Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Kwa maoni yangu, hali ya muungano inaendelea kuwa mbaya. Wanaosema muungano ni imara ni viongozi tena wa chama fulani. Chuki ya wananchi wa pande hizi mbili inaendelea kukua. Sasa kwa mwenendo huo nawaonya viongozi wa hicho chama fulani wasije wakalogwa na kusema sasa ni zamu ya visiwani, wataangukia pua na watajuta. Siasa za nchi hii chini ya uongozi wa sasa zimekuza ufa kati ya bara na visiwani. Wabara hawatakubali kudanganywa tena.