Elections 2010 Kwa hili CCM au makampuni ya simu washitakiwe

Hiki ni kiini macho cha CCM magari walishaagiza hela walipata wapi leo wanakuja na michango huo ni uongo hela walishachota wanachofanya ni kuzuga watu na vyama vya Upinzani
Walikopa benki au kuchota Hazina!!
 
USISHANGAE kama wewe ni mwanaCCM kweli. CCM walifanya mchezo huu wakati wa uandikishaji kura wa pili kwa kupitia kwa wajumbe wa shina (Nyumba kumi). Wajumbe hao walipewa form maalum kupita kwenye kaya zao kandikisha majina ya wapiga kura na kuwaomba pia namba za simu za mkononi. Lakini wakazi hawakuelezwa ni za nini. Kwa wale waliokuwa macho waliwauliza wajumbe hao kadi zao za kupiga kuar zinauhusianao gani na CCM. Binafsi niligundua hilo baada ya kuona fomu hiyo ina nembo ya CCM na si ya serikali au Tume ya uchaguzi.
Hivyo usirukie mambo bila kujua, ma Carl Pieters wapo huko mitaani wakitafuta data zenu!!!
Kuhusu kukatwa hizo fedha inawezekana kabisa, makampuni ya simu yatakata gharama za ujumbe wako. Hii ni njia mpya kuchangisha pesa kutoka kwa wadau. Redio Tumaini, ya Wakatoliki, wame/natumia njia hii kuchangisha pesa za kuiwezesha matangazo yake yawe kwenye satelaiti. Kikuu sasa kuhusu matumizi ya njia hii ni kuwepo kwa regulating and auditing bodies ilikuhakikisha kwanza kodi stahiki inalipwa TRA na haziendi kwenye matumizi mabaya. Ni vyema vyama vingine pia vikatumia njia hii ili kujidhatiti kimapato toka kwa wanachama wao wadogo wadogo ili wachangie gharama.

HAPANA! Mie sijafuatwa na mjumbe yeyote wa nyumba kumi lakini nimepata ujumbe huo. Ni 'ujangili' tu wa CCM huenda wameenda kwenye mitandao na kutuma hizo ziujumbe kwa wote wanaotumia mitandao hiyo.
 
Sasa huku ni kuchangisha au kuomba? Unajuwa mtu anaweza kujiuliza iwapo mwananchi anataka huduma kwa kupitia Serikali na wale wanaoongoza Serikali wanawatoza watu pesa ili wapate nafasi ya kuonoza Serikali, hii si sawasawa na kujilipia huduma za Serikali itakayoingia madarakani?
 
Miaka minnen ya CCM ya KIKWETE, sijaona treni ikipita kwenye reli kiasi kwamba kwenye Railway Cross Road (Check Reail) nimesahau kabisa kuangalia kama nitagongwa na tren au la! Sasa kuchangia CCM tena ni kuwaruhusu waje wang'oe hata hayo mataruma. Miaka mitano ya Muungwana tumeshuhudia bei za vitu zikipanda kama rockets! Hivi bado tuwachangie tena? Bandari zimekufa, sasa waKenya wanajenga uwanja wa Kimataifa wa Ndege karibu kabisa na KIA, sis tunahangaika kwenda kuomba kibali cha kuuza meno ya Tembo , tuna akili kweli?
Kwa hiyo jamani mie nina wasi wasi na bongo zetu, haingii akilini kuona nchi inaenda kombo kiasi hiki , halafu bado tuchangie. Waambie CCM wakachukue kiasi cha pesa kutoka STIMULUS package, au KILIMO kwanza...maana mifuko yote hiyo ni danganya toto tu....
 
