Kuzuia uchafu kwenye uchaguzi, tufute mishahara kwa wachaguliwa wote

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,085
Nchi Yenye Matatizo makubwa ya umaskini, huduma na mifumo mbalimbali, kama ilivyo Tanzania, ili iweze kutoka ilipo, inahitaji viongozi wenye ubunifu zaidi, akili zaidi, uadilifu zaidi na uzalendo zaidi kuliko Nchi zilizoendelea.

Bahati mbaya, nchi hizi zenye matatizo kama Tanzania, ndiyo zinazoongoza kuwa na viongozi walio duni zaidi katika ubunifu, uadilifu, akili na uzalendo. Wengi wanatafuta uongozi ili waondokane na umaskini au ili wajitajirishe zaidi, na hivyo kuyaongeza matatizo zaidi kuliko kuyapunguza.

Ni vema tukawa na mfumo unaowachekecha wale wote wanaoutafuta uongozi ili kujitajirisha na kujineemesha.

Kwa kuanzia, tungeweka sheria ya kipindi cha mpito, angalao cha miaka 20, viongozi wa kisiasa, wale wanaochaguliwa na wananchi, wasiwe na mishahara. Badala yake walipiwe gharama kama vile malazi, usafiri, matibabu, na chakula tu, pale wanapokuwa mbali na makazi yao. Lengo iwe ni kuwaondoa wale wote wanaoutafuta uongozi kwa dhamira ya kujineemesha.

Kisha kuwe na sheria maalum kwaajili ya kuwadhibiti viongozi ambao watakuwa wamekosa uadilifu kama vile kupokea rushwa au malipo yoyote yanayohusiana na ufisadi. Viongozi hao baada ya kumaliza muda wao, kuwe na kamati maalum ya kufuatilia utendaji wao wakati wakiwa viongozi, na wale wote ambao watathibitika bila shaka kuwa walifanya kazi kwa weledi mkubwa, ujasiri, ubunifu, na kwa uadilifu mkubwa, watapewa vyeti maalum na kupewa malipo ya mara moja ya uongozi uliotukuka. Wale ambao watathibitika kutenda kinyume chake, watatangazwa majina yao kwa umma, na wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa kipindi cha miaka 20.

Hii itawafanya wanaotafuta pesa kupitia uongozi kutogombea uongozi, na waliopo kwenye uongozi kufanya kila wawezalo kutenda vyema ili mwisho wa term yao wapate mafao mazuri, na kuruhusiwa kugombea uongozi.

Tukiwekwa sheria ya namna hii, hakika nami na wengine wengi wasiopenda kuchafuliwa na mifumo ya kifisadi iliyopo, tutagombea uongozi.

Kama kweli mtu unasema unataka kuwasaidia watu na Taifa kupitia uongozi, basi dhamira hiyo ionekane kwa vitendo. Isiwe kinyume chake. Unasema unataka kuwasaidia watu kupitia uongozi kumbe unataka kuwaibia watu na Taifa kupitia uongozi. Nchi inahitaji viongozi wanaoumizwa na matatizo ya Taifa, lakini siyo kuumizwa tu bali wenye uwezo na walio wabunifu wa kuyaondoa au kuyapunguza hayo matatizo yanayowaumiza.
 
Tanzania tukipata rais mwenye maono na nia ya dhati ya kurekebisha mambo utakuwa mwanzo mzuri sana wa mabadiliko kama haya. Taizo liko kwenye namna ya kumpata!
 
Wabunge wawe watu wenye kiu ya kulete maendeleo ya wananchi wao kwa hiyo wajitolee na kuyaishi maneno yao kuwa wananchi wanawapenda na kuishi nao. Kwa sasa kila kiongozi ana walinzi sijui ni kwa nini ingawa wanasema wamechaguliwa kwa kishindo na wananchi wanawapenda?
 
Kila kiongozi anasema kuwa anataka kuwasaidia wananchi, lakini akiyapata madaraka anapigania uongezwe mshahara wake, marupurupu yake, na anaishia kuiba kwa njia mbalimbali kwa kiwango cha kukufuru.

Kama kweli wanataka kuwasaidia wananchi, basi wajitolee, wasiwe na mishahara. Wawe kama makasisi wa Kanisa, hapo ndipo tutaweza kutamka kuwa uongozi ni wito. Lakini kwa sasa, kwa nchi yetu, uongozi ni 'tamaa ya kuutafuta utajiri kwa kuiba na kufanya ufisadi'.
 
Upo sahihi kabisa mkuu, hii mishahara minono ndiyo inasababisha tupate viongozi wa hovyo, Mbona Mapadre, Wachungaji na Maaskofu hawana mishahara na wanahudumia jamii vizuri?
 
