Kuwepo na minimum qualification wabunge

Silly

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
569
180
Nadhani viwango vya uchangiaji kwa wabunge wengi vimekuwa duni kutokana na elimu yao ndogo pamoja na wengi kuwa na nafasi za kuzawadiwa. Kwa maana hiyo nadhani ni vema kuwepo na sifa lets say degree angalau moja ili mtu apitishwe kuwa mgombea wa ubunge, na diploma/certificate kwa madiwani. Kama ikiwa hivi mimi nadhani vile vituko vya mjengoni Dom na halmashauri zetu vitapungua maana wengi watakuwa focussed,

nawasilisha...
 
mawazo mgando hayo! unafikiri kuwa na elimu kubwa ndio kutoa mchango mzuri bungeni? uongozi ni kipaji pia kama vilivyo vipaji vya soka.Wabunge wengi kutoka Zenji wana elimu ndogo sana lakini angalia jinsi wanavyojua kujenga hoja na kutetea maslahi ya Wazanzibar.
Kumbuka ha Rostam na Dewji ni wasomi lakini umeshawahi kuskia michango yao bungeni?
 
Wabunge kazi yao ni kuchonga kama wamemeza redio, sioni kaa wana nafasi yoyote kuleta maendeleo ktk taifa hili. Serikali hii ya fikra kongwe is more likely kufeli with or without wabunge, the better choice ni kuondoa mamlaka kwa wanasiasa na kuwapa wanataaluma na vyombo vyao vya udhibiti waongoze nchi based on reason and specialization of labor. Najua it is so unpopular kuwamwaga wanasiasa maana wao wameshika mpini, lakini mpaka hapo tutakapoona huu mwanga ndio hapo ndege ya uchumi (lolz at Mamvi) itakapopaa
 
Kwa ulimwengu wa sasa minimum qualifications inatakiwa! Hawa wabunge ujanja wao wote wa kuongea kama wamemeza kanda ya Taarabu ni humuhumu nchini. Wakitoka nje ya TZ huwa wanageuka mabubu, wanaishi kusema YES YES tu.
mawazo mgando hayo! unafikiri kuwa na elimu kubwa ndio kutoa mchango mzuri bungeni? uongozi ni kipaji pia kama vilivyo vipaji vya soka.Wabunge wengi kutoka Zenji wana elimu ndogo sana lakini angalia jinsi wanavyojua kujenga hoja na kutetea maslahi ya Wazanzibar.
Kumbuka ha Rostam na Dewji ni wasomi lakini umeshawahi kuskia michango yao bungeni?
 
I support you, wabunge kama Lusinde ni aibu kwa taifa, eti naye yuko mjengoni !
 
Ingekuwa ni usomi wasomi wangapi wanalala bungeni akishtushwa na kupiga meza anasema naunga mkono kwa asilimia mia.
 
unajua kuwa chenge kasoma wapiI? Chuo gani? Jibu unalo lakini elimu ni muhimu pia
 
Wabunge wengi hasa wa CCM hawana viwango, tunajipa moyo tu kutokana na mchakato wenyewe wa kuwapata hugubikwa na vioja vya rushwa, matumizi ya nguvu, udini, fitna, uzushi, wizi wa kura, ushirikina etc
Yaani asilimia zaidi ya 8O% ya wabunge wa CCM ni bomu linalosubiri nguvu ya mabadiliko kuliteketeza.
 
mawazo mgando hayo! unafikiri kuwa na elimu kubwa ndio kutoa mchango mzuri bungeni? uongozi ni kipaji pia kama vilivyo vipaji vya soka.Wabunge wengi kutoka Zenji wana elimu ndogo sana lakini angalia jinsi wanavyojua kujenga hoja na kutetea maslahi ya Wazanzibar.
Kumbuka ha Rostam na Dewji ni wasomi lakini umeshawahi kuskia michango yao bungeni?
Mkuu vp maneno makali kwani nawewe ni mbunge poa?
 
Wabunge wengi hasa wa CCM hawana viwango, tunajipa moyo tu kutokana na mchakato wenyewe wa kuwapata hugubikwa na vioja vya rushwa, matumizi ya nguvu, udini, fitna, uzushi, wizi wa kura, ushirikina etc
Yaani asilimia zaidi ya 8O% ya wabunge wa CCM ni bomu linalosubiri nguvu ya mabadiliko kuliteketeza.
Chadema walishaliona hilo na wameanzia kwenye viti maalumu mchuano ulikuwa mkali kwa kuwa higher marks was the factor
 
mawazo mgando hayo! unafikiri kuwa na elimu kubwa ndio kutoa mchango mzuri bungeni? uongozi ni kipaji pia kama vilivyo vipaji vya soka.Wabunge wengi kutoka Zenji wana elimu ndogo sana lakini angalia jinsi wanavyojua kujenga hoja na kutetea maslahi ya Wazanzibar.
Kumbuka ha Rostam na Dewji ni wasomi lakini umeshawahi kuskia michango yao bungeni?

Huyu jamaa ana point hii itatusaidia katika international forum tusiburuzwe!!! Hivi unajua elimu inampa mtu confidence sometime? ndo sababu mkuu wa kaya anjiita Dr Dr Dr.... kwa anjua impact yake kwa jamii..
Just imagine mkurugenzi wa halmashauri ni msomi and then Diwan ni std seven do you think huyu diwan ataweza kucoment chochote kwenye kikao zaidi ya kupiga makofi?
 
Amesoma LLB ktk moja ya vyuo vikuu bora duniani(HAVARD) yeye na former secretary wa EAC hon.mwapachu.
 
Amesoma LLB ktk moja ya vyuo vikuu bora duniani(HAVARD) yeye na former secretary wa EAC hon.mwapachu.

Na ndiye mnojawapo kati ya wabunge wawili wa CCM angalau waliochangia hoja ya mswada wa kuunda katiba juzi. Wengine wote ilikuwa mipasho tu dhidi ya CDM/Lisu. Tuna safari ndefu TZ.
 
Ninatamani kungekuwa na mfumo kama wa wachezaji mpira ambao kabla hujasajiliwa lazima ufanye mechi za majaribio ndo ufuzu kusajiliwa isipokuwa wale wazoefu wanaosajiliwa moja kwa moja, najua wabunge kama lusinde wasingegusa pale mjengoni. Uongozi ni kipaji kutoka kwa allah, ukiona mtu anafanya kama ya lusinde ujue ndo mifumo yetu ya kupeana kwa kujali matumbo na vile vile elimu ni muhimu sana
 
mbona rahisi hiyo,kwani sh ngapi kuchukua degree ya online kama lyatonga.

Mkuu, hata serikalini wakitangaza kazi wanahitaji uwe na elimu stressing( From a recognized institution), sidhani hizo za online kama zina uzito wowote.
 
Hivi leo ikifanyika sensa pale bungeni, mbunge wako kipenzi tena aliyechaguliwa kwa kura nyingi sana atakuwa na mchango gani, najua wapo watakaopata record ya mahudhurio mazuri, wapo hawajawahi kuchangia chochote sio kujibu maswali wala kuuliza au kuleta hoja zozote, wapo ndugu zetu wazuri kupga ile mi-meza na wale wa ndiooooooooooooooo,
 
Back
Top Bottom