Kutoka ZIRPP: Abdallah Kassim Hanga na mapinduzi ya Zanzibar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
KUTOKA ZIRPP: ABDALLAH KASSIM HANGA

Yaliyotokea kifo cha Abdallah Kassim Hanga

Mohamed Said
Toleo la 405
13 May 2015

1tc4plj0bIg81BMLMPamUdLARA-pozwHec-dyHC6XXzutYysJEJozGnL5XlcSMhta9dKbcBMo14L7Aa54rwkzTXX2QFywKeUz4WaTh47UaUlzF_YDIX8td2KLKFFKUpR4LLtI936nEL5NexHxL1VKEvJNP0P4nWtGIOvLENRlTfh=s0-d-e1-ft

WAKATI Dk. Harith Ghassany anaandika kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' siku moja usiku alinipigia simu kutoka Washington. Wakati ule mimi naishi Tanga. Dk. Ghassany akaniuliza kuhusu Abdallah Kassim Hanga aliyewahi kuwa Waziri baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nadhani katika mazungumzo yetu siku za nyuma nilipata kumweleza kuwa nilimfahamu Hanga katika utoto wangu. Baada ya kumpa kisa hiki sikumaliza akanikatisha na kuniambia angependa anirekodi katika kinasa sauti ili atumie maelezo yangu kwenye kitabu. Hapa chini ndiyo niliyosema kuhusu Hanga na ndivyo yalivyo katika kitabu:

''Mimi nikiishi na baba yangu mtaa wa Somali, namba 22. Klabu ya mwanzo maarufu ya Kilwa Jazz Band ilikuwa kwenye nyumba ya mama yake Abdu Kigunya. Mbele ya nyumba yao ikifika kama saa tisa, kumi, laasiri, wazee walikuwa wanaweka jamvi pale, wanacheza bao. Sasa hivi ukienda pamejengwa majumba ya maghorofa.

"Hanga akija pale mtaa wa Gogo, kona na Mtaa wa Mchikichi, nyumba ya kona barazani wazee wametandika majamvi wanacheza bao. Mimi nilimjuwa Hanga kwa sababu nikimuona kwenye magazeti. Na wakati ule mawaziri wakitembeya na yale magari meusi yakiitwa "Humber." Sikumbuki kumuona Hanga kuja pale na gari.

"Basi ikapita, Mapinduzi Unguja yakatokea sisi wadogo, hatujui nini kinachotokea. Mwaka 1967 nadhani, pale Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Anatoglou Hall, tukicheza mpira wa miguu pale. Mambo yalianza Mnazi Mmoja katika mkutano wa hadhara. Hanga katolewa jela Ukonga kaletwa pale kuadhiriwa na Nyerere. Sisi ni watoto, mambo yale na nyimbo zile lazima tujumuike. Hanga akaletwa pale. Namuona Hanga mimi kwa macho yangu ya kitoto na miwani yake ile.

"Hanga alikuwa mwembamba na mrefu na alikuwa na thick hair. Alikuwa mtu mwenye kupendeza. Kaja pale na uso ulionyong'onyea. Lakini sisi hatujui kinachotendeka. Watoto wa Kiswahili miaka 14, 15, 16, ni wadogo. Hatujui kinatendeka nini. Lakini mimi najua kuwa yule pale Hanga namuona kuwa ni mfungwa.

"Hanga miwani iko puani uso umemparama kama jiwe la kiama, madevu yamemjaa. Anaadhiriwa! Jua la saa sita mchana linampiga vizuri. Kwa pale kukaa na kajiinamia nilijuwa kuwa mambo si mazuri. Nyerere pale anazungumza na wote wanasikiliza. Nyerere unajua. Nyerere alikuwa ni orator (mzungumzaji mzuri).

"Na kuna kumuuwa mtu kiungwana. Nakumbuka incident moja Nyerere anamuonyesha kidole Hanga anasema "hili, hili, hili. Hana lolote. Hakuna lolote anaweza kufanya huyu. Afadhali huyu mwanzake [Babu]." Ukitizama kwenye Tanganyika Standard, wakati ule bado halikuchukuliwa na serikali, wakati ule mhariri ni yule Muingereza, Brandon Grimshaw.

"Utakuta full page. Mimi kwa jicho langu nimeona kwa sababu baba yangu mimi akinunua lile gazeti. Picha ya Hanga iko mbele na madevu na miwani yake ile. Si mimi tu, watu wengi wanakumbuka hiki kisa. Mimi baba yangu rafiki zake walikuwa Jaha Ubwa, Twala…Wakitembeleana zamani wakati wa pasaka. Baba yangu alikuwa memba wa band ya Black Birds ya Bwana Ally Sykes.

