Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,816
- 12,264
Jana Kamishina wa Mamlaka Kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya (DCEA) Bw. Lyimo alitangaza kumnasa mmoja wa Mapapa wakubwa duniani wa biashara ya madawa ya kulevya akiwa na wenzake watatu. Papa huyo aliyekamatwa na zaidi ya gram 600 za cocaine hajatajwa jina hivyo hakuna mwananchi ye yote anafahamu.
Kitendo cha Kamishina Lyimo kuficha jina lake kinatia shaka kwa kuwa kinatengeneza mazingira ya Papa huyo na wenzake kufanya mazungumzo ambayo yanaweza kupelekea kuachiwa huru kwa rushwa.
Kwa vyo vyote vile Papa hilo lina utajiri mkubwa kiasa kwamba kutoa rushwa ya mabilioni ya fedha ili liachiwe siyo tatizo. Hivyo ni vema Papa hilo na wenzake watajwe majina yao na mahali wanapoishi ili wafahamike na wananchi waweze kuwa na tahadhari nao.
Pia soma: Chalamila: Wakubwa wa madawa ya kulevya tumewakamata, hatuwataji