Kutokuwepo kwa umeme kila siku asubuhi na jioni mpaka usiku, tatizo ni nini?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Kuna mambo yanayoendelea mpaka unajiuliza, hivi nchi hii hatuna watu wenye akili, uwezo na dhamira safi ya kuendeleza Taifa?

Nimesafiri na kukaa kati ya wiki moja hadi mwezi mmoja kwenye mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mara. Yanaoendelea katika maeneo haya kuhusiana na nishati ya umeme ni maafa, upuuzi na kioja kikubwa. Sijui hali ipoje kwenye mikoa mingine. Ni kama nchi haina huduma ya umeme.

Karibia kila siku, kuanzia saa 2.30 hivi asubuhi umeme unakatika. Unaweza kurudi muda wa mchana au jioni, na ifikapo kwenye saa mbili usiku unakatika tena, kurudi ni usiku wa manane.

Nimewahi kusafiri siku za karibuni, kuanzia mwezi July mwakajana nchini Burundi, Rwanda, Msumbiji, South Africa, Zambia, Ghana na Mali, kwa nchi za Afrika. Katika nchi hizo, hakuna hata siku moja nilishuhudia umeme unakatika.

Katika tekinolojia rahisi kabisa Duniani, ni pamoja na uzalishaji wa umeme. Usafirishaji na Usambazaji wa umeme, hata huwezi kusema ni tekinolojia, ni kazi tu ya kawaida ya kuunganisha wire, ku=stepdown umeme mkubwa na kuwaunganishia wateja.

Hata umeme tu tunashindwa!! Hivi nchi hii ni kitu gani tutaweza? Biashara ya mabenki tumeshindwa, viwanda tumeshindwa, simu tulishindwa, kilimo tumeshindwa, demokrasia tumeshindwa, kuheshimu haki za binadamu na utawala bora tumeshindwa, kujenga uchumi mzuri tumeshindwa, kutengeneza ajira tumeshindwa, Sayansi ya tiba tumeshindwa. Tumebakia kusifiana hata pale ambapo hakuna cha maana tulichofanikiwa, na watu kupeana degree za udaktari wakati hao watu upeo na ujuzi wao katika fani wanazopewa shahada, wengi wao ni chini hata ya mtu mwenye certificate huko kwenye mataifa yaliyoendelea.

Kati ya mashirika yaliyojaza watu wenye uwezo duni kabisa na ufanisi zero ni TANESCO. Huko ndiko kuna wahandisi ambao hawawezi kujenga hata njia ya umeme yenye urefu wa kilometa 50. Huko ndiko kuna wahandisi ambao hawawezi kutengeneza mradi wa umeme wa maji kwa kwaajili ya matumizi ya kijiji kimoja. Huko ndiko kuna watu ambao hata reasoning ya kawaida, hawana. Wanaweza kukuambia hakuna nguzo, mteja anunue nguzo, agharamie wire na kila kitu, akishagharamia wanasema kila kitu ni cha TANESCO, halafu wanaunganishia wateja wengine kuanzia pale bila hata ya angalao kumrudishia gharama yule mteja wa mwanzo aliyeufikisha umeme mahali hapo. Na hapo kuna waziri, kuna mkurugenzi na maafisa mauzo, na wote wanajiona ni wazima, wana akili timamu na wana uelewa juu ya misingi ya kibiashara.

Wahandisi majina, uwezo sifuri wamejaa TANESCO. Nakumbuka kuna wakati kulikuwa na mradi wa umeme wa kijiji kwa ufadhili wa Kanisa katoliki, fedha ikitoka kwa wafadhili wa parokia moja huko Ujerumani. Paroko wa kijiji hicho akaenda kuonana na Mkuu wa Mkoa kuomba kupatiwa mtaalam wa umeme wa kufanya tathmini ya mradi mzima ikiwa pamoja na kutafuta maporomoko ya mto. Mkuu wa mkoa alijigamba kuwa watapeleka mtaalam mhandisi ambaye ni the best kwenye mkoa. Mhandisi huyo alikwenda kijijini hapo, akakaa miezi miwili, alichokiandaa, kilipopelekwa Ujerumani kilionekana ni takataka, na Paroko yule anasema aliulizwa kama mara nne hivi kama kweli anaamini huyo aliyeandaa report ile alikuwa ni mhandisi. Ikabidi kule Ujerumani wamtume technician. Akaenda akaa kijijini hapo siku 10, alikuwa amemaliza kazi, na baadaye alienda kusimamia ujenzi wa mradi, mpaka leo umeme upo.

