
Simba ilipozindua WhatsApp channel yake, hadi CEO Imani Kajura akafanya press conference kuhusu uzinduzi huu. Binafsi na wengi wetu tuliona hii siyo issue kubwa kihivyo na tulikwazika pale ilipoorodheshwa kwenye Mkutano Mkuu kama ni moja ya mafanikio ya klabu msimu huu.
Pamoja na yote hayo yote haiondoi ukweli kuwa WhatsApp Channels ni moja ya trends mpya zinazoshika kwa kasi sasa kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyo "Threads". Mpaka sasa timu nyingi kubwa duniani zimefungua channel zao na hata viongozi wakubwa akiwemo Rais SSH naye anayo ya kwake.
Kwa klabu inayojipambanua kwenda na wakati na kuendeshwa kisasa, inashangaza sana kwa Yanga kushindwa kufungua channel yake na ni aibu kubwa, na najua wanajivuta kufanya hivyo kisa tu inaogopa kuonekana imeifuata Simba. Aliyekutangulia amekutangulia tu hata ujifiche vipi, dawa ni kuingia ulingoni tu kwenda naye sambamba.
PS. Kama shida ni bando au simu janja, mtuambie wadau tuchangie au tuwafungulie kwa niaba yenu halafu tuwakabidhi, mbona ize tu. Ni vizuri kuepuke aibu ndogo ndogo kama hizi.