Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!

Wanabodi,

Declaration of Interest
Pasco wa jf, sio tuu ni Mtanzania Mzalendo wa nchi hii, pali pia Mjeda. Once Mjeda, Always Mjeda. Kila Mtanzania, anapaswa kuwa ni mzalendo ila anaweza asiwe mzalendo na bado akawa ni Mtanzania ila kila Mjeda ni lazima awe mzalendo! .

Hadithi za Ushupavu wa Kijeshi Vitani.
Hivyo mtu mwenye hulka za kijeshi, kutoonyesha hisia za kuguswa na kuonyesha huruma ya kutembelea eneo la tukio kujionea na kutotoa pole kwa kauli ya sauti si udikiteta bali ni ushujaa na ushupavu wa kijeshi awapo vitani, hivyo kuna majanga mengine ni kama vita, hayahitaji huruma za kubembelezana kwa pole za kufarijiana bali actions za kupanga strategies on how to go about it and move forward !.

Ajira ya kwanza kabisa ya Pasco wa Jf baada ya kumaliza shule na kupitia JKT kwa mujibu wa sheria, aliunganisha moja kwa moja kwa kujiunga na JWTZ, hivyo Pasco wa JF ni Mjeda kamili ambapo ikitangazwa vita, ndio wale askari wa akiba ambao tunaitwa kuingia front!.

Miongoni sifa kuu ya askari yoyote ni nidhamu na kutii amri, hivyo mafunzo muhimu ya wajeda, zaidi ya mazoezi ya vitendo na ukakamavu ni somo la linaloitwa Mbinu za Medani, au MM.

Somo hili linafundisha mbinu mbalimbali ambazo askari Jeshi hutakiwa kutumia akiwa vitani; ambapo nyingi ya mbinu hizo zinahusisha mazoezi ya ukakamavu, ushupavu na uzalendo, ustahimilivu na kutoonyesha hisia zozote za aina yoyote ya huruma wakati wa jambo la hatari linapotokea mkiwa mstari wa mbele vitani.

Mfano unit ikiwa kwenye rake patrol aneo la adui na mkapigww ambush na adui mkaasambaratishwa!, hapo hakuna tena kusubiri amri bali kila askari anatumia "akili mu kichwa" au (self initiative) kujiokoa, hivyo mnaweza kujikuta mmebaki wawili tuu tena wewe na best wako kabisa ambaye amejeruhiwa sana, kumbeba kumuokoa huwezi, na ukimuacha adui wakimkuta na kumkamata akiwa hai ni hatari zaidi!.

Hivyo katika hali hiyo, MM inakuelekeza kuwa inakubidi wewe uweke pembeni urafiki, utu na huruma, umlambishe morphine huyo askari aliyejeruhiwa ili kumpunguzia mateso ya maumivu ya kujeruhiwa,, na ulazimike to take some drastic measures kumsaidia huyo best wako kwa kumuoakoa kwa namna ambayo naomba nisiitaje hapa, (siri za jeshi ), unaweza kumtaka akupe salamu kwa familia yake tena ni wewe ndio utazifikisha salamu hizo kwa mkewe bila kusema aliondokaje baada ya kujeruhiwa!

The bottom line, ni kuwa askari vitani unatakiwa awe jasiri sana na usiwe na huruma hata kidogo!, sometimes unawajibika kufanya ukatili wa ajabu kabisa kwa best wako, hata kwa ndugu yaki, ikiwa ukatili huo ndio njia pekee ya kumsaidia, kujisaidia wewe mwenyewe kulisaidia taifa lako!, hivyo msamiati wa "Utu" na kupeana pole jeshini kwenye mstari wa mbele hakuna!. Huo ni ujasiri na ushupavu wa kijeshi na si ukatili au udikiteta!.

Ujasiri na ushupavu wa aina hiyo ya kijeshi jeshi unapozidi huku uraiani ndio hutafasiriwa kama ni udikiteta!. Once ukiwa ni dikiteta, always ni dikiteta! .

Dikiteta maarufu zaidi duniani nadhani kuliko madikiteta wote, alikuwa Adolf Hitler, huyu anasemekana alisisitiza nidhamu ya hali ya juu kwa mtutu wa bunduki ambapo alinyoosha mistari ya vikosi vyake kwa risasi za moto usawa wa kichwa!, ukikaa nje ya mstari, unakwenda chini!. Kufuatia unyooshaji huu, kiukweli mistari ilinyooka wima!, hivyo sisi Watanzania inatubidi tuwe wavumilivu tuu mistari yetu nayo itanyooka tuu! .