Kwa ujumla, taasisi nyingi za Serikali na mashirika ya umma, kuna wataalam majina, kikubwa wananchokijua ni kuandaa bajeti za posho, lakini kiutendaji ni zero. Ndiyo maana hakuna shirika lolote la umma au taasisi ya Serikali yenye ufanisi mzuri. Angalia, Serikali ilifeli kabisa kwenye mawasiliano ya simu wakati leo makampuni yameeneza huduma ya mawasiliano ya simu mpaka vitongojini. Serikali ilishindwa kabisa kuzalisha hata bia, sigara, sabuni, sukari, n.k; makampuni yameeneza huduma na bidhaa kila mahali mpaka wateja kubembelezwa. Tulikuwa na kampuni ya ujenzi wa barabara ya MECO, mwaka mzima ikipewa kazi ilikuwa inaweza kujenga kilometer moja, na haitakamilika, na ikikamilika, basi baada ya mwezi mmoja mashimo yanaanza kutokea. Tulipoleta makampuni ya Japan, kama KAJIMA, ilikuwa mshangao mkubwa jinsi wajapan hao wanavyoweza kufanya kazi huku watendaji wakuu ni hawa hawa Watanzania lakini wasimamizi ni Wajapan.

Jambo moja lililo dhahiri kwenye makampuni haya yenye ufanisi, japo watendaji wakuu ni watanzania, uongozi wa juu kabisa ni wa watu wageni.

Hakuna nchi yoyote ambayo inaweza kupata maendeleo bila ya uwepo wa nishati. Ndiyo maana kati ya vigezo/vipimo vya maendeleo, kimojawapo ni wastani wa matumizi ya nishati kwa kila raia.

Bila kuiua TANESCO, tukawa na makampuni binafsi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme, kila siku itakuwa ni ngonjera za miaka yote, lakini hakutakuja kuwa na umeme wa uhakika. Watu waliomo kwenye mashirika yanayosimamuwa na Serikali, na Serikali yenyewe, hawana uwezo wa kufanikisha chochote. Huduma zote zinazoamua ustawi wa watu na uchumi, Serikali ijitoa kwa sababu imedhihirika wazi kuwa haina uwezo.

Kama tumeshindwa, ni afadhali hata hiyo TANESCO wapewe wageni ili angalao wananchi wawe na uhakika wa huduma.

Tunakoenda, ni aheri hata mawaziri wasiwe wabunge wala wanasiasa. Wateuliwe hata watu wa nje ambao wana uwezo. Kama hatutaki TANESCO kuibinafsisha, basi nafasi za juu za menejiment ya TANESCO zisiwe za uteuzi, zitangazwe kote Duniani, wenye uwezo waombe na waajiriwe kwa kupewa tasks zinazoeleweka. Waarabu walifanikisha kwa namna hiyo. Emirates airlines ilijengeka sana na kupanuka kuanzia miaka ya 2000 ambapo waarabu walimwajiri Mwingereza Tim Clark kuwa Airline Executive. Baadaye baada ya mifumo kujengeka na kuimarika, walianza kuwapunguza wageni, japo mpaka keo bado kuna wageni wengi ndani ya shirika.
 
Inamaana mleta mada hujajua kama tatizo ni waziri?
IMG_20211228_160309.jpg
 
Kuna mambo yanayoendelea mpaka unajiuliza, hivi nchi hii hatuna watu wenye akili, uwezo na dhamira safi ya kuendeleza Taifa?

Nimesafiri na kukaa kati ya wiki moja hadi mwezi mmoja kwenye mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mara.
Leo ndio siku watu makini wameamua kuwa makini.kuna majitu humu kazi yao ni kufurahia uhuru bila tafakuri.

Siasa za nchi hii wanasiasa na wafanyabiashara wameunda Cartel ya ktufilisi watanzania!

Wanasomesha Ulaya na kutuibia wakificha Ulaya hukohuoko!

Kinachoitwa mikopo kwa wingi ni Ubadhirifu wa fedha za wazumgu ..zinaletwa halafu zinarudi kwa mlamgo wa nyuma na kufichwa Ulaya.

Kinachosalia wanapewa watukuzaji ili wapige mapambio na zumari kuuhaadaa Umma kwamba zomeingia zilikotakiwa.

Lakini kiuhalisia washika rote wejipanga!
 
Kuna wakati walisema wameleta teknolojia ya kurekebisha miondombinu ya umeme bila kukata!
Hii Wizara, kwa ujumla inaongoza kwa porojo. Wizara ya nishati, na TANESCO ni kiwanda cha hadaa. Kila mwaka kila wakati watasema kuwa tunafanya hiki, baada ya hapo mgao au kukatika kwa umeme kutakuwa historia, lakini kitakachoshuhudiwa ni huduma hovyo zaidi.

Kukitokea upungufu wa mvua, wamepata sababu ya kusema mabwawa hayana maji wakati umeme mwingi kwa sasa hauzalishwi kwa maji. Zikija mvua nyingi, wamepata sababu ya kusema nguzo zimeoza na nyingine kuanguka kutokana na mvua nyingi zinazoendelea. Kukiwa hakuna mvua na mabwawa yamejaa maji, watasema, tunarekebisha mifumo ili kuondoa kabisa tatizo la umeme nchini. Ni watu wa maneno ya hadaa, lakini utendaji ni zero.
 
