Kuunganisha mifuko hakufuti deni la Serikali

lunganzira

Member
Nov 9, 2018
58
28
akizungumza na mwandishi wetu Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Dkt. Irene Isaka alisema lengo la kuunganisha Mifuko ya pensheni ilikuwa ni kuongeza ufanisi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na si kufuta madeni ya Serikali.

Alisema hadi sasa Mamlaka haijapokea maelekezo yoyote kutoka Serikalini kwamba serikali imefuta madeni inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya jamii.

Alisema taarifa ambayo mamlaka inayo ni kwamba Serikali ilisitisha kukopa toka mwaka 2013 na baada kufikia ukomo wa kukopa ambao kwa mujibu wa Miongozo ya Uwekezaji ambayo inaelekeza ukomo wa 10% ya rasilimali za Mifuko.

Alisema madeni yamegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ni deni la michango ya wanachama na sehemu ya pili ni deni la miradi. Na kwamba Mamlaka haina taarifa zinazoonesha kwamba deni lote limefika Tln 8

Alisema sehemu ya kwanza ambayo ni deni la michango. Taarifa za uhakiki uliofanywa na ofisi ya mkaguzi mkuu wa ndani zilionesha kwamba kiwango cha deni la michango ni Trlioni 2 ambapo hadi kufika Disemba 2017 Serikali ilikuwa imelipa shilingi. Trilioni1.3
Kwa upande wa deni la miradi taarifa baada ya uhakiki zinaonesha Shilingi Trl 1.1. Hili ni deni ambalo linajumuisha (mikopo na riba) kwenye miradi ambayo ilidhaminiwa na Serikali. Ikumbukwe kwamba tunaposema mikopo kwa serikali haina maana kwamba serikali ilikopa moja kwa moja bali ilidhamini miradi iliyokopeshwa na Mifiko ya Hifadhi ya jamii. Miradi kama vile ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma, Chuu cha Nelson Mandela, Daraja la Kigamboni, Jengo la Bunge ambalo zaidi ya 50 ya deni tayari imelipwa.

Katika hili Serikali iliahidi kuaanda hati fungani (non cash Bond ) baada ya kukamilisha mchakato wa uhakiki na kupitishwa na kamati ya madeni ya Serikali (National Debt Committee).

Alisema sababu za msingi za kuunganisha Mifuko zilikuwa ni

kutekeleza matakwa ya wanachama wa Mifuko ya kuondoa utitiri wa Mifuko na

Kupunguza gharama za uendeshaji;

Kuboresha mafao ya pensheni kwa kufanya (indexation)

Kuweka usawa na yanayofanana kwa wanachama:

Kuboresha mafao ya Warithi:

Kuweka mikopo ya nyumba kwa wanachama

Kuweka mafao ya upotevu wa ajira
Kuweka mafao yanayoendana na viwango vya Shirika la kazi Duniani (ILO) na kuboresha usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
KUUNGANISHA MIFUKO HAKUFUTI DENI LA SERIKALI.

Jamani nawasihi tuache uanaharakati kwenye mambo ya kitaalam hasa pale tunapokuwa hatuna ufahamu wakutosha kwenye jambo husika. Lakini pia kwenye jambo lenye maslahi mapana ya jamii kama mfumo wa pensheni siku zote tujifunze kulijadili kwa kuzingatia mapana yake, tusiwe wabinafsi. Kabla ya kubeza mabadiliko yaliyofanyika kupitia Sheria Na. 2 ya mwaka 2018 tunapaswa kuelewa mambo yafuatayo:
1. Mfuko wa Pensheni siyo benki ni mfuko kwa ajili ya mafao ya uzeeni. Mafao yake yamekusudiwa kumsaidia mwanachama pale anapopoteza uwezo wa kujipatia kipato kwa sababu ya uzee, kupata maradhi au ulemavu utakaopelekea kupoteza uwezo wa kufanya kazi. Mafao haya pia yanakusudia kuwasaidi warithi/wategemezi wa mwanachama au mstaafu pale anapofariki.

