Kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kabisa kuwa Paul Makonda atajiuzulu au atatenguliwa!

Vita ya madawa ya kulevya ipo pale pale, waambieni madoni wenu wa madawa waliowatuma kupunguza makali wamefeli, tutapigana vita to our last breath


Na so far, wakimpoteza mmoja kutoka kwetu tutahakikisha tunawaondoa wa kutoka upande wao kumi
 
Vita ya madawa ya kulevya ipo pale pale, waambieni madoni wenu wa madawa waliowatuma kupunguza makali wamefeli, tutapigana vita to our last breath


Jamani huyu jamaa anatia huruma sana ,Tumsamehe kama taifa kwani hiyo video mwisho makonda analia kwa uchungu sana.
 
SHIDA SIYO KUJIUZULU AU KUMTOA NAFASI YA U-RC, LAZIMA AFIKISHWE MAHAKAMANI NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE KWA KUGUSHI VYETI.
MFANO KUNA DADA KAHUKUMIWA JELA MIAKA 28 KWA KUGHUSHI VYETI,SASA HUYU KWAKUWA NI KIONGOZI AWE MFANO HUKUMU IENDANE NA SIFA ZAKE PIA YAANI MIAKA NA FINE ZA KUTOSHA.
VINGINEVYO NAYE PIA ALIYEMTEUA AWAJIBIKE NA KUJIPIMA KUWA ANAFAA AU LA KWANI NI NANI ALIYEFANYA VETTING YA HAWA BASHITE NA NI KWANINI ALIMTEUA MTU WA NAMNA HII?
SHERIA IWE NI MSUMENO NA SIYO KWA MASIKINI AU WATU WA CHINI TU IWE KWA WOTE.
 
Flaud mbaya sana. Nakumbuka maneno ya mkuu Wa kaya anavyosema kuhusu vyeti feki na udanganyifu uliofanyika kwa baadhi ya watendaji.
 
Hiyo ni theory, andika practicality yake. Taasisi husika ilikuwepo miaka yote ya Kikwete, ilifanikiwa. Kama ulikuwa mfuatiliaji wa matukio, kumbuka Reginald Mengi alivyohangaishana na wakubwa wa taasisi hiyo. Mbinu ya kawaida haikufanyakazi miaka yote hadi watu wanakamatwa airport, usoni remorselessness. Hapo tunahitaji unorthodox method. Period!

Ukianza kuleta theories sijui za taasisi, sheria za nchi, sijui oohh Bashite! bla-bla kibao wakati unaona njia yake ndo imeliamsha taifa ktk hilo, then kuna tatizo kwako!
Taasisi ilikuwepo Lkn nadhani kwa kuwa wewe ni mfuatiliaji wa matukio ulimsikia mh RAIS Magufuli kuwa sheria mpya ya madawa ya kulevya ilipitishwa 2015 ambayo ndiyo inayoipa nguvu serikali kushughulikia kikamilifu wafanya biashara wa madawa.na nadhani ikiwa bado una kumbu kumbu ni kuwa tangu kamanda Nzowa amalize muda wake nchi imekuwa haina Kamishna wa madawa ya kulevya. Na nadhani wakati wa kamanda Nzowa magwiji wa wakubwa wa madawa ya kulevya walikamatwa ikiwemo Yule mama aliyekuwa anatafutwa mpaka Na wamarekani. Pia mtoto wa LIYUMBA pia alikamatwa Na Sheena kubwa ya madawa . Japo hatukatai watumiaji Na wauzaji pia wameongezeka Hili sio tu kwa Tanzania Bali ni kwa ulimwengu.

Nadhani makonda Angelikuwepo wakati wa Kukamatwa kwa Mtoto wa Liyumba au Yule mama wa Mbezi angetangaza "NASIKIA mtoto wa LIYUMBA anakuja Na madawa Na atatua mtwara basi tunamsumbiri" au "au wewe mama unayetafutwa Na wamarekani tukutane polisi ijumaa" huu ni zaidi Ya UJINGA ndugu. Kuna kipindi ktk maisha inabidi tutofautiane Na hata tunaowapenda pindi wanapokosea. Au Huyu mtoto wa liyumba alikamatwa kwa kutangaziwa kwenye . ?

