THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Kuna taarifa kwamba waziri mkuu aliyejiuzulu E.N.Lowassa leo atazungumza na wanahabari.
Lowassa atazungumzia mambo matatu;1.Sakata la RICHMOND,2.Habari zinazoandikwa na kusemwa juu yake,na 3.Hali ya siasa za CCM arusha.
Wakati hayo yakitokea mh.Mwakyembe yupo nchini India kwa matibabu lakini ikumbukwe mh.Mwakyembe aliwahi kusema " kama kuna wabunge wasioridhika na maazimio ya Bunge, waombe kazi hiyo ifanyike upya ili yasemwe yote, hata yaliyoachwa ili kulinda heshima ya serikali."
Hapa naona kuna kamchezo ka kuviziana.Iweje mambo ya RICHMOND yazungumziwe wakati huyu bwana aliyesema kama kuna mtu hajaridhika aseme ili atoe siri zote hayupo nchini?
Lowassa aliyelalamikia sana kamati ya Mwakyembe sidhani kama anaweza kuzungumzia sakata zima la RICMOND bila kumtaja Mwakyembe wala kamati yake.
Kama kweli mh.Lowassa ana nia njema ya kulizungumzia sakata la RICHMOND namsihi amsubiri Mwakyembe apone ili kama ataguswa aweze kujitetea.Vinginevyo kile alichokiita mh.Lowasa "NATURAL JUSTICE" naye atakuwa amemnyima Mwakyembe.