Kwa hili la pongezi kwa Askofu Mbinga, JK kawa mnafiki tu!

Bless the 12

Member
Nov 5, 2010
61
4
Leo TBC news, eti JK katoa pongezi za kuteuliwa askofu wa katoliki, mie naona Rais hili amekuwa mnafiki tu maana hizo pongezi za kuteuliwa askofu basi azitoe kwa makanisa mengine pia na hata masheikh basi. Naona kwa hili amechemka tu kama kawaida yake au anajigonga kwa Roman asionekane mdini. Sasa kama rais we utatoa pongezi kwa viongozi wa dini ngapi au ndo anahalalisha ubaguzi tu. Kwa hili sijaona sense yake kwa kweli.
 
Sioni tatizo na kitendo hicho!
Tukubali ukweli kuwa kwa makanisa makubwa kama Katoliki, Lutheran, Moravian, Anglikan etc wana taratibu ambazo ni very explicit and specific katika kumtawaza mtu kuwa uaskofu, na huwa inajulikana kuwa ni mtu mwenye hekima na uelewa, lakini pia ni mtu challenging kimawazo, ambapo anaweza kutoa criticism au constructive ideas kwenye system yoyote ya utawala, uongozi na mifumo yake.

Sitaisemea Misikiti na Mashehe, lakini najua kuwa kuna makanisa ya kisasa ambayo yana waumini 5, 10, 14 etc, ambapo hata wanavyopeana ngazi za uongozi haina standards wala si official...kwa hili ni wazi rais au kiongozi mwinginewe wa serikali hawezi kualikwa, au kutoa pongezi maana hata protocal itakosekana kwenye tendo zima.
 
Atawapongeza Maaskofu wanaokataa kuwasilisha report ya mapato na matumizi ya kanisa serikalini kwa kisingizio cha kwamba serikali haitoi ruzuku kwa makanisa?
Kuna siku nilishangaa kuona taarifa ya Kanisa moja nchi za ughaibuni kitoa mapato na matumizi ya kanisa ikiwemo kodi waliyolipa serikalini. Hapo sasa makanisa yetu yanadai kupata ruzuku toka serikalini, je yakidaiwa kulipa kodi?

Nikirudi nyuma kwenye mada Rais kafanya sawa kutoa pongezi hizo kwa askofu mpya wa Kanisa Catholic, huu ni utaratibu wa kidiplomasia kwa vile Kanisa hilo lina diplomat mission Tanzania (Papal Pronuncio), balozi wa Vatican nchini. Nadhani kwa maelezo hayo nimeeleweka katika kutoa ufafanuzi wa alivyofanya Rais.

Jamani tusiwe negative opposition tu, kwenye mazuri tumpongeze kwani sote ni ndugu, nchi moja na usitawi wa taifa moja, tukishateremka toka jukwaani tunakaa pamoja na kucheza bao, ndio kukomaa kisiasa.
 
Back
Top Bottom