Kwa hali ilivyo sasa, ccm inajichimbia kaburi kwa kuendelea kumhifadhi Rostam

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu wanaJF,
Sasa imedhihirika waziwazi kuwa adui namba moja anayeifilisi nchi hii ni ccm. Chama hiki ndiyo kimekuwa mwavuli wa kufunika uovu na waovu wote wanaoifilisi nchi yetu na kusababisha mateso makubwa kwa wananchi. Chama hiki ndicho kinacholea watu waina ya Rostam na kuwatetea kwa maneno ya kila aina ili waonekane mbele ya wapiga kura wao kuwa ni watu wazuri. Pamoja na jitihada hizo za kufunika uovu unaofanywa na wanachama wao ambao ni mafisadi papa, wananchi hatimaye tumeweza kubaini uovu huo na vinara wao.

Sasa ccm ichague moja kati ya haya mawili, ama ikubali kufa kifo cha aibu kwa kukubali kuendelea kumhifadhi Rostam au kimtimie Rostam kutoka kwenye chama. Vinginevyo, moto utawaka na kuishangaza Dunia.
 
Baadhi wanatamani atimke lakini wanajiuliza kwa namna gani ataweza kutoka ikiwa amejijengea himaya kubwa ndani ya chama kwa kutumia kodi zetu kiasi cha kuonekana ndo mmliki wa chama na serikali.
 
Ndugu haiwezekani CCM kumfukuza Rostam; ni chanda na pete hawa jamaa. Ni rahisi kwa mbingu kupita kuliko CCM kufanya hvyo. In fact binafsi nadhani kumfukuza huyu jamaa ni hatari zaidi kuliko kuwa naye - anafahamu siri zote za nchi hii - kuanzia ikulu, jeshi, mfumo mzima wa sheria, bunge, media, ..., n.k. yaani kwa ufupi ni mafia. Usishangae nyaraka zote muhimu za nchi hii kazihifadhi anakojua yeye huko nje pengine hata mikononi mwa magaidi.

Hii thread inanikumbusha wale jamaa wa Taliban walivyokubali bora kufa kuliko kumtoa Osama wakidai ni "mgeni" wao; Mullah Mohamed Omar aliwahi kutamka hadharani ni mgeni wao aliyeletwa na Mwenyezi Mungu hivyo wasingeweza kumtosa hadi leo hii wako naye - CCM na Rostam nao vivyo hivyo pengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom