Kwa hili nampongeza sana Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkarim Shah

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Leadership.jpg


MBUNGE wa Mafia, mkoani Pwani-CCM, Abdulkarim Shah, akiwa kwenye boti, aliyoikodi kutokana na kupigiwa simu msamaria mwema kwa ajili kusaidia kuokoa wananchi wa maeneo hayo, akitoa maelekezo kwa nahodha ni sehemu gani ya kupita wakati alipokuwa akishiriki katika kuwaokoa wananchi hao,waliokumbwa na mafuriko

Leadership2.jpg


Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, akimpokea mtoto aliyekuwa amehifadhiwa juu ya paa la nyumba, pamoja na msichana mmoja wa nje ya nchi, aliyejitambulisha kwa jina la Janne Borold, aliyekuwa naye sambamba katika kusaidia kuwaokoa wananchi hao
 
​mambo ya hollywood unaweza kuona watu wanapigana risasi kumbe hakuna kitu ni kuunganisha picha tu
 
Nampongeza Shah, hii sio photoshop...What would it save anyway?
By the way Nimetabasamu na hiyo picha ya pili baada ya kuona mtoto huyo anaepokelewa ameveshwa "Condenser" kiunoni!
 
wakati mafia hakuna boti ya abiria miaka yote, si angewatafutia usafiri wa uhakika wananchi wake kwanza na miaka yake 15 ya ubunge? Huyu ni Mr misifa tu, nakumbuka kuna siku nilimuona anachangia bungeni huku povu linamtoka juu ya suala la uda, huku akisahau kuhusu jimboni kwake hakuna usafiri wa aina yeyote wa uhakika kwa wananchi anaowakilisha!
 
Nampongeza Shah, hii sio photoshop...What would it save anyway?
By the way Nimetabasamu na hiyo picha ya pili baada ya kuona mtoto huyo anaepokelewa ameveshwa "Condenser" kiunoni!
"Condenser" Hahaaa...., imani za watu hizo. Kakikuwa hako katoto taifa tutegemee nini eti...!!? By the way mi nimependa yeye mwenyewe mbunge kuingia kwenye maji kuokoa watu, ni zaidi ya kutoa hela bana. Bravooo mheshimiwa mbunge!!
 
Mnyika, Mdee, zungu, mtemvu, na wabunge wengine wa Dar mmejifunza nini kwa Shah? Huyu ni mbunge wa CCM hongera sana kwa kuking'arisha chama chako wakati wa mafuriko ya Dar ukitoka mkoa mwingine wa pwani. Wabunge wa mikoa mingine mmejifunza nini? kwamba kumbe mbunge wa jimbo anaweza kuwa wa Taifa lote linapojitokeza janga la kitaifa
 
tunataka viongozi kama hawa sio porojo tu na kukosoa...... leo shah akikosoa hatuna shaka naye wajibu wake tumeuona
 
chadema mmeisoma hiyo picha huyo ni mbunge wa CCM tusikosoe tu pengine tusifie taifa hili ni letu sote. huwezi kupoteza utu wako kwa kumpongeza mbunge wa CCM japo inauma
 
si kweli kwamba mpaka mbunge apata nyongeza ya posho ndipo asaidie wananchi Shah kaonyesha mfano wa kuigwa.... kujitolea ni moyo si utajiri.
 
Lakini jambo la kumpongeza zaidi Shah hakukodi mtumbwi tu aliingia mwenyewe kwenye mafuriko kuokoa maisha ya watanzania wenzake. kitendo hiki kingeweza kugharimu maisha yake lakini yeye alijali maisha zaidi ya watanzania wenzake kwanza. vifo vya kishujaa hutokea kwa nadra angekufa kishujaa
 
Mbunge kama huyu hata mimi niko tayari kuvimbisha mishipa usoni kumtangaza, kwani ana uchungu kwa watanzania wote na wala si kwa wapiga kura wake tu. Kiwango hiki wabunge wengi wameaibika na wataishia kutoa tafsiri potovu kwa kuwa wamepigwa kisogoni.
 
Shah nakukumbuka kwenye sakata la UDA kule bungeni uliongoza mapambano ya kudai haki ya wakazi wa Dar sauti yake ilisimamia haki za wengi. wewe ni mbunge unayeongea kwa uchungu unapotetea haki za wengi kwa siku nyingi nilikuwa sikufahamu lakini matukio kadhaa yaliyojitokeza ndani na nje ya bunge katika siku za hivi karibuni nimekuona wewe ni mmoja wa tunu za CCM
 
wapo watakaosema Shah anataka sifa lakini wajue kwamba kitendo cha shah ndicho wananchi tulitaka kufanyiwa badala ya kuleta siasa kwenye majanga
 
bulji kwanza amuokoe Binti yake Naima toka kwa sadi mwanamboka

kwake kunavija kwa nini anaenda kuziba kwa wengine/.
 
Binafsi, sishangai hata kidogo kumuona Shah a.k.a Buji sehemu kama hiyo!!! Jamaa, ni mtu wa kujichanganya kwelikweli na raia...siku ya kwanza kukutana nae physically, nilistaajabu kusikia jamaa ni mbunge!! Nikapigwa na butwaa zaidi, siku nimekutana nae barabarani akanichukua hadi ghetoni kwake!!!! Kumbuka, am just ordinary person, kwahiyo ni mara chache sana kukuta mbunge anajichanganya na mtu wa kawaida kabisa hadi kufikia kukukaribisha sehemu anayokaa, hatukuishia nje, bali ndani kabisa!! Na kwavile nyumba yenyewe inaishi watu wengi, ilibidi kupigia stori kwenye room lake kabisa!!!!! Kwangu ilikuwa ni ajabu kidogo nikizingatia madaraka aliyonayo pamoja na age difference kati yetu!! Na sio siri, nazani kinachoibeba zaidi CCM Mafia ni tabia ya Buji kupenda kujichanganya na vijana otherwise, nazani CUF wana nguvu sana kule!!!
 
Back
Top Bottom