Kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kabisa kuwa Paul Makonda atajiuzulu au atatenguliwa!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,059
24,452
Hili suala la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam limefikia mahali pabaya!

Wapo watu wanaoamini kuwa limepoa na litapita, lakini ni kwamba kwa namna ambavyo ukweli unavyozidi kutafutwa ni dhahiri kabisa kuwa mambo makubwa zaidi yatabainika na kuwekwa hadharani!

Naamini mda mfupi ujao lazima atajiuzulu au utatenguliwa na bila shaka sheria itachukua mkondo wake!
 
kwa siasa za hapa za ukada na kujuana ataendelea kuleta maajabu na matukio kila uchao na 2020 atapewa uwaziri mkuu
Haitoweza kutokea..
Kwanza japokuwa alikuwa kashatengeneza mazingira ya kugombea ubunge ni kwamba ndoto zake za kuingia bungenu zimeyoyoma...
Sifa za kugombea ubunge keshapoteza na hata akipitishwa haitakuwa rahis kuchaguliwa tena kutokana na hii kashfa!
Lakini pia ashukuru kama hiyo 2020 itamkuta uraiani, huyu mtu inabidi awekwe korokoroni!
 
Haina haja kumhurumia huyu, aliwadhalisha watu na taaluma zao madokta na mainjinia, mara akajiita mungu!
Its tit for tat...

Kwa kweli amedhalilisha sana watu, na mbaya zaidi amemkufuru Mungu. Muda sio mrefu Mungu wa kweli atamshusha tu. Yeye baada ya kujibu tuhuma zinazomkabili, anakimbia huku a kule na kudai anasakamwa kwasababu "anapambana na madawa ya kulevya." Nachelea kusema kwamba tuhuma zinazomkabili zingekuwa sio kweli angeshajitokeza asubuhi na mapema na vyeti vyake halali ili kuonyesha waandishi wa habari, na mjadala ungeisha, basi! Na yule Boss wake "msema kweli mpenzi wa Mungu" bado ame kaa kimnya tu, baada ya kuchukua hatua...nashangaaa ni upenzi wa Mungu gani huu unaleta upendeleo dhahiri kabisaaa!!
 
Back
Top Bottom