I think this is a serious issue. Ni breach kubwa sana ya privacy. Lakini kwa vile ninavyowajua WaTz, hii ishu itaishia hapa hapa! Lakini kusema kweli hii ishu inabidi iongelewe bungeni na hata kuna uwezo mkubwa wa kupeleka watu kadhaa mahakamani! Swali muhimu ni hizi numba wamepata wapi? Kama ni kutoka kwa makampuni ya simu, basi wao ndo wa kushtaki maana wamevunja privacy ya namba za wananchi!
Pia unaweza kukuta CCM wameingia (hack) katika mitandao ya haya makampuni ya simu na kuiba hizi numba! Hii itakuwa ni soo kubwa zaidi, ikiwezekana itabidi hadi uchaguzi uhairishwe. All in all, hii sio ishu ndogo hata kidogo na ningependa kuona inapewa kipaumbele zaidi hapa JF. CCM imezidi ubabe! Sasa njia ni kuwakomesha tu! We have to draw a line. Je tusubiri mpaka wafanye nini ndo tuamke jamani?
 
USISHANGAE kama wewe ni mwanaCCM kweli. CCM walifanya mchezo huu wakati wa uandikishaji kura wa pili kwa kupitia kwa wajumbe wa shina (Nyumba kumi). Wajumbe hao walipewa form maalum kupita kwenye kaya zao kandikisha majina ya wapiga kura na kuwaomba pia namba za simu za mkononi. Lakini wakazi hawakuelezwa ni za nini. Kwa wale waliokuwa macho waliwauliza wajumbe hao kadi zao za kupiga kuar zinauhusianao gani na CCM. Binafsi niligundua hilo baada ya kuona fomu hiyo ina nembo ya CCM na si ya serikali au Tume ya uchaguzi.
Hivyo usirukie mambo bila kujua, ma Carl Pieters wapo huko mitaani wakitafuta data zenu!!!
Kuhusu kukatwa hizo fedha inawezekana kabisa, makampuni ya simu yatakata gharama za ujumbe wako. Hii ni njia mpya kuchangisha pesa kutoka kwa wadau. Redio Tumaini, ya Wakatoliki, wame/natumia njia hii kuchangisha pesa za kuiwezesha matangazo yake yawe kwenye satelaiti. Kikuu sasa kuhusu matumizi ya njia hii ni kuwepo kwa regulating and auditing bodies ilikuhakikisha kwanza kodi stahiki inalipwa TRA na haziendi kwenye matumizi mabaya. Ni vyema vyama vingine pia vikatumia njia hii ili kujidhatiti kimapato toka kwa wanachama wao wadogo wadogo ili wachangie gharama.
Msavila

Umejitahidi ku justify wizi wa CCM kwa njia ya mtandao wa simu kama uko CCM Lumumba vile
 
Jamani leo saa 8:38:10 mchana nilipata ujumbe wa msg kwa simu yangu. unasomeka hivi

"Je unajua unaweza kuchangia maoni yako CCM ilikuimarisha chama chako? Tuma sasa maoni yako kwenda 15016. kumbuka huduma hii ni bure." sender ni CCM.

Hivi maoni yangu watasikiliza hawa kweli? kama ya kina Mwakyembe, na tume nyingi tu yamewekwa kapuni?.

kwa nini hizi kampuni za simu zinaruhusu watume msg kwa watu hata wasio sajiri kupata huduma hiyo. sasa kila mtu akiamua kwenda huko na ku-broadcast msg si itakuwa tatizo.

wahusika zingatieni privacy za watu; kusajiri namba isiwe tatizo.
 
Haya makumpuni tumeyalea wenyewe ndo mana wanakutumia, we have never reacted on this company ndo mana wanakuwa na kiburi cha kutuma, I think utakuwa unatumia VODACOM
 
Serikali ya CCM na wasimamizi wa sera wooote ni CCM. ujue hakuna privacy hapo.
Ninaamini kuwa mahala pekee ambapo utaweka details zako na zikaheshimiwa na kulindwa ni JF pekee na siyo ktk idara za serikali.

Inabidi kuwashtaki tume ya mawasiliano kwa kuruhusu namba zetu kuingiliwa na hawa mafisadi kwa kututumia sms za kuudhi sana.
 
Mie nimepata the same sms. Ina maana kwamba usajili wa namba zetu ni kuingilia privacy zetu eeeh!!!
Mbona wamehakiki daftari la wanachama wa chama chao na kwa nini wasiwatumie wanachama wao pekee?
Kama mimi ni CHADEMA nina lipi ktk kuisaidia CCM? Huu ni umamluki na unapaswa kukemewa kwa nguvu zote....

Kama wewe siyo mwanachama ama mpenzi wa ccm hawana haki ya kufanya hivyo,kwanza this can amount to black mailing,sijawahi kuona chama cha kisiasa kikienda kuomba michango kwa wananchi wasio wanachama wake,hili ni suala la kutupiwa macho kwasababu siasa zetu zilivyo ni sawa na kuwaogopesha wananchi kwamba we know you dont support us etc.
 
Mie nimepata the same sms. Ina maana kwamba usajili wa namba zetu ni kuingilia privacy zetu eeeh!!!
Mbona wamehakiki daftari la wanachama wa chama chao na kwa nini wasiwatumie wanachama wao pekee?
Kama mimi ni CHADEMA nina lipi ktk kuisaidia CCM? Huu ni umamluki na unapaswa kukemewa kwa nguvu zote....

Serikali ya CCM na wasimamizi wa sera wooote ni CCM. ujue hakuna privacy hapo.
Ninaamini kuwa mahala pekee ambapo utaweka details zako na zikaheshimiwa na kulindwa ni JF pekee na siyo ktk idara za serikali.

Inabidi kuwashtaki tume ya mawasiliano kwa kuruhusu namba zetu kuingiliwa na hawa mafisadi kwa kututumia sms za kuudhi sana.

Ha ha ha well detailed point,i like it
 
Utamaduni wa kusikiliza maoni ya walalahoi wameanza lini ? Na bado watatutumia na za kutuamkia kila asubuhi ili mradi tu waturubuni tuwape kura.
 
Nafikiri ni vema tukaangalia taratibu za kisheria zikoje juu ya hili. Kwa wale wanaoishi NJE ya TZ, wanaweza tupa uzoefu na huko kwao mambo yakoje.

Hizi Directory za SIMU ni sawa na Directory za SIMU za nyumbani. ambazo TTCL huwa wanatoa litabu kuubwa la Yellow pages. Makampuni mengine huwiita White pages..whaterver the name...lkn Kampuni za simu huwa zinatoa hizi no.za simu...

Nafikiri hii ni biashara ambayo makampuni mengi ya simu yanafanya, na siku hizi inaitwa SMS Marketing, unaflood sms kama vile wanavyofanya wataalam wa SPAM...kuwatumia emails watu wasiowajua. The good thing ya Email SPAM unaweza iblock, ktk sms kidogo kuna kazi....labda na uwe special phone, yenye special software kufilter sms.

Wakati mwingine watumaji wa SPAM SMS, ni wale ambao tumezoea kuwapa Business Card zetu...Baadhi ya watu hukeep hizi Business card na anapokuwa na haja, basi hurusha sms hizo au Ulijiandikisha wakati fulan wa business promotion or...whatever... Inawezekana pia kwa utaratibu huu, CCM wameweka vijana wao maalum wa kutafuta no.za simu ili kuwatumia Ujumbe Changia...so thru friends basi database yao inajaa. Assume kila mpenzi au mwanachama makini wa CCM aamue kusubmit PHONE directory ya simu yake...itakuwaje? ktk Maisha haya unajikutana unarafiki CCM, Chadema, CUF au vyama vingine au waso na chama kabisa. In this uwezekano kupokea sms usoitarajia ni mkubwa sana....Chukulia tu Kila Mjumbe wa Nyumba 10 ambae anamiliki simu au kijitabu chake anaandika simu za wake atashindwa kuwapa CCM?..
 
Back
Top Bottom