Kuumwa kwa Mwakyembe na kuibuka kwa Lowassa

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,779
1,304
Kuna taarifa kwamba waziri mkuu aliyejiuzulu E.N.Lowassa leo atazungumza na wanahabari.
Lowassa atazungumzia mambo matatu;1.Sakata la RICHMOND,2.Habari zinazoandikwa na kusemwa juu yake,na 3.Hali ya siasa za CCM arusha.
Wakati hayo yakitokea mh.Mwakyembe yupo nchini India kwa matibabu lakini ikumbukwe mh.Mwakyembe aliwahi kusema " kama kuna wabunge wasioridhika na maazimio ya Bunge, waombe kazi hiyo ifanyike upya ili yasemwe yote, hata yaliyoachwa ili kulinda heshima ya serikali."
Hapa naona kuna kamchezo ka kuviziana.Iweje mambo ya RICHMOND yazungumziwe wakati huyu bwana aliyesema kama kuna mtu hajaridhika aseme ili atoe siri zote hayupo nchini?
Lowassa aliyelalamikia sana kamati ya Mwakyembe sidhani kama anaweza kuzungumzia sakata zima la RICMOND bila kumtaja Mwakyembe wala kamati yake.
Kama kweli mh.Lowassa ana nia njema ya kulizungumzia sakata la RICHMOND namsihi amsubiri Mwakyembe apone ili kama ataguswa aweze kujitetea.Vinginevyo kile alichokiita mh.Lowasa "NATURAL JUSTICE" naye atakuwa amemnyima Mwakyembe.
 
Mi nadhani tusubiri nini anataka kukisema, kwa kuanza kubashiribashiri unaweza ukajikuta unasababisha tusikipate anachotaka kukisema hasa akizingatia ushauri wa kila mtu
 
Anachotafuta EL ni huruma za wananchi kwa kuwaponda wenzake,lakini ikumbukwe alikuwa NIGERIA pengine anataka kupima nguvu alizokuja nazo
 
huyu bwana wa Nigeria ni noma, yaani naanza kubadilisha msiamamo wangu taratibu na hii ni 2011 bado miaka 4, nafikiri ile dawa, zindiko, dua inafanya kazi
 
Acha kuyazua Kaka!Mbona unalazimisha kuhusianisha mambo yasiyochangamana!
Kamati ya Bunge Ikimaliza kazi inampa Spika Majawabu afu ndo unakuwa mwisho wa kamati!
Kimantiki Mwakyembe hakuwa mwenyekiti wa Kudumu wa Ile Kamati na hata kitakachofata kuhusiana na Richmond si chake tena!
 
huyu bwana wa Nigeria ni noma, yaani naanza kubadilisha msiamamo wangu taratibu na hii ni 2011 bado miaka 4, nafikiri ile dawa, zindiko, dua inafanya kazi
Ole wenu enyi wenye Imani haba, kwani hata Shekh Yahaya alikuwa noumer.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom