Kuuliza si ujinga: Ni sawa/sahihi Kamishna Mkuu wa TRA kuwa Mwenyekiti wa Bodi NMB?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dr. Edwin Mhede ndiye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB.

TRA ndiye mkusanya kodi na mapato wa nchi hii wakati NMB ni mmoja wa walipakodi. Bodi ya Wakurugenzi ndiyo itoayo maamuzi makubwa ya kikampuni ikiwemo kuteua, kukopa na kadhalika.

Kutokana na uelewa wangu huo wa TRA na Bodi ya Wakurugenzi, ni sawa/sahihi kwa Kamishna Mkuu wa TRA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, mmoja wa walipakodi? Hakuna mgongano wowote wa kimaslahi katika utendaji kazi wake?
 
Kodi si wanatakiwa kulipa kisheria sio maamuzi ya Mhede Mkuu. Kwa hiyo hata account zake afungulie TRA bank au Bot maana akienda kwingine itaonekana kuna conflicts of interest.
 
Ni makosa makubwa Tax collector kuwa ndo mwenyekiti wa board ya benki kubwa ya kibiashara hasa ikitokea sintofahamu ya suala la kodi. Ningeelewa kama Msajili wa Hazina angekuwa ndo Mwenyekiti kwa niaba ya serikali.

Mgogano sio tu kwenye masuala ya kodi bali pia na masuala ya kukusanya mapato ya serikali. Halafu kwa nini Kamishna wa TRA alundikiwe kazi nyingine badala ya kuweka kipaumbele kazi yake kuu ya kukusanya kodi.

Wapo watu wengi tu wa kufanya hii kazi ya Uwenyekiti wa Bodi kwa ifanisi kuliko Kamishna wa TRA
 
Ni kitu cha kushangaza sana. NMB ikifanya kosa lolote la kijinai au madai lazima Mwenyekiti awajibike, sasa huyu Mhende amewekwa sehemu ambayo hawezi kutetea benki au serikali na wala wateja!
 
Back
Top Bottom