mujemaso
Senior Member
- Apr 26, 2012
- 112
- 44
Habari wanajamvi...
Hivi juzi nilikutana na mtwasi mwenzangu na tukawa na stori za hapa na pale kuhusu maisha. Katika mazungumzo tukagusia maendeleo ya watoto shuleni.
Jamaa ana watoto wa kiume wanne na akawa analalamika kuwa watoto hawako vizuri shuleni. Ni wazito sana kuelewa masomo. Akaongeza kitu ambacho kimenifanya niandike hapa jamvini kuwa:
Akili (intelligence) kwa mtoto wa kiume inachangiwa kwa asilimia kubwa na mama yake. Kwa madai kuwa akili (intelligence) hubebwa na kijinasaba (gene) ambayo inakuwa kwenye X chromosome (ikumbukwe kuwa mtoto wa kiume huwa ni XY) hivyo baba ni asilimia ndogo sana huchangia kwenye akili ya mtoto wa kiume kwani X inachangiwa na mama. Akaendelea kusema kuwa baba huchangia kwa mtoto wa kike na akanambia kuwa yuko mbioni kutafuta mtoto wa kike ili angalau amrithishe akili.
Mazungumzo hayakuishia hapo akadai kwamba ndo maana baba zetu walikuwa wanaoa wake wengi ama wanazaa nje ya ndoa ili tu kujaribu kuwa na watoto mchanganyiko na matokeo yake unaweza ukapata mtoto mwenye akili. Akasema jaribu kuangalia familia ambazo baba ana wake wengi utakuta watoto wa mama mmoja ndo wana akili kuliko wengine. Pia watoto wa nje ya ndoa wanavyokuwa tofauti.
Swali ni je, huyu jamaa yuko sahihi? Ni kweli akili ya mtoto wa kiume inachangiwa zaidi na mama?
Nawasilisha.