"Nadhani kule ndo walikofanya urafiki na hawa jamaa wa Zanzibar. Picha yangu mimi ya Mzanzibari, wakija kule nyumbani, unamuamkia na suala lilikuwa "wewe umeshahitimu wewe." Na ile ''sophistication'' ya wake zao wakija nao pale, yale mavazi, mabuibui, uturi ule, vile vyakula wakiandaa nyumbani pale.

"Hii ndo picha yangu ya Mzanzibari. Palikuwa na picha pale ukutani ya marahemu father wangu na kina Jaha Ubwa. Ile picha ikapotea pale ukutani. Ikawa haionekani tena. Lakini palikuwa mzee akizungumza habari za akina Twala alikuwa akinong'ona. Nahisi mzee alikuwa ana khofu. Ile ni dalili ya woga. Kitu kibaya kimetendeka.

"Lakini lazima aulize. Vipi mkewe. Watoto vipi? Lakini hawezi kusema kwa sauti. Siku nilipokuja kukutana na Ali Nabwa aliponielezeya habari za Zanzibar, nikamwambia mimi baba yangu alikuwa ana masikilizano na akina Twala na yeye akaanza ku open up sasa. Nikasema duu! Alipotoka jela Ali Nabwa alikuja pale mtaa wa Narungombe na Skukuu.

"Pale palikuwa na baraza maarufu sana ya Saigon Football Club. Nabwa alikuwa anakuja pale. Tukitoka tukikaa pembeni tukizungumza chamber. Nilijua baadaye sana kuwa kumbe alikuwa ametoka jela. Pale ndo nilipoanza kuwaona Wazanzibari kwa sura nyingine sasa. Kumbe zile bashasha zinadanganya?

"Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa mauti yaliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kikatili kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa.

"Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho na kutangulia mbele ya haki yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma na kuhangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa miujiza ya aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake.

Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kwa mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.

"Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa hao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi?

"Fikra za Hanga zilikuwaje pale alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikimpitikia katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali akijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi?

Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah na Masultani wengine waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu, au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde wakata mkonge kutoka Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti?

Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyaasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar.

Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere, ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume.

Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, "Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliyopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui.

Itaendelea wiki ijayo.

CHANZO: RAIA MWEMA
MAONI: Tunaarifiwa hapa "Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa mauti yaliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kikatili kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa".

Kauli hii inayodai kuwa Abdulla Kassim Hanga alikuwa kinara wa mapinduzi si sahihi na haina ukweli wowote. Si sahihi kwa sababu Hanga hajapata kushika wadhifa wowote ule katika Afro-Shirazi, (hata uenyekiti wa Tawi la ASP), seuze kuwa "Kinara wa Mapinduzi". Ukweli wa mambo ni kuwa Hanga hakupanga wala hakushiriki katika mapinduzi ya Zanzibar. Aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais baada ya mapinduzi ya 1964 kutokana na mapenzi aliyokuwanayo Mzee Abeid Amani Karume kwake.

Karume alimuona Hanga kama mtoto wake binafsi; alisaidia sana, kwa hali na mali, kumpeleka masomoni USSR na Chicago, USA, kwa masomo ya juu baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu katika chuo cha TTC pale Beit el Ras, Unguja.

Kwa hivyo, kama ilivyokuwa kwa akina Othman Sharif, Abdulaziz Kassim Twala, Aboud Jumbe, Idris Abdul Wakil na wasomi wengine ambao walipewa nyadhifa mbali mbali katika serikali na baraza la kwanza la mapinduzi, Hanga hakuhusika kwa namna yoyote ile na vifo vya Wazanzibari wakati wa/na baada ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa kweli, Hanga ni mmoja miongoni mwa wahanga wengi wa mapinduzi ambaye amedhulumiwa kwa kuuawa kikatili kama walivyodhulumiwa akina Othman Sharif na Wazanzibari wengine wengi wakati wa/na baada ya mapinduzi. Mimi binafsi nilimjua Hanga kwa karibu sana kwa sababu kaka yake wa mama mmoja, Ali Hassan Ngwenge, alimuoa mama yangu mkubwa, Ashura bt. Haji Dau. (Mama yangu mzazi akiitwa Talha Haji Dau). Hanga hakuwa na ubavu wala ujasiri wa kumuua hata nzi, seuze binaadamu yoyote.

Hapana shaka yoyote ile kuwa, siku moja, historia itamkumbuka Hanga, Othman Sharif, Abdulaziz Twala, Mdungi Ussi, Jaha Ubwa, Khamis Masoud, Aboud Nadhif, Idrisaa Majura na wengineo, kwa jinsi na namna ambayo wanavyostahiki kukumbukwa.
Allah azilaze roho zao mahala pema Peponi - Amin.
cleardot.gif

Yaliyotokea Kifo cha Abdallah Kassim Hanga na Mohamed Said

Msiba mkubwa wa historia za viongozi wa Afrika ni kuwa wao hutaka historia ziandikwe zitakazowakweza wao na si kinyume cha hivyo. Historia ya Zanzibar haikusalimika na tatizo hili. Hadi kilipotoka kitabu cha Dr. Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," historia ya mapinduzi yaliegemezwa katika ujuzi wa mipango ya ASP na Makomredi wa Umma Party. Historia ikisema kuwa hawa ndiyo waliofanikisha mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964. Ikiwa tutachukulia hii kuwa ndiyo historia ya kweli basi Kassim Hanga hawezi kuwa kinara wa mapinduzi ya Zanzibar. Historia itamtaja Abeid Amani Karume, Abdulrahman Babu, Yusuf Himidi na wanamapinduzi wengine. Hii ni picha moja.

Ikiwa tutafunua picha nyingine kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na mikono mingi itabidi tuitafute hii mikono imetoka wapi. Hapa ndipo anapoingia Dr. Harith Ghassany na utafiti wake uliompitisha maktaba nyingi Marekani na Uingereza na mwisho kuishia katika mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi, Tanga. Hapa ndipo lilipotoka jeshi la Wamakonde waliovushwa hadi Zanzibar na kusaidia katika mapinduzi. Katika mashamba haya ya mkonge ndipo anapoingia Abdallah Kassim Hanga.

AV4856%255B1%255D.JPG
Kushoto: Abdallah Kassim Hanga, Abeid Amani Karume

Kipande hiki cha historia kwa karibu zaidi ya miaka 46 kilikuwa hakijatajwa popote si na wanamapinduzi wenyewe wala watafiti wa ndani na nje ya Tanzania. Dr. Ghassany ndiyo alikuwa mtafiti wa kwanza kuja na habari ya Jeshi la Wamakonde katika mapinduzi ya Zanzibar. Hili jeshi nani aliliunda na kwa idhini ya nani na nani walikuwa wasimamizi wa mpango ule? Ukifika hapa ndipo sasa utaiangalia historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa hii picha ya pili.

Jeshi lile lilikuwa katika ardhi ya Tanganyika huru na kiongozi wa Tanganyika anafahamika kuwa niJulius Kambarage Nyerere. Iweje nchini kwake liwepo jeshi ambalo lilivuka mikapa ya nchi yake kwenda kushiriki katika kuvamia nchi jirani. Hapa ndipo unapokutana na Abdallah Kassim Hanga naOscar Kambona. Marafiki hawa wawili ndiyo waliokuwa wapangaji wa mipango ya mapinduzi ya Zanzibar. Kambona wakati ule alikuwa na sauti kubwa katika TANU na serikali yake. Hanga naKambona hawakuwa peke yao. Vyombo vya dola vya Tanganyika viliwapa kila aina ya msaada ili mpango huu ufanikiwe.

Hapa ndipo unapokutana na Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah viongozi wa ngazi ya juu katika serikali Mkoa wa Tanga wakati wa mapinduzi. Hapa ndipo unapokutana na wahusika wengine wakuu katika mpango ule kama Victor Mkello na Mohamed Omar Mkwawa. Orodha bado ndefu. Wapo wengine katika Tanganyika katika ngazi za juu ndani ya TANU na vyombo vya usalama wote walihusika katika kufanikisha mpango wa mapinduzi na Dr. Ghassany kawataja wote kwa majina yao katika kitabu chake.

CPouovOhcYaMLt-XH13tABXsjyYGOv0Kccjn8IstvFs=w291-h207-p-no
Victor Mkello Nyumbani Kwake Nguvumali, Tanga 2003

41106_152104221469073_3582704_n.jpg
Mohamed Omari Mkwawa Akiwa Nyumbani kwa Mwandishi Barabara ya 14 Tanga

Hanga hakupata kutia mguu Sakura na Kipumbwi lakini Jimmy Ringo alifika Tanga kukagua mipango. Mkono wa Hanga ulikuwa chini ya mkono wa Kambona wakati wote wa kukamilisha mpango wa mapinduzi. Unaweza sasa ukajiuliza mkono wa nani ulikuwa juu ya mkono wa Kambona? Waarabu wana msemo: "Ukiijua sababu huondoka ajabu." Sishangai kuwa hawa wote