Kuna mambo yanayoendelea mpaka unajiuliza, hivi nchi hii hatuna watu wenye akili, uwezo na dhamira safi ya kuendeleza Taifa?

Nimesafiri na kukaa kati ya wiki moja hadi mwezi mmoja kwenye mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mara. Yanaoendelea katika maeneo haya kuhusiana na nishati ya umeme ni maafa, upuuzi na kioja kikubwa. Sijui hali ipoje
Maneno mazito sana !! Lakini wengine watakuwa wanapita na kusonya tu !!
 
Leo ndio siku watu makini wameamua kuwa makini.kuna majitu humu kazi yao ni kufurahia uhuru bila tafakuri.

Siasa za nchi hii wanasiasa na wafanyabiashara wameunda Cartel ya ktufilisi watanzania!

Wanasomesha Ulaya na kutuibia wakificha Ulaya hukohuoko!

Kinachoitwa mikopo kwa wingi ni Ubadhirifu wa fedha za wazumgu ..zinaletwa halafu zinarudi kwa mlamgo wa nyuma na kufichwa Ulaya.

Kinachosalia wanapewa watukuzaji ili wapige mapambio na zumari kuuhaadaa Umma kwamba zomeingia zilikotakiwa.

Lakini kiuhalisia washika rote wejipanga!
Kuna mambo nimeyashuhudia, lakini siwezi kuweka wazi hapa maana nikiweka nitakuwa nimeanika jina langu.

Kwa dhati ya moyo, na ukweli ulio wazi, japo wengine watasema nilete ushahidi, kitu ambacho siwezi kufanya hapa kwa sasa, lakini wenye imani waniamini (maana imani ni kusadiki bila kuona, kama hekima yako inakuongoza na kuona kinachosemwa kina mantiki), kuna watu, tena walio karibu na Rais, wanajitajirisha kwa kila namna, na mara nyingi kwa kutumia jina lake, kwa vile tu wapo karibu naye.

Rais awe makini, kuna watu wanaomzunguka na walio karibu naye, hawana hata chembe ya uadilifu, wao wanachohangaikia ni kujitengenezea utajiri kupitia jina lake. Na hawa watu wamekuwepo wakati wote, walikuwepo wakati wa Kikwete, walikuwepo wakati wa Magufuli, na wapo hata sasa. Sijui na sina uthibitisho wakati wa Mwinyi na Mkapa. Lakini vipindi hivi vitatu nina uthibitisho.

Nyakati hizo zote, wasaidizi hao ili kuukupa nafasi ya kumwona Rais, lazima utoe hela ya maana kwao. Hiyo pesa siyo kwamba anapewa Rais, ni ya kwao. Na nina uhakika, Rais hajui. Wakati wa Kikwete ilikuwa kuanzia sh 20m kwenda juu. Wakati wa Magufuli ilifika mpaka shilingi 400m. Na kwa sasa, imefika mpaka milioni 200.
 
well said

tatizo ni mifumo mibaya ya uendeshaji na sera mbovumbobu za nchi,
hiyo kauli ya marekebisho imeanza kusemwa toka miaka ya 2000 lakini hakuna improvements zozote zaidi ya swala kama hili kuingizwa kua jambo la kisiasa,,

 kwenye shirika mtu anateuliwa kufit hali ya kisiasa sio kufit katika kuliendesha shirika,

kama ulivyosema hizi kazi za mashirika ya uma ziwe zinatangazwa kama kazi ili mtu yeyote anayekidhi vigezo aajiriwe kama ajira nyingine sio kila kitu kuteuliwa tuu tuuu

angalia mashirika yote ya uma yanajiendesha kwa hasara,sio kwa hasara kwasababu hayaingizi hela bali ni kwa usimamizi mbovu wa hawa wasimamizi wa kuteuliwa

kama hao TANESCO ni hovyo kabisaa,sahivi napoongea hapa umeme umekatika na wananchi hatujui nini sababu ya kukatika,hii awamu tutaisoma namba dadeki,
hata umeme kukatika ni Laana
 
MIAKA 60 YA UHURU HAKUNA TUNACHO KIWEZA.

HAKUNA WIZARA AU SEKTA YA KUJIVUNIA.
NI WIZI, MAGUMASHI, UPUMBAVU MTUPU.

HII NCHI YA HOVYO SANA
Inasikitisha na kuleta hasira.

Tatizo kubwa ni uongozi. Hatuna bahati ya kuwapata watawala wenye maono. Mwalimu Nyerere alisema ili uendelee unahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Tumekosa viongozi bora na siasa safi.

Watawala wanatangulia kuwa na majina badala ya sifa zinazotakiwa. Mtawala anakuwa na majina ya watu ambao ni lazima wapate madaraka, halafu anaanza kutafuta pa kuwapachika, badala ya kutangulia kuwa na sifa zinazotakiwa kila mahali, halafu ndiyo aangalie ni nani mwenye sifa hizo kwa wakati huo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom