Kutokuvaa tai na kwenda na makobasi kwenye interview ya oral imekaaje?

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,711
Ni kwenye usaili pale utumishi kuna wengine walienda na makobasi kabisa sasa nilitaka kuuliza hivi Utumishi kwenye masuala ya appearance huwa hawajali sana.

Maana watu tulikuwa casual mno hata tai hatukuvaa wengine.

Hivi inaweza kuppteza marks kweli?
 
Achen Utan,,,,,,mavaz yana umuhim wake jaman tusidanganyane

hakuna anayekataa mavazi yana umuhimu wake lakini hizi nguo tunazoziita za ofisini ukikaa mtaani bila kazi kwa muda mrefu huwezi kuwa nazo utaishia kuvaa jeans tu.....vile vile habari ya tai me mwenyewe na kisomo changu kuifunga siwezi....
 
Smartness ina %ge yake asikudanganye mtu.
Hata uwe na kichwa vipi, jinsi ulivyotokelezea kwenye interview ina matter kwa sana tu pia.
 
mmm ila kuvaa vizur kunahusika sana tusijitetee. aikaruwa1983 Tan'gana yaani tai ya buku tatu suruali ya buku kumi na shati hata la buku saba mtu anakosa... hapana kabisa sio sawa
 
Last edited by a moderator:
You must be smart in both, dressing and addressing!Kwanza ukiwa na muonekano nadhifu tu ni sababu tosha ya kuwa na reasonable confidence kwe interview kuliko ukiwa umevaa mashakamashaka umo mwilini.
 
hakuna anayekataa mavazi yana umuhimu wake lakini hizi nguo tunazoziita za ofisini ukikaa mtaani bila kazi kwa muda mrefu huwezi kuwa nazo utaishia kuvaa jeans tu.....vile vile habari ya tai me mwenyewe na kisomo changu kuifunga siwezi....

Isu co kuvaa tai au suti lkn mwonekano wako in term f mavaz lazma uonekane safi,,,,,we ishia kuvaa kobasi utakua kila cku unalalamika unakosa kazi,
 
Ni kwenye usaili pale utumishi kuna wengine walienda na makobasi kabisa sasa nilitaka kuuliza hivi Utumishi kwenye masuala ya appearance huwa hawajali sana.

Maana watu tulikuwa casual mno hata tai hatukuvaa wengine.

Hivi inaweza kuppteza marks kweli?

Nashukuru Mungu wakati nasoma Chuo kuna mama mmoja (Mwalimu) alikua anapenda sana tuvae kiheshima hata mimi nilishangaa juzi baada ya kufika Maktaba Complex baadhi ya Wasailiwa wamevaa Jinsi, Sandoz, Kadeti za ajabu ajabu, Mamiwani ya Jua, Shanga(Culture) Shingoni, Kimkanda kiunoni chembaba kama utambi wa Jiko, Tai lenye maua maua hata haliendani na nguo alizovaa , Vimini, Mlegezo nilisikitika sana kuwaona vile Casual mno bora mabinti kidogo walijitahidi ila kwa sisi wanaume hali haikua nzuri Waliowengi wamefuga mizuzu wengine wametelekeza tuu Madevu yao wakati hata wale wanaotufanyia interview hakuna mtu aliyekua na Ndevu (yaani wamezinyoa) . Kwenye written ndo unaweza kwenda Vile jamani lakini siyo kwenye oral wengine hata selection ya viatu tuu inamshinda mtu kavaa suruali ya kitambaa na Ma American Buti makubwa vituko tupu kwenye oral wanafuatilia hata mavazi na U smart wako jamani tuwe makini. Ila nilochokiona Utumishi kinasikitisha yaani over tunasubiri lecture na siyo interview.

Pia utumishi wa Uma walitoa Dressing code na Orodha ya mavazi yasiyotakiwa.
 
Kama unataka ajira UTUMISHI WA umma KATIKA SUALA la mavazi kuna waraka elekezi unaelekeza mtumishi WA umma avaeje pamoja na picha zake nazani OFISI za umma ukiomba picha zake utapewa.kila sehemu na. Miongozo YAKE ndo maana mgodini au kiwandani au bandarini unaambiwa lazima uwe na helment na reflectors
 
Hizo oral hawa consider sana chamuhimu ni kichwani. Mm huwa nasafiri usiku ambapo huwa navaa tai lakin kutokana na hekaheka za usafiri najikuta n bora nivue tu hiyo tai, maana inakuwa imechafuka, imejikunja kunja, mara jasho shngoni na mikonon mwa shati maana huwa napendelea kuvaa white. Mara nyng kabla cjafika eneo la tukio huwa natoa tai na kuiweka mfukon. Km wanatambua kuwa watu weng wanatoka mikoan kuja dar for interview hawawez wakacomplicate issue ya tai
 
Mkuu elewa somo isu co tai.... Tunangalia umuhim we kuvaa vizur kwny oral intrvw
 
Mkuu elewa somo isu co tai.... Tunangalia umuhim we kuvaa vizur kwny oral intrvw

Unakichwa kigumu sana kuelewa jambo, hata vazi la tai lmehusishwa ndan ya maelezo yake. Mm cjatunga majibu toka mbingun bali nmejibu kipande kutoka kwenye maelezo yake
 
Kama ulivaa hivyo na wakakupa kazi basi mimi nitakuzawadia Tsh 300,000/=!
 
msingi ni kuvaa kawaida tu siyo lazima tai unavaa suruali yako kama ni mvulana unachomekea vizuri viatu vya kawaida alafu unaweka mkanda simple mweusi nywele at least zisiwe ndefu sana pia mara6shi yasiwe na harufu kali kama unataka.
Kwa wadichana suruali ya heshima sanasana iwe suti au sketi ya kawaida isiwe fupi.sana na kiatu simple.
Utiambiwa tell us about yourself unaongea confodently jina lako kamili umri.na uraia alafu unasema unaanza na elimu kuanzia std 7 ........
Ukimaliza unaanza na experience alafu unamaliza na abilities and awards. Unawambia nashukuru sana
Watakuuliza utasaidiaje jamii katika shughuli za.maendeleo ya jamii unawambia
Utawaelimisha elimu ya watu wazima, voluntarism, access to technology na ownership ya ardhi
Wanakuuliza kwa nini wanajambii hupaswa kushirikihwa kwenye shughuli za maendeleo ya jamii unawaambia
Harmonization, sustainability, ownership, decision na avoiding conflict of interests
Wanakuuliza components za reserch unawaambia zipo nne au kumi wanakwambia taja tano unawaambia
Title, introduction, hypothesis, literature review and methodology
Wanakwambia uwape qualities za cdo unawaambia
Ethics, political neutrality, deligence, respect to human right na decisive. Wanakwambia unamaana gani kwa ethics unawaambia moral.standards like wearing style na lg use.
Yule mama anakuambia tumefikia mwisho wa kukuinterview matokeo yatakuwa kwenye website yetu so tembelea mara kwa mara mwanangu ujue kama umechaguliwa.
Unasema asante unawashika mkono wa upendo unatoka nje unamshukuru Mungu unasubiri
Baada ya wiki tatu matokeo yanatoka unachaguliwa unakuwa.mtumishi wa umma.
As simple as.that my dear
 
Back
Top Bottom