Ni katika strictness hii ya kunyoosha mistari ilifanya Hitler kuonekana kuwa ni kama dikiteta na kweli baada ya mistari kunyooka, alinyoosha kila kitu kwa jeshi style hadi kutaka kunyoosha a pure breed ya Wajerumani pure hivyo kufanya ile genocide ya Holocaust kwa ukatili wa hali ya juu kabisa ambao uligeuka ni hulka au tabia tuu ya mtu kwa kama kugeuka kuwa ni dikiteta halisi aliyeanza kwa kusisitiza tuu nidhamu ya kunyoosha mstari ya vikosi vyake kwa risasi za moto na aliweza kufanya vile kufuatia kutokuwa na hisia kabisa za kuonyesha huruma au kuguswa na utu kuhusu uhai wa askari wake!. Kwa Hitler kilichohitajika ni mstari kunyooka, atakayepindisha mstari, hatujali utu wake wala uhai wa roho yake bali tunacho jali ni mstari tuu unyooke! .

Sasa swali ni kunapotokea janga kubwa la Kitaifa lililopoteza maisha ya watu, mtu unaweza kuwa ni kweli unajali sana na unafanya mambo makubwa sana kuhusiana na janga hilo behind the scenes , lakini kitendo tuu cha kutotamka kwa kauli ya sauti yake kwa kusema neno moja tuu "Poleni!", kunaweza kupelekea kutafasiriwa kuwa mtu huyu hajali na hana huruma ambazo ni hulka za kidikteta! .

Sasa jee Inawezekana huku kuonekana kama kutojali kunauwezekano kukawa ni baadhi ya traits za udikiteta ule kama wa Hitler kunyoosha mistari ya askari wake kwa risasi au ni ule ujasiri, ushujaa na ushupavu wa MM kwa askari jeshi akiwa hatarini kwenye mstari wa mbele kuwajibika kutoonyesha hisia za huruma na kupeana pole za kauli bali hapa ni kuchapa kazi tuu pole baadaye baada ya mambo kutengemaa?!.

Hisia zipo, na kuguswa pia kupo, ikiwemo kujali kwa hali ya juu kabisa behind the curtains , lakini kutoonyesha hisia za kuguswa, kutoonyesha kujali kwa kauli na matendo ya kutosikika ukisema neno lolote kwa kauli na kutoonekana kabisa kwenye eneo la tukio, jee kunaweza kuwa kunachangiwa na hulka na tabia za kidikteta? au ni ule ushujaa na ushupavu wa askari jeshi akiwa vitani kwenye mbinu za Medani, MM?!.

Nauliza pia, kunapotokea janga halafu mtu ukatuma tuu salamu za pole kwa taarifa ya maandishi bila kutamka pole yoyote kwa kauli ya sauti yako, au bila kuonekana kwenye eneo la tukio jee kunaweza kutafasiriwa ni kutojali na kutoguswa au ni kuguswa na kujali kimya kimya!.

Na jee, pole ya kuguswa na kujali wazi wazi na pole ya kuguswa na kujali kimya kimya ipi inafariji zaidi? , au ipi inafaraja zaidi? .

Nawatakia Jumamosi Njema.
Pasco
Pasco# umeongea mengi lakini amini me nipo ktk jeshi la dunia tumekuwa Afghan, Iraq na hapo Africa.
Unachotetea si ubinadamu wala utu, pole ya makaratasini haibebei mguso ndo maana hutashangaa ukiona kina Obama, Bush wamekuwa na desturi za kufika pale tatizo lilipotokea.
Utakumbuka kisa cha mafuriko kule ktk jimbo la New Jersey, Obama alikatiza safari akaenda japo Gov.Christie ni Rep.
So usitete hoja zako kwa kutumia mifano ya jeshi.
Hujaona vita wala huijui vita, so plz acha kuwatisha raia.
 
Hadi Jumatano atakapokuwa anatoa misaada mtabadilika na kuanza kusema kumbe kimya kingi kina mshindo
Hahahaha. Wewe umetoboa. Jirani yetu ameumia sana, hakusubiri kupiga simu na kutuma msaada. Hakuitisha harambee. Mwezi wa 10 huu, trillion kila mwezi ziko wapi?
 
Bro unahaha sana kupata attention, unatamani ungekuwa game changer wa siasa hizi...
Pole!
Mkuu Mphamvu, ni vile tuu watu humu hatujuani in reality hivyo kuwachanganya the game changers na attention seekers! .

Pasco wa JF atafute attention kwa nani ili iweje?!. Kwa kukusaidia tuu, sio tuu ni kabila moja, bali nikienda Chato hata Biharamulo, nafikia kwake! . Aliyeripoti uchaguzi mdogo wa Biharamulo humu jf ni mimi na sio tuu nilifikia kwake bali Janet ndio alitupikia!, hivyo ni seek attention ya nani for what! .

