Kuzuia wimbo wa chura, ni kuzuia uhuru wa wananchi, ni uonevu na Unyanyasaji

Ninajiuliza suala la kupinga huu wimbo wa chura ni kuzuia uhuru wa wananchi kufanya wanachotaka au ni kuvuka mipaka ya uhuru uliopo kikatiba. Tukiwaacha hawa na wafanyao, tutaathirika vipi? Hiyo ndio kazi ya rasilimali chache tulizonazo? Kwa msio ufaham wimbo huo fikeni YouTube unaitwa chura. Nchi hii wananchi wake wanapenda sifa

Una umri gani kiakili, hata ushindwe kung'amua tatzo katika wimbo na video yake dhidi ya jamii yetu ya kitanzania?
 
Nilikua nairudia hii video ya Marehem Chura wa Snura niangalie Hicho kinachoitwa utovu wa nidham na Uvunjifu wa Maadili!!Mbona kuna video za hivi nyingi Sugua gaga,diamond Ule wa mahadhi ya taarab!!na nyingine nyingi ! Sijakiona cha ajab kwenye Chura au kilichozidi zaidi ukilinganisha na...

1.Video nyingine za bongo ambazo wamekua wanakata mauno hasa za miondoko ya hivo

2.video za nyimbo za nje kama Marekani ambazo zinapgwa kwenye runinga zetu

3.Post za Picha za uchi na video za wa bongo wanazo advertise Instagram,Facebook au Whatsapp

Unafungiaje wimbo kama huu ambao n afadhali wakati kuna access ya porngraph internet 24hrs,kuna baikoko live,kanga moja live na YouTube tena ni Bongo!! Hivyo vyote bado vipo na vinatazamwa deilee na ndivo vinaharibu jamii??
Mawazo yangu tu!!
Labda wengine mniambie
 
181b72064889504f88e7e20508423cc5.jpg

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ni si kongwe kama ilivyo BASATA, lakini pamoja na kuongozwa na wasomi na watu wenye uzoefu mkubwa lakini matokeo ya utendaji wao aidha umekuwa butu wa makengeza au usiokidhi viwango vya kile kilichotegemewa kutoka kwao.

Tasnia ya sanaa Tanzania inakua kwa kasi, sasa ni ajira rasmi inayotegemewa na wengi...! Kazi ya kutengeneza mziki mmoja au filamu hujumisha utaalam tofauti ambako kote huko watu hupata kula yao.

Kumekuwa tabia ya mlipuko wa kufungia kazi za wasanii kutoa adhabu baada ya hapo kimya.

Lakini hawa wana jukumu kubwa sana la kusimamia hii tasnia muhimu
Waunde sasa chombo cha kuratibu kazi zote za sanaa kabla ya kurushwa hewani, hiki chombo ndio kitakuwa na jukumu la kuangalia mapungufu ya kazi yenyewe na kuona kama inafaa kuwapelekea walaji kulingana na mila tamaduni na desturi zetu.

Wasanii wengi ni vijana chini ya miaka 30 wanaohitaji miongozo ya kila aina, wana vipaji lakini wanakosa uzoefu na hata hekima kwenye mengi...pesa zao wanapata kwa shida Sana hivyo ni vema wakapata chombo cha kupitia kazi zao kabla hawajazitoa ili kuepuka hasara kama hizo za kufungiwa.

Kutegemea wasimamizi binafsi na waongozaji haisaidii kwakuwa tumeona mara nyingi makosa yakijirudia.

Isaidieni Tanzania wasaidieni vijana wetu waweze kusimama tokeni ofisini undeni chombo cha kuratibu kazi zao kabla hazijatoka hili ni jukumu lenu nyie
2627c4496add88632358adc380447313.jpg
 
Badili kichwa cha habari kwanza na uandike kwa kiswahili fasaha,nitarudi baadae kuchangia.
 
Ebu nirekebishe nilipokosea AF nitabadili kwa sabab napenda kujifunza zaidi
Naona umesharekebisha Kichwa cha habari ila umekuja na makosa mengine tena hapo kwenye red!!

Kuhusu kichwa cha habari imebaki hapo kwenye iliikua toa i moja ili isomeke ilikua
 
Naona umesharekebisha Kichwa cha habari ila umekuja na makosa mengine tena hapo kwenye red!!

Kuhusu kichwa cha habari imebaki hapo kwenye iliikua toa i moja ili isomeke ilikua
Bila shaka wewe ni HKL!! upo sensitive sana kwenye Makosa ya Kisarufi kuliko Maada
 
Picha mbalimbali za video ya wimbo wa chura
4a764bd5a2835b8673493daf3a6a5152.jpg
815d16df669a23da925e8f643f51d7af.jpg
5d2256e3eab2f35d6ca03c4697fccec3.jpg
0209e30789d38a03743075d6e29d7a45.jpg

Wimbo kama huu kama kungekuwa na chombo cha kuratibu picha zilizokosa maadili kama hizi zisingeweza Kuwekwa kwenye video badala yake zingwwekwa picha za chura halisi au vikatuni
 
hahahaha takataka kabisa na uchafu katika jamii .....
hivi snura ni mchaga wa wapi huyu, angemtafuta hata kakake ney wa mitego ampe maujanja ya kutokea lol
 
Jamani churaaa...afu basata mna wivu... hivi kwenye simu zenu tukizikagua hatumkuti chura kweli.?
 
181b72064889504f88e7e20508423cc5.jpg

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ni si kongwe kama ilivyo BASATA, lakini pamoja na kuongozwa na wasomi na watu wenye uzoefu mkubwa lakini matokeo ya utendaji wao aidha umekuwa butu wa makengeza au usiokidhi viwango vya kile kilichotegemewa kutoka kwao.

Tasnia ya sanaa Tanzania inakua kwa kasi, sasa ni ajira rasmi inayotegemewa na wengi...! Kazi ya kutengeneza mziki mmoja au filamu hujumisha utaalam tofauti ambako kote huko watu hupata kula yao.

Kumekuwa tabia ya mlipuko wa kufungia kazi za wasanii kutoa adhabu baada ya hapo kimya.

Lakini hawa wana jukumu kubwa sana la kusimamia hii tasnia muhimu
Waunde sasa chombo cha kuratibu kazi zote za sanaa kabla ya kurushwa hewani, hiki chombo ndio kitakuwa na jukumu la kuangalia mapungufu ya kazi yenyewe na kuona kama inafaa kuwapelekea walaji kulingana na mila tamaduni na desturi zetu.

Wasanii wengi ni vijana chini ya miaka 30 wanaohitaji miongozo ya kila aina, wana vipaji lakini wanakosa uzoefu na hata hekima kwenye mengi...pesa zao wanapata kwa shida Sana hivyo ni vema wakapata chombo cha kupitia kazi zao kabla hawajazitoa ili kuepuka hasara kama hizo za kufungiwa.

Kutegemea wasimamizi binafsi na waongozaji haisaidii kwakuwa tumeona mara nyingi makosa yakijirudia.

Isaidieni Tanzania wasaidieni vijana wetu waweze kusimama tokeni ofisini undeni chombo cha kuratibu kazi zao kabla hazijatoka hili ni jukumu lenu nyie
2627c4496add88632358adc380447313.jpg
Nafikiri kuna chombo kinaitwa "National Film Censorship Board" ndiyo kazi yake kuchuja vitu kama hivi sasa sijui kama bado ipo.
 
Nafikiri kuna chombo kinaitwa "National Film Censorship Board" ndiyo kazi yake kuchuja vitu kama hivi sasa sijui kama bado ipo.
Kilikuwepo mara ya mwisho wayback miaka ya 90 kilikuwa live kidogo halafu kikafa kile kifo cha moja kwa moja...sasa kulingana na mahitaji ya wakati na kwa kushirikiana na hao wadau hapo juu wangekirejeshea uhai
 
Kuna mtu alisema wakatazwe na wanawake wenye chura kutembea barabarani
Vigodoro mnavitandika asubuhi na mapema huko uswahilini na hakuna kiingilio mpaka watoto wapo
Leo unaenda kufungia video ambayo ipo Youtube TU!!
 
Back
Top Bottom