Kuwepo na minimum qualification wabunge

Naunga mkono hoja kwamba wabunge wanapaswa na elimu lakini najiuliza maswali hivi mbunge kama Mwingulu Nchemba kwani hana degree???? Juma Nkamia??? na wengine wengi tu..
Je kama wanazo kweli unaweza kulinganisha mchango wao labda na wa mbunge kama Mnyika ambaye inasemekana hana cheti???? Kiwango flan cha elimu kinahitajika lakini pekee hakitoshi katika kutambua kiongozi bora.
 
Wawe na degree ; hili sio mjadala ni jinsi ya kutekeleza ndio linahitaji mjadala tuanzie hapo mengine ya busara sijui na nini yatafuata baadaye huko tukijaaliwa uhai!!!

Hili tukiliweza pale ndani patabadilika na tutaona faida ya elimu na mkazo utaongezeka juu ya elimu na hadhi ya elimu itaonekana!!!!!!

Ila wasionazo lazima wapinge sana hili na wapambe wao
 
Nadhani viwango vya uchangiaji kwa wabunge wengi vimekuwa duni kutokana na elimu yao ndogo pamoja na wengi kuwa na nafasi za kuzawadiwa. Kwa maana hiyo nadhani ni vema kuwepo na sifa lets say degree angalau moja ili mtu apitishwe kuwa mgombea wa ubunge, na diploma/certificate kwa madiwani. Kama ikiwa hivi mimi nadhani vile vituko vya mjengoni Dom na halmashauri zetu vitapungua maana wengi watakuwa focussed,

nawasilisha...

Uongozi ni kipaji, wabunge wengi hawana kipaji cha uongozi.Wanagombea kwa maslahi yao na si kama sehemu ya kuwatumikia wanachi kwa mantiki hiyo wengi hawanauwezo wakuongoza.
 
Back
Top Bottom