nafikiri kauli mbiu iwe KILIMO NA VIWANDA,na tuwe na viongozi ambao ni committed,wazalendo wenye uchungu na taifa hili.waliopo sasa ni wasanii,kilimo kwanza kinaubiriwa kempinsy hotel pamoja na kunywa mvinyo.
Fikra,siasa na sera hizi zinazo tumiwa na viongozi na kuwaaminisha watanzania zitaifanya Tanzania ibaki maskini na tegemezi milele.
Leo nimekumbuka tangia nianze kusoma huko primary nilifundishwa kuwa KILIMO NI UTI WA MGOGO WA TAIFA. Mpaka leo nimemaliza kidato cha nne bado ninaambiwa kauli, fikra na sera hiyo hiyo.
Najiuliza kama kilimo ndo uti wa mgongo mbona mpaka leo maskini wengi ni wakulima?
Kama tunategemea kilimo sasa tutashindanaje na mataifa mengine na je hii si inaendelea kutufanya tegemezi wa watu wenye viwanda ambao wao ndo wanapanga bei?
NADHANI NI WAKATI MUAFAKA WA KUSEMA UTI WA MGONGO WA NCHI YETU NI VIWANDA KULIKO KILIMO.
Jamani MODS siyo kila post iweinakabalika hapa jamvini!Sasa huyu sijui form four leaver ameandika nini upupu tu.Anaijua tanzania,hajui maana ya sera,uelewa mdogo sana,tatizo shule za kata.Ukiangalia post zake hazina ata mashiko ndo maana nilikuwa ni mesusa kuja Jf bwana ondoa hizi post za huyu form four.
Nadhani mtaongea weeeeee, lakini haina tofauti na hadithi ya nyani na mpango wa kujenga nyumba.Program zipo nzuri tu, tafiti zimefanywa nyingi tu. Tatizo letu la msingi ni moja tu, UMASIKINI WA AKILI. Tukiweza kujitambua kwamba sisi ni wanadamu kama wao, tuna uwezo wa kufikiri kama wao, tuna uwezo wa kujilisha na kulisha wengine kama wao. Na zaidi ya yote tuna umuhimu mkubwa katika hii dunia zaidi yao. Hapo ndipo ukombozi wa kweli utakapofikiwa. Una taifa lenye ukubwa wa km za mraba 900,000 na ushee, ardhi yenye rutuba, bahari, maziwa yote makuu barani africa, hakuna majanga makubwa ya kidunia kama matetemeko, vimbunga, tsunami n.k. Madini yaliyopo ardhini, mamilioni ya tani. Madini yote yenye dhamani kubwa duniani unayo. Una gesi, mafuta, uranium, coal, joto la ardhi, upepo, jua mwaka mzima, hakuna snow, hakuna jangwa, popote ukilima unapata chakula, above all una hazina ya watu 40 millioni.
Pamoja na kupewa vyote hivyo, kwa akili nyingi sana tulizonazo tunaenda kuomba msaada Sweden nchi ndogo kuliko mkoa wa kilimanjaro, yenye watu 10% ya watu wako - Shame!
VIJANA NDIO TEGEMEO LA MABADILIKO YA KIFIKRA NA KIMAENDELEO, TUSIPOSHIKAMANA NA KUONDOA HAWA VIONGOZI WAZEE WALIOCHOKA KIFIKRA NA CHAMA KILICHOPOTEZA DIRA, TUTAENDELEA NA UMASKINI NA KUITWA MASIKINI WANAOLALIA VITANDA VYA DHAHABU. WAO WAMEWEZA WANA NINI, TUACHANE NA NYIMBO ZA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE! TUTHUBUTU KWA KUJITEGEMEA KIVITENDO (SI KWA FIKRA ZA JK), TUTAWEZA, NA TUTASONGA MBELE. TUJIKOMBOE WENYEWE KUTOKA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI, HAKUNA WA KUTUKOMBOA ILA NI SISI WENYEWE! BY LATE BOB MARLEY.
Jamani MODS siyo kila post iweinakabalika hapa jamvini!Sasa huyu sijui form four leaver ameandika nini upupu tu.Anaijua tanzania,hajui maana ya sera,uelewa mdogo sana,tatizo shule za kata.Ukiangalia post zake hazina ata mashiko ndo maana nilikuwa ni mesusa kuja Jf bwana ondoa hizi post za huyu form four.
Isee haya sijui tutafikaje huko tusikokujua
Kwa Tz bado kilimo kiwe uti wa mgango, kwa nini? Nchi nyingi zilizoendelea zilianzia kwenye kilimo na mali ghafi walizokuwanazo kama vile chuma, mkaa wa mawe nk. mali ghafi hizi ndizo zilizowasaidia kuanzisha viwanda vidogovidogo na baadae vikawa vikubwa kutokana na mahitaji ya watumiaji. Najiuliza, tukihamia kwenye viwanda, mali ghafi zitatoka wapi wakati hatujajiandaa? Viwanda vichache tulivyonavyo kwa kiasi kikubwa vinategemea mali ghafi toka nje ambazo zinatumia fedha za kigeni kuziagizia, kwa mfano, viwanda vya Bakharesa vinaingiza nafaka toka nje, TBL inaagiza shairi toka nje, viwanda vya magodoro, hata vya plastic vinaagiza plastic toka nje, vya mafuta ya kula, nk. Wakati ardhi tunayo tele ya ziada. Mie naona tujikite zaidi katika kilimo, kwa jinsi tutakapozalisha mazao kwa wingi kama vile pamba, shairi, alizeti, nafaka, mpira na mengineyo ndivyo ambavyo wawekezaji wataamua kuanzisha viwanda humuhumu nchini kwa kutumia mali ghafi zilizopo kwa vile hata gharama za uzalishaji zitakuwa chini (tuondoe tatizo la umeme na bei pamoja na urasimu ktk uwekezaji). KILIMO KWANZA bora tuwe na malengo ya masoko na kuondoa fikra zilizopitwa na wakati.
Tunahitaji viongozi walio na mtazamo wa kuona mbali na sahihi ili kubadilisha hali ya mkulima wa Tanzania. Hatuhitaji misemo, hatuhitaji majigambo bali vitendo. Hebu fikiri kidogo iwapo kiwanda cha ngozi kitaweza kuzalisha viatu kwa wanafunzi na walimu wao, majeshi yote, mikanda ya suruali, mikoba ya akina mama, mabegi na masanduku. Je, utakuwa umewaondoa watu wangapi katika umaskini? Fikria iwapo tutakuwa na viwanda vya nafaka ikauzwa nadani na nje ya nchi. Fikiria iwapo kilimo chetu kitaacha kutegemea mvua bali umwagiliaji. Fikria viwanda vya nyama kama cha Kawe walichoua. Fikiria viwanda vya nguo, zikavaliwe hapa kwetu. Bila shaka umaskini wa mkulima unalelewa na viongozi tuliowaweka madaraknani. Umefika wakati wa mkulima kusema HAPANA sasa imetosha.Viongozi wetu wanendekeza vitu vya wageni lakini vya hapa hawavitaki. Hebu fikiria samani maofisini wanataka za Ulaya lakini za JKT na Magereza hawazitaki. Tuukomboe uongozi kwanza. Tupate uongozi utakao badili mifumo ya sasa hivi na kuleta mifumo yenye kuliangalia Taifa kwanza. Then Umaskini utafutika.