Kuzembea wajibu wa matunzo makusudi kunaweza kuvunja Ndoa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,502
8,380
Maana ya Talaka

Sheria inayosimamia masuala ya talaka ni sheria ya Ndoa ya mwaka 1971. Na kwa mujibu wa sheria hiyo, “Talaka ni ruhusa ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzie”.

Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka Chombo pekee chenye uwezo wa kuvunja ndoa ni mahakama. Kwa kawaida mahakama hutoa talaka kwa ndoa ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi. Lakini mahakama inaweza kutoa talaka hata kama ndoa haijadumu kwa kipindi hicho cha miaka miwili iwapo mlalamikaji atatoa sababu nzito sana.

Sababu ya kutoa talaka Mahakama hufikia uamuzi wa kutoa talaka baada ya kuridhika kuwa ndoa imevunjika kiasi ambacho haiwezi kurekebishika tena.

Kuzembea wajibu kwa makusudi Mume ana wajibu wa kumtunza mkewe, kwa kumpa chakula, mahali pa kulala na mavazi yanayofaa kulingana na hali yao ya maisha. Mke pia ana wajibu wa kumtunza mume ikiwa mke huyo anao uwezo na mume hawezi kujipatia pato lolote, kwa sababu ya maradhi au maumivu ya mwili.

Hivyo basi kama mume anaishi na mke, lakini hampi matumizi hata kidogo, au anatoa matumizi kidogo sana kwa mkewe, ukilinganisha na uwezo wake na hali yao ya maisha, huu unaweza kuwa ushahidi kuonyesha kwamba ndoa imevunjika.

Kadhalika, kama mume hawezi kujisaidia kwa matumizi ya kila siku, lakini mkewe anao uwezo ila anakataa, basi mke anaweza kupewa talaka, kwa sababu ndoa hiyo inahesabika kuwa imevunjika kiasi kisichoweza kurekebishika.
 
Back
Top Bottom