Kutowalipa mishahara siyo solutions,walipwe lakini ukipatikana unakula rushwa au kumiliki akaunti ya Benki nje ya nchi(isipokuwa kwa waliothibitika kuwa ni Wafanyabiashara)utafungwa jela maisha na kutoruhusiwa wewe na kizazi chako chote kufanya kazi za umma ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zako.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hapa hapana kwengine ni sawa
 
Wabunge wawe watu wenye kiu ya kulete maendeleo ya wananchi wao kwa hiyo wajitolee na kuyaishi maneno yao kuwa wananchi wanawapenda na kuishi nao. Kwa sasa kila kiongozi ana walinzi sijui ni kwa nini ingawa wanasema wamechaguliwa kwa kishindo na wananchi wanawapenda?
Sahivi hatuna wabunge tuna majangili tupu
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi yanaweza kutengeneza mwanzo mpya wa kiutawala ulio sahihi hapa nchini.
Tunapenda kuwaza yasiyowezekana na kuacha kufikiria kufanya yale yenye kuwezekana hata kama ni kidogo kidogo.
 
Nchi Yenye Matatizo makubwa ya umaskini, huduma na mifumo mbalimbali, kama ilivyo Tanzania, ili iweze kutoka ilipo, inahitaji viongozi wenye ubunifu zaidi, akili zaidi, uadilifu zaidi na uzalendo zaidi kuliko Nchi zilizoendelea.

Bahati mbaya, nchi hizi zenye matatizo kama Tanzania, ndiyo zinazoongoza kuwa na viongozi walio duni zaidi katika ubunifu, uadilifu, akili na uzalendo. Wengi wanatafuta uongozi ili waondokane na umaskini au ili wajitajirishe zaidi, na hivyo kuyaongeza matatizo zaidi kuliko kuyapunguza.

Ni vema tukawa na mfumo unaowachekecha wale wote wanaoutafuta uongozi ili kujitajirisha na kujineemesha.

Kwa kuanzia, tungeweka sheria ya kipindi cha mpito, angalao cha miaka 20, viongozi wa kisiasa, wale wanaochaguliwa na wananchi, wasiwe na mishahara. Badala yake walipiwe gharama kama vile malazi, usafiri, matibabu, na chakula tu, pale wanapokuwa mbali na makazi yao. Lengo iwe ni kuwaondoa wale wote wanaoutafuta uongozi kwa dhamira ya kujineemesha.

Kisha kuwe na sheria maalum kwaajili ya kuwadhibiti viongozi ambao watakuwa wamekosa uadilifu kama vile kupokea rushwa au malipo yoyote yanayohusiana na ufisadi. Viongozi hao baada ya kumaliza muda wao, kuwe na kamati maalum ya kufuatilia utendaji wao wakati wakiwa viongozi, na wale wote ambao watathibitika bila shaka kuwa walifanya kazi kwa weledi mkubwa, ujasiri, ubunifu, na kwa uadilifu mkubwa, watapewa vyeti maalum na kupewa malipo ya mara moja ya uongozi uliotukuka. Wale ambao watathibitika kutenda kinyume chake, watatangazwa majina yao kwa umma, na wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa kipindi cha miaka 20.

Hii itawafanya wanaotafuta pesa kupitia uongozi kutogombea uongozi, na waliopo kwenye uongozi kufanya kila wawezalo kutenda vyema ili mwisho wa term yao wapate mafao mazuri, na kuruhusiwa kugombea uongozi.

Tukiwekwa sheria ya namna hii, hakika nami na wengine wengi wasiopenda kuchafuliwa na mifumo ya kifisadi iliyopo, tutagombea uongozi.

Kama kweli mtu unasema unataka kuwasaidia watu na Taifa kupitia uongozi, basi dhamira hiyo ionekane kwa vitendo. Isiwe kinyume chake. Unasema unataka kuwasaidia watu kupitia uongozi kumbe unataka kuwaibia watu na Taifa kupitia uongozi. Nchi inahitaji viongozi wanaoumizwa na matatizo ya Taifa, lakini siyo kuumizwa tu bali wenye uwezo na walio wabunifu wa kuyaondoa au kuyapunguza hayo matatizo yanayowaumiza.
Hii njia itakuwa muarobaini wa uchaguzi wetu
 
Wabunge wawe watu wenye kiu ya kulete maendeleo ya wananchi wao kwa hiyo wajitolee na kuyaishi maneno yao kuwa wananchi wanawapenda na kuishi nao. Kwa sasa kila kiongozi ana walinzi sijui ni kwa nini ingawa wanasema wamechaguliwa kwa kishindo na wananchi wanawapenda?
90% wanaingia kwa maslahi zaidi
 
Kila kiongozi anasema kuwa anataka kuwasaidia wananchi, lakini akiyata madaraka anapigania uongezwe mshahara wake, marupurupu yake, na anaishia kuiba kwa njia mbalimbali kwa kiwango cha kukufuru.

Kama kweli wanataka kuwasaidia wananchi, basi wajitolee, wasiwe na mishahara. Wawe kama makasisi wa Kanisa, hapo ndipo tutaweza kutamka kuwa uongozi ni wito. Lakini kwa sasa, kwa nchi yetu, uongozi ni 'tamaa ya kuutafuta utajiri kwa kuiba na kufanya ufisadi'.
Mungu ibariki Tanzania
 
Upo sahihi kabisa mkuu, hii mishahara minono ndiyo inasababisha tupate viongozi wa hovyo, Mbona Mapadre, Wachungaji na Maaskofu hawana mishahara na wanahudumia jamii vizuri?
Hivi haiwezekani ukaanzishwa mjadala wa kitaifa juu ya kuondoa malipo kwa wabunge na madiwani ?
 
Back
Top Bottom