Kwa Hili la Bima ya Afya Kwa watoto-Hapana

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,033
3,916
NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

NHIF Yasajili Wanafunzi 342,933 Bima ya Afya

Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

Uzi huu ambao JF waliufuta amba niliandika mwenyewe kwa ukali kabisa

Nimeambatanisha pia hapa andiko la SERA ya Afya ya Tanzania kwa ajili ya kuipitia

Nimeweka huu uzi tena kwa mtazamo tofauti ili kuhakikisha kwamba Ujumbe wangu wa Msingi haupotezwi kwa sababu ama ya ukali au ukweli wa maneno niliyotumia.Niseme tu zile laana nilizotamka wakati naandika uzi wangu wa awali ni sala ambayo nilisali,ninasali na nitaisali na kufuta tu ule uzi hakuwezi kufanya laana ile iondoke kwa wale ambao niliwatamkia na watatamkiwa laana hiyo na wote ambao wanahusika,Naendelea kusisitiza WALAANIWE,MLAANIWE kwa kutaka kuwatoa watoto KAFARA.

Sisi nirudi kwenye Mjadala

Je sera ya Afya inasema nini kuhusu huduma za BIMA ya AFYA?
Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya Tanzania Sehemu ya 5:10:7 na 5:10:8

Inasema hivi :
Hii ni 5:10:7
"
Tamko la Sera
(i) Mfuko utaongeza wigo ili huduma zitolewazo ziwafikie wananchi wote.

(ii) Mfuko utaboresha huduma na mafao kwa wanachama wake, ili kuwezakulipia huduma za ndani na nje, kwa ngazi zote mpaka huduma zaubingwa maalum.

Hii ni 5:10:8
"Tamko la sera
(i) Serikali itaboresha na kuendelea kusimamia mikakati na miongozoya uchangiaji wa gharama za huduma za afya pamoja na matumizi yamapato yanayotokana na uchangiaji huo.
(ii) Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kubuni njia endelevuza kuchangia gharama za huduma za afya kwa manufaa ya wananchiwote kama vile Bima za Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii."

Hili ni tamko linatoka kwenye sera inayozungumzia hasa BIMA za Afya hasa kupitia Mfuko wa Taifa wa BIMA ya Afya.

Ukisoma sera ya afya utaona pia wamegusia watu wa Makundi Maalum kama watoto wa umri chini ya miaka 5,Wazee juu ya miaka 60 watu wenye magonjwa kama Cancer,Diabates,HIV/AIDS, na magonjwa mengine sugu.

Mimi binafsi ninaamini katik HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE(UNIVERSAL HEALTH CARE) na Ili kufikia hapo ni lazima tuanze na UNIVERSAL HEALTH INSURANCE. Hata hivyo ili kufikia eneo hiloni lazima kwanza gharama za HUDUMA za AFYA na HUDUMA za BIMA ya AFYA ziwe ndani ya UWEZO wa kiuchumi wa wananchi.Swali la kujiuliza ni JE kuondoa huu mpango wa BIMA ya AFYA kwa watoto au kubadilisha utaratibu wa USimamizi wake ni kwa maslahi ya nani?

Kwa mfano,Katika moja ya uzi hapo juu waziri anasema kwamba watoto waandikishwe kupitia shule zao Swali ni JE ni kwa hiyari au ni kwa lazima?Kama ni lazima Je watakaoshindwa kulipia itakuaje?Kama ni hiyari je itakiwa kwa utaratibu gani?Na Je uamuzi huo umezingatia Uhalisia wa hali za Watanzania?

Ushauri wangu kwa waziri na NHIF kwa pamoja ni huu:Shusheni bei ya Hicho kifurushi cha WAtoto na kukiweka katika makundi 2,Kundi la la kwanza liwe la watoto ambao wako shule za msingi na sekondari au wan umri wa chini ya miaka 18 mkifanye kiwe chini ya 50400 then mfanye kwamba ni lazima,Hapo kama mzazi ana watoto wake 4 anaweza kuwakatia wote kwa gharama ya hio 120,000 kama bei ikiwa ni 30,000.Mkiweza hata kufanya iwe chini ya hapo itakuwa vizuri zaidi.Ila 50400 kwa mtu mwenye watoto 4 inamaana tunaongelea 200,000 sio hela rahisi kupata kwa Mkulima wa Jembe la mkono.

