kwa aliye-SINGLE TU.

Kisiya Jr.

Senior Member
Nov 21, 2011
102
29
Habari zenyu wanajamvi.
Kusema kweli hili jukwaa na Love Connect binafsi naliheshimu mno,naamini litasuluhisha hitaji la mtima wange. Ni Siku nyingi nimekuwa nahitaji kufunguka nami nimpate ndege,Ila kwa mentality za wanajamvi nimeshindwa ndio maana Leo nimeamua kuja na Uzi huu kwanza ili nikipata majibu ndo nikajipange
Binafsi naamini kila binadam anapenda kupendwa bila kujali hali yake ya kiuchumi wala kielimu au kasoro yoyote ile. Hapa jamvini wanatafuta wenza sifa zao kubwa ni;
1.Pesa
2.Kazi
3.Elimu
4.Mvuto.

Leo naomba niongelee kidogo pesa. Ninavoona Mimi watu wanaingia kwenye mapenzi wakiwa na mentality za spending only ndo wanahisi watadumu...stupid!
Kwa mfano flesh graduate wa chuo hapa kwa men hawezi kupata mpenzi,kisa hana kazi hivyo hana hela. Wanawake wengi bado wanahisi wenyewe ni watumiaji tu sio wataftaji,hawezi kukaa na kijana kama Mimi tukajipanga nae tukatengeneza maisha na kuwa historia ya mafanikio.
Badala yake wanapaka wanja na kwenda milangoni kwenye nyumba za starehe ili wanaume waje wawaokote na kuwaingiza ndani.
Leo simalizii....
 
kwa mfano flesh...fresh..
umekuja na gia kuukuu kweli.....
haya twakusubiri......
 
khaaaa!! hivi kweli bado kuna wanawake wenye mentality ya spending tu dunia hii ya sasa hivi ambao wanategemea mkwanja kutoka kwa kidume?. Thanx God kwa kunipa mwanamke mchakalikaji na anayejua nini maana ya maisha ya kusaidiana. Kwahiyo mleta uzi unamaanisha unataka hapa jamvini ajjitokeze mwanamke akupende hivyo hivyo kutokana na sifa zako ulizozielezea au vipi?
 
Habari zenyu wanajamvi.
Binafsi naamini kila binadam anapenda kupendwa bila kujali hali yake ya kiuchumi wala kielimu au kasoro yoyote ile.....

Mapenzi hayao utayapata kwa aliyekuzaa tu, hata nao pia wanaangalia siku hizi. Lord have mercy!
 
...............................Kwa mfano flesh graduate wa chuo hapa kwa men hawezi kupata mpenzi,kisa hana kazi hivyo hana hela. Wanawake wengi bado wanahisi wenyewe ni watumiaji tu sio wataftaji,hawezi kukaa na kijana kama Mimi tukajipanga nae tukatengeneza maisha na kuwa historia ya mafanikio.........
Acha longolongo zako mkuu, MKONO MTUPU HAULAMBWI.
 
halafu jamaa kasema" kijana kama mimi" ina mana hana kazi au kipato kinachoeleweka?aacha longo2 wanaume kazi yetu kutunza familia bila hivyo heshima hupati ndani
 
halafu jamaa kasema" kijana kama mimi" ina mana hana kazi au kipato kinachoeleweka?aacha longo2 wanaume kazi yetu kutunza familia bila hivyo heshima hupati ndani

Oya mwanamke ni mtu kama wewe,Ana wajibu na majukum sawa kama wewe. Tofauti yenu ni jinsia tu,heshima haipatikani hivo unavofikiria.
 
khaaaa!! hivi kweli bado kuna wanawake wenye mentality ya spending tu dunia hii ya sasa hivi ambao wanategemea mkwanja kutoka kwa kidume?. Thanx God kwa kunipa mwanamke mchakalikaji na anayejua nini maana ya maisha ya kusaidiana. Kwahiyo mleta uzi unamaanisha unataka hapa jamvini ajjitokeze mwanamke akupende hivyo hivyo kutokana na sifa zako ulizozielezea au vipi?

Sip Mimi tu hata mwenye pesa angetamani apendwe vile alivo na sio pesa au elimu alokuanayo.
 
Kundi la wasema ukweli???? Niweke tu.

Hahaha eti la wasema ukweli?? Wanawake wengi wenu mnajifanya pesa si issue kubwa ila nyuma ya pazia ndo mpango mzima. Au ndo yale mambo ya ukipanda mti unapata kivuli so ukipanda wa matunda unapata kivuli n matunda. Au sio..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kijana women want a man that will enable them to have fun. sasa hiyo fun sio kumegana. it means going out to different places enjoying different hobbies na kadhalika. sasa hivyo bwana unavipata pale tuu unapokiwa na hela so hela ni important .
 
Mapenzi hayao utayapata kwa aliyekuzaa tu, hata nao pia wanaangalia siku hizi. Lord have mercy!

mwambie huyo...mwanamke atakupenda koz una kitu fulani. madamex jamani mie waniacha hoi na ukweli unaowapaga hawa watu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom