Kwa aina hii ya wanawake tulionao sasa hivi ni sahihi kweli?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,117
Kama ikitokea umeachishwa kazi (kibarua kimeota nyasi ) basi siku hiyo hiyo ukirudi nyumbani umwambie? Au ni bora tu uuchune na umchezee filamu ya kaole kwa kujifanya na wewe asubuhi unaenda mjini kisha unaenda kukaa kwa masela kijiweni na jioni unajirudisha kitaa?

Manake kwa aina hii ya hawa mademu au wake zetu kama akina nifah ukiwaambia tu huna ajira tena au kibarua kimeota nyasi utadharauliwa na kukanyagiwa hadi uone dunia hii chungu.

Naombeni michango yenu katika hili na karibuni tuchangie.
 
ukweli siku zote ndio utakuweka huru. universal principle.


Usiruhusu kuingia katika vifungo vya nje ili kumfurahisha mwanadamu. hata hao matajiri pia tunasikia wake zao wanafanya mapenzi hadi na wakata majani.

crisis is the ultimate measure of true friendship/relationship
 
Solution nikumwambia kwan hakuna cha ajabu hapo. Na ukiona hii inatokea ujue ni kwa wale ambao hawajakomaa kimahusiano na walikutana juu juu pasi kupitia shida za maisha.
 
kwa pesa usiwalaumu kina dada tu hata ndugu zako kama huna pesa heshima inapungua yaani dunia ya sasa mwenye mapenzi ya kweli ni mama yako mzazi tu baaasi, hao wengine ukiwaona wapo karibu na wewe ujue wapo after something, hata washikaji wa kweli utakuja wajua unapofulia.
 
The safest bet ni kujiimarisha tu kwa saving na investing. Ili hata ikitokea kazini wamekuzingua, usipate tabu.
 
Back
Top Bottom