Pili Badilisheni kabisa Muundo wa NHIF hasa kuhusu namna wanavyofanya KAZI badala yake watumia MFUMO wa QUOTA kwa hospitali.Hii ina maana kwamba Hospitali zisimamiwe kwa kupewa Quotas na Budget Support kupitia JOINT investment badala ya kukusanya tu PESA na kupokea BILI na KULIPA Hospitali kwa sababu hii inatengeneza mazingira ya Ujanja ujanja hasakutoka kwa vituo vya afya vinavyokosa uaminifu.

Kwa mfano Vituo vidogo vya Afya vinaweza kuambiwa kwamba vinaweza kuhudumia wateja 20 tu wa NHIF kwa mwezi na TOTAL Charges za kila mteja zisizidi Certain Capped Value,The Hospitali kubwa za Binafsi na serikali zinaweza Kupewa Quota KUBWA zaidi ili kuwalazimisha kufanya self checks na monitoring.

Specialist Clinics etc zikapewa QUOTA zake.

Lakini cha muhimu ni kuondoa ubadhirifu ambao unafanyika ndani ya NHIF kwa kuweka mifumo ya wazi ya uwajibikaji.

Najua maoni yako mengi na kama waziri anasomaga anaweza kuangalia yale ambayo yanafaa na kuyachukua na kwa wale ambao wana maoni zaidi wanaweza kuongeza.
 
Attachments

  • Sera ya Afya.pdf
    591.9 KB · Views: 7
Swala la Mfuko wa Bima ya Afya unaendeshwa kwa michango ya wanachama wake ,na unawajibika kutoa huduma kwa wanachama na kuhakikisha uendelevu wa mfuko ili wanachama waliochangia waweze kupata huduma wakati wote ,na unaweza kufanya maboresho ili kulinda mfuko ,kukiwa na utaratibu wa watoto wengi kujiunga kabla ya kuugua kunauwezesha mfuko kumuda gharama ndio maana wanataka watoto wengi kujiunga
 
Moja ya njia pekee ya kuimarisha mfuko ni kusajili wanachama wengi zaidi na ndio maana wattoto wanapojiunga kupitia mashule itakuwa na mafanikio makubwa zaidi na ni njia ya kufikia watoto wengi zaidi ,haiwezekani TOTO toka kuanzishwa imesajili watoto laki 2 kati ya watoto Milion 31 ina maana watoto wengi hawajafikiwa ,lakini pia inapaswa wananchi kuweka umuhimu swala la Bima ,kabla unaweza kuona ni hela kubwa lakini kuna watu wanauza mashamba kugharamia matibabu mpaka Milion 10 na zaidi wakati angekata bima ingekuwa nafuu ,na si kweli kwamba watanzania wote hawana uwezo sema hawana elimu na pia hawajaweka kipaumbele swala la afya ,ni kweli kuna makundi maalum ambayo hayana uwezo hayo yanaweza kufikiwa kwa njia nyengine lakini tujue BIMA ni muhimu na tutaimarisha mfuko tukijiunga kwa wingi kabla ya kuugua na sio mpaka tuumwe ndio tujiunge
 
Swala la Mfuko wa Bima ya Afya unaendeshwa kwa michango ya wanachama wake ,na unawajibika kutoa huduma kwa wanachama na kuhakikisha uendelevu wa mfuko ili wanachama waliochangia waweze kupata huduma wakati wote ,na unaweza kufanya maboresho ili kulinda mfuko ,kukiwa na utaratibu wa watoto wengi kujiunga kabla ya kuugua kunauwezesha mfuko kumuda gharama ndio maana wanataka watoto wengi kujiunga
Jinga kabisa, kodi na tozo zinafanya kazi gani? pesa za kupandishia mishahara wabunge na posho zipo lakini za kutibu watoto wa wawalipa kodi hakuna. Shame on you
 
Hongera kwa Mawazo yako mazuri lakini ukumbuke Mfuko haupewi fungu kuwa endesha hili unajiendesha kulingana na malipo ya wanachama watu walipe pesa hili unazungumza tu nijambo gumu kulifanya wewe unaandika utekelezaji wake ni mgumu sana
 
NHIF Waongeza gharama za Bima ya Afya kwa Watoto, sasa kulipa Tsh. 120,000/= badala ya Tsh. 50,400/=

NHIF Yasajili Wanafunzi 342,933 Bima ya Afya

Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

Uzi huu ambao JF waliufuta amba niliandika mwenyewe kwa ukali kabisa

Nimeambatanisha pia hapa andiko la SERA ya Afya ya Tanzania kwa ajili ya kuipitia

Nimeweka huu uzi tena kwa mtazamo tofauti ili kuhakikisha kwamba Ujumbe wangu wa Msingi haupotezwi kwa sababu ama ya ukali au ukweli wa maneno niliyotumia.Niseme tu zile laana nilizotamka wakati naandika uzi wangu wa awali ni sala ambayo nilisali,ninasali na nitaisali na kufuta tu ule uzi hakuwezi kufanya laana ile iondoke kwa wale ambao niliwatamkia na watatamkiwa laana hiyo na wote ambao wanahusika,Naendelea kusisitiza WALAANIWE,MLAANIWE kwa kutaka kuwatoa watoto KAFARA.

Sisi nirudi kwenye Mjadala

Je sera ya Afya inasema nini kuhusu huduma za BIMA ya AFYA?
Kwa mujibu wa Sera ya Afya ya Tanzania Sehemu ya 5:10:7 na 5:10:8

Inasema hivi :
Hii ni 5:10:7
"
Tamko la Sera
(i) Mfuko utaongeza wigo ili huduma zitolewazo ziwafikie wananchi wote.

(ii) Mfuko utaboresha huduma na mafao kwa wanachama wake, ili kuwezakulipia huduma za ndani na nje, kwa ngazi zote mpaka huduma zaubingwa maalum.

Hii ni 5:10:8
"Tamko la sera
(i) Serikali itaboresha na kuendelea kusimamia mikakati na miongozoya uchangiaji wa gharama za huduma za afya pamoja na matumizi yamapato yanayotokana na uchangiaji huo.
(ii) Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kubuni njia endelevuza kuchangia gharama za huduma za afya kwa manufaa ya wananchiwote kama vile Bima za Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii."

Hili ni tamko linatoka kwenye sera inayozungumzia hasa BIMA za Afya hasa kupitia Mfuko wa Taifa wa BIMA ya Afya.

Ukisoma sera ya afya utaona pia wamegusia watu wa Makundi Maalum kama watoto wa umri chini ya miaka 5,Wazee juu ya miaka 60 watu wenye magonjwa kama Cancer,Diabates,HIV/AIDS, na magonjwa mengine sugu.

Mimi binafsi ninaamini katik HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE(UNIVERSAL HEALTH CARE) na Ili kufikia hapo ni lazima tuanze na UNIVERSAL HEALTH INSURANCE. Hata hivyo ili kufikia eneo hiloni lazima kwanza gharama za HUDUMA za AFYA na HUDUMA za BIMA ya AFYA ziwe ndani ya UWEZO wa kiuchumi wa wananchi.Swali la kujiuliza ni JE kuondoa huu mpango wa BIMA ya AFYA kwa watoto au kubadilisha utaratibu wa USimamizi wake ni kwa maslahi ya nani?

Kwa mfano,Katika moja ya uzi hapo juu waziri anasema kwamba watoto waandikishwe kupitia shule zao Swali ni JE ni kwa hiyari au ni kwa lazima?Kama ni lazima Je watakaoshindwa kulipia itakuaje?Kama ni hiyari je itakiwa kwa utaratibu gani?Na Je uamuzi huo umezingatia Uhalisia wa hali za Watanzania?

Ushauri wangu kwa waziri na NHIF kwa pamoja ni huu:Shusheni bei ya Hicho kifurushi cha WAtoto na kukiweka katika makundi 2,Kundi la la kwanza liwe la watoto ambao wako shule za msingi na sekondari au wan umri wa chini ya miaka 18 mkifanye kiwe chini ya 50400 then mfanye kwamba ni lazima,Hapo kama mzazi ana watoto wake 4 anaweza kuwakatia wote kwa gharama ya hio 120,000 kama bei ikiwa ni 30,000.Mkiweza hata kufanya iwe chini ya hapo itakuwa vizuri zaidi.Ila 50400 kwa mtu mwenye watoto 4 inamaana tunaongelea 200,000 sio hela rahisi kupata kwa Mkulima wa Jembe la mkono.

Pili Badilisheni kabisa Muundo wa NHIF hasa kuhusu namna wanavyofanya KAZI badala yake watumia MFUMO wa QUOTA kwa hospitali.Hii ina maana kwamba Hospitali zisimamiwe kwa kupewa Quotas na Budget Support kupitia JOINT investment badala ya kukusanya tu PESA na kupokea BILI na KULIPA Hospitali kwa sababu hii inatengeneza mazingira ya Ujanja ujanja hasakutoka kwa vituo vya afya vinavyokosa uaminifu.

Kwa mfano Vituo vidogo vya Afya vinaweza kuambiwa kwamba vinaweza kuhudumia wateja 20 tu wa NHIF kwa mwezi na TOTAL Charges za kila mteja zisizidi Certain Capped Value,The Hospitali kubwa za Binafsi na serikali zinaweza Kupewa Quota KUBWA zaidi ili kuwalazimisha kufanya self checks na monitoring.

Specialist Clinics etc zikapewa QUOTA zake.

Lakini cha muhimu ni kuondoa ubadhirifu ambao unafanyika ndani ya NHIF kwa kuweka mifumo ya wazi ya uwajibikaji.

Najua maoni yako mengi na kama waziri anasomaga anaweza kuangalia yale ambayo yanafaa na kuyachukua na kwa wale ambao wana maoni zaidi wanaweza kuongeza.
Bila Michango nhif haiwezi kujiendesha hui mfuko unaendeshwa kwa michango ya wanachama wake ni wajibu wake kutoa huduma kwa wanachama

Lakini pia ni jukumu la mfuko kuhakikisha mfuko unanawiri na wanachama waliochangia waweze kupata bila kikwazo cha aina yoyote
 
Njia kubwa ya kuufanya mfuko uimarike ni kulitia usajili na michango ya wanachama wengi zaidi na ndio maana watoto nhif imependekeza wajiunge kupitia shukeni kwa wingi wao, na ni njia ya kufikia watoto wengi zaidi ,ni jambo la kufikirisha sana tangu TOTO ianzishwe ni watoto laki 2 tu ndio wamesajiliwa kati ya watoto Milion 31 takwimu za Sensa 2020 ina maana watoto wengi hawajafikiwa
 
Je mtoto asie soma au ambae muda w shule kuanza bado inakuaje?
 
Njia pekee na rahisi kuchangia bima ya afya ni Serikali kuanzisha Mfuko wa bima wa kwa wote, insurance fund, itokane na makato kwa simu, makato yasiyo umiza wananchi.
 
Rais , Makamu , wabunge na mawaziru wakipunguza 30% ya posho zao na mishahara.

Serikali ikaacha matumizi yasiyo na tija kwenye ununuzi wa magari na safari za viongozi.

Wakamalizia kwenye matumizi sahihi ya kodi zinazokusanywa.

Hizo bima watoto wanaweza lipiwa chini ya 50400 .
 
Back
Top Bottom