2. Mfuko wa pensheni ni wa wanachama wenyewe . Hivyo, uhai na uendelevu wa mfuko unategemea uchangiaji wa wanachama na mfumo wa ukokotoaji na ulipaji wa mafao. Ni lazima kuwe na uwiani halisi baina ya kiwango cha uchangiaji na kiwango cha mafao yanayolipwa. Tofauti na hapo utakuwa na mfuko wenye sura ya "Desi/Upatu" ambapo mfuko utaishia kulipa wanachama wachache na waliowengi watakosa mafao:

3. Mafao ya pensheni yanakusudiwa kuwa mbadala wa kipato/mshahara ambao mwanachama alikuwa akipata kabla ya kustaafu. Ndiyo maana sehemu nyingine duniani hakuna utaratibu wa kulipwa kwa mkupuo, badala yake pensheni yote (full pensheni) hugawanywa na kulipwa kwa kila mwezi (monthly pensheni). Lengo ni kuhakikisha kwamba kiasi cha pensheni ambacho
mwanachama anakipata kinamwezesha kuishi maisha yanayofanana na maisha aliyokuwa akiishi akiwa kazini. Hii ndiyo sababu ya Kanuni za 2014 na 2018 kuweka mgawanyo wa pensheni wa asilimia 25% (mkupuo) na 75% (pensheni ya kila mwezi). Kwa utaratibu huu malipo ya pensheni ya kila mwezi yataongezeka.

4. Ni muhimu pia kutambua kwamba Kanuni za Mafao za mwaka 2018 ni mwendelezo wa Kanuni za Mafao za Mwaka 2014 ambazo zimekuwa zikitumika kwa wanachama wa Mifuko ya PPF na NSSF na pia kwa Wanachama wa Mifuko ya PSPF, LAPF na GEPF walioajiriwa kuanzia Julai, 2014. Hivyo, siyo Kanuni mpya kama ambavyo baadhi ya watu wanajaribu kupotosha.

5. Kuhusu ukomo wa mafao ya mstaafu. Mstaafu atapokea mafao yake mpaka mwisho wa uhai wake. Hata baada ya mstaafu kufariki, warithi/wategemezi wake wataendelea kupokea mafao kwa kipindi cha miaka mitatu bila kujali mstaafu huyo amepokea pensheni kwa miaka mingapi. Hii ni tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ambapo mafao ya mstaafu yalikuwa yanakoma siku mstaafu anapofariki.
Hivyo, taafsiri kwamba mstaafu atapokea pensheni kwa miaka 12.5/15.5 tu siyo sahihi hata kidogo na ni upotoshaji wa makusudi. Kipindi hicho kimewekwa kwa madhumuni ya ukokotoaji wa mafao tu. Ni muhimu pia kufahamu kuwa vipindi hivyo pia vilikuwepo kwenye kanuni zilizopita lakini wastaafu wameendelea kupokea pensheni zao hata baada ya kumalizika kwa vipindi hivyo.

TUSIWE WABINAFSI, MIFUKO NI YETU SOTE NA INAPASWA KUENDELEA KUWEPO KWA MASLHAHI YA WANACHAMA WOTE
 
Matango pori!

Hizo nchi ambazo wastaafu hawalipwi malipo ya pensheni ya mkupuo watumishi katika nchi hizo wanalipwa mishahara duni na yenye rundo la makato kama hapa kwetu kiasi kwamba mtumishi mpaka anastaafu anashindwa hata kujenga na kufungua miradi akiwa kazini?

Mazingira na standard ya maisha ya wafanyakazi katika nchi hizo yanafanana na ya wafanyakazi wa hapa kwetu?

Kuhusu deni la trilioni 8, ina maana CAG alidanganya?

Kama alidanganya,waliwahi kupinga hiyo figure?

Mpaka CAG anatoa ripoti yake, hawakushirikishwa na kuridhia taarifa ya CAG kuhusu hilo deni la trilioni 8?

Je,ni kweli tangu 2013 serikali haijakopa katika hii mifuko?

Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa tangu 2013 serikali haijakopa hela kutoka katika hiyo mifuko hasa serikali hii ya awamu ya tano,
 
I wish siku moja JF wangetoa ruhsa ya watu kutuka.......
HAKYANANI huu uzi leo ungenitambua mana ningeuporomoshea mitusi mizito mizito mitupu
 
]Hatutaki kulipwa Asilimia 25 tunataka tulipwe kama zamani kinachobaki ndio kiwe cha kila mwezi
 
Maagizo toka juu.
Ina maana yeye si mwanachama wa mfuko wo wote ila ana mamlaka ya kuamua juu ya hiyo mifuko.
Pesa yetu tuliyokatwa kwenye mshahara inaamuliwa na maagizo ya mporaji wa hizo pesa.
Kwanza kukopwa hizo pesa kunamnufaisha vipi mwanachama?

Kweli hii ni nchi ya kusadikika.
 
Mamlaka haina taarifa ya deni?!!! Serious? ama ni wanataka kutufanya sisi wajinga? Wanafanya kazi gani kama hata hawajui deni ni kiasi gani...!!
 
kama hawana uaminifu bora mifuko isitishwe wafanyakazi wapate pesa yao wote wahifadhi wenyewe kiinua mgongo chao
 
Back
Top Bottom