Pasco
 
Jana ulisema ukimya wake "something is wrong" leo unasema ni ushujaa, kwa sisi tunaokujua hatushangai undumilakuwili wako labda wageni wa hii nyumba.
Mkuu Quinine, ukimya wa kutokusema neno kwa kutakuwa na neno la kusema ni jambo moja, na ukimya wa kuwa na neno la kusema lakini ukaamua kutokusema hilo neno kwa kukaa kimya ni jambo jingine! .

Pasco
 
Hivi uongozi wa mbinu za kijeshi na Mbinu za kidikteta una tofauti gani...?
Ndio ule ule na Tanzania hapa tulipo fikia tulimuhitaji sana kiongozi dikiteta mzalendo mwenye anayekerwa na rushwa na ufisadi toka ndani ya nafsi yake hivyo anaufanya huu udikiteta wake kwa nia njema kabisa ya kulikomboa taifa hili toka kwenye lindi la umasikini uliotopea uliogubikwa na rushwa na ufisadi.
Pasco
 
Hahahahahaha kwani jeshini kuna bahasha za khaki? maana ulivyozoea bahasha naona kabla ya vita utataka kujua mshiko ni kiasi gani?
Mkuu Makuta, JWTZ ndio appointment yangu ya kwanza kabla ya uandishi!. Kule ni kula bure!, kulala bure!, fedha za mshahara ni kulewa tuu na kuhonga! ,sasa bahasha za nini? .

Bahasha nimezijulia kwenye media!.

Pasco
 
Hadi Jumatano atakapokuwa anatoa misaada mtabadilika na kuanza kusema kumbe kimya kingi kina mshindo



"Ubinadamu Kazi", Utu wa mtu haupimwi kwa wingi wa mali alizonazo au kwa wepesi wake wa kumwaga fedha pindi yatokeapo majanga.Huruma ya mtu haipimwi kwa michango yake ya kifedha,bali kwa kuonesha kuguswa na kukubali kuacha vyote na kuungana na watu wake ili augue,ahudhunike,alie na kuomboleza pamoja nao.

Upendo hauna mwakilishi!,hauwakilishwi kwa fedha wala kwa kutuma ujumbe wa watu wengine waende kwa niaba yako,huwezi kuonekana kuwa unalia na kuomboleza na watu waliopatwa na majanga kwa wewe kujifungia mahali kwa siku kadhaa kisha uibuke katika eneo la tukio kwa mbwembwe halafu uonekane ulikuwa pamoja na waombolezaji.

Kushirikiana na jamii pale yatokeapo majanga ni tendo la kiutu linalodhihirisha upendo wako kwa jirani zako.Misaada huwa sehemu ya faraja pale itolewapo baada ya mhusika kwenda eneo la tukio kujionea hali halisi,kuona jinsi watu wanavyoteseka,kuwasikiliza mahitaji yao na kilio chao.Kujifungia ndani kisha ndipo ukusanye " mazagazaga"na kwenda kuyabwaga kwa waathirika ni ishara ya kiburi na majivuno yanayotokana na nafasi(uwezo)uliyonayo.

Huku kwetu mtu asipokuwa na ushirikiano na wenzake(wananzengo),badala yake akatumia "Ukwasi" wake kuonesha jeuri yake kwa matatizo ya wenzake na yeye asihudhurie katika matatizo hayo,jamii itamfanyia vivyo hivyo pale naye yatakapomkuta.Atafanyiwa kila kitu na kupata kila kinachohitajika,lakini hawatahudhuria katika tukio lenyewe.

Badala ya kusubiri kuonesha mbwembwe,anapaswa kujitokeza kwa haraka katika majanga ya aina hii ili kuonesha kuguswa kwake na Shida za watu wake.Kutoonesha kuguswa na matatizo ya wenzako si ushujaa bali ni dalili za wazi za kutokuwa na "Emotional Intelligence".
 
Mkuu Mphamvu, ni vile tuu watu humu hatujuani in reality hivyo kuwachanganya the game changers na attention seekers! .

Pasco wa JF atafute attention kwa nani ili iweje?!. Kwa kukusaidia tuu, sio tuu ni kabila moja, bali nikienda Chato hata Biharamulo, nafikia kwake! . Aliyeripoti uchaguzi mdogo wa Biharamulo humu jf ni mimi na sio tuu nilifikia kwake bali Janet ndio alitupikia!, hivyo ni seek attention ya nani for what! .

Pasco
Loh, kutajataja wanasiasa mwenzio naogopa. Usinitege tafadhali... Ninachojua maisha ni mchakato. Hata mie niliwahi kula msosi wa kupikwa na Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani. So what?
 
Back
Top Bottom