Lkn nadhani Ili ukubaliane Na njia aliyotumia BASHITE kupambana Na madawa kwa kuwaita mateja (rocky, rid, tunda, nk ) hadharani kwa kutumia vyombo vya habari Ili wawatajie ni nani wanaowauzia inabidi kwanza UJIJAZE UJINGA KICHWANI :(:(:mad::confused: Ili ukubaliane nae kuwa ni sahihi au yupo sahihi. Ni sawa Na kujua Juma alikuwepo sehemu Na akashuhudia mauaji na kiukweli Juma anajua wauaji kwa majina , halafu mpelelezi mwenye weledi akatangaza hadharani Juma njoo kituoni unitajie ALIYEUA. MPELELEZI itakuwa mwandawazimu Na Juma atakuwa kichaa akitaja MUUAJI.
 
Same to Gwajima, anatafuta cheap popularity, huwezi sema una ushahidi wa mtu ana cheti feki halafu haujakiweka hadharani wiki ya pili sasa, wala haujaenda kushitaki kwenye mamlaka husika ya necta ili wamchukulie hatua.

Cheap popularity ya kutafuta waumini wengi zaidi maana jana watu wengi walienda kanisani kwake wakisubiri ataongea kuhusu cheti feki ambacho hana ndio maana hawezi kukiweka hadharani, sadaka iliongezeka., umaarufu wa kanisa unaongezeka maana huwezi kumtaja gwajima bila kanisa lake, hata asiye lijua atalitafuta.

Yeye Gwajima aliwaji kujibu tuhuma zilizomkabili za kuvunja ndoa ya Mbasha kwa yeye kutembea na Flora?

Alifika na style ya misukule akaona haikumpa popularity, na hata hili la bashite sijui dadui halitampa popularity ya kuongeza waumini, atawapata wavivu wa kusoma Biblia ambayo imetoa angalizo ya siku za mwisbo manabii wa uongo wataongezeka, kazi kuchumia matumbo badala ya kufanya kazi ya Mungu.

Suala la bashite Gwajima analitumia kutafuta cheap popularity.

Na laana ya kumtukana Kardinali pengo inamuandama pia gwajima
Hoja iliyoko hapa haina uhusiano na gwajima...
 
Vita ya madawa ya kulevya ipo pale pale, waambieni madoni wenu wa madawa waliowatuma kupunguza makali wamefeli, tutapigana vita to our last breath


Vita ya madawa ya kulevya inaenda sambamba na uhakiki wa vyeti na sheria zichukue mkondo wake.
 
MIMI BINAFSI SIJAPENDEZWA NA VITA YA YULE JAMAA YA KUWASOMBA WASANII HADI KISUTU KISHA HUKUMU IKAWA NI KUOMBA MSAMAHA NA KUCHUNGUZWA TABIA MWAKA MMOJA,NA SIDHANI KAMA KUNA MTU ATAKAYEFUNGWA KATIKA ZILE LIST ZAKE,PILI KUNA WENGINE ALIWATAJA KWA UONEZI MFANO GWAJIMA NA POLISI NA MKEMIA WA SERIKAL ALITHIBITISHA HAWATUMII,SASAAAAA WALE ALIOWAONEA NADHANI NDO WANAKOMAA NAYE.NA VITA YA MADAWA ITAENDELEA SIO KWENYE MEDIA LAKIN KUNA WATAALAM WAPO WAMECHAGULIWA
 
Huyu jamaa alishawahi kupita kule kahore nini maana anacharactet zote za usani
 
Vita vya madawa ya kulevya viko pale pale; na pia vita ya kuwashugulikia wenye vyeti vya kufoji nayo iko pale pale. Moja ya vita hizo mbili haitatumiwa kama kisingizio au scapegoat ya kuonewa huruma na wananchi.
 
Vita ya madawa ya kulevya ipo pale pale, waambieni madoni wenu wa madawa waliowatuma kupunguza makali wamefeli, tutapigana vita to our last breath


Vita ya madawa iendelee tu tena kwa kasi ya kamatakamata na vyeti tuwekeeni jamani kwani shida nini?
 
Alichelewa kanisani, akaomba awakilishwe kwenye mapokezi.
Mmmmh! labda aliogopa asije atatumbuliwa kwenye mapokezi hayo maana mkuu wa kaya mwenyewe hatabiriki. Akubali tu hata wale waliotumbuliwa walikuwa na moyo unaoogopa na kuuma kama yeye!
 
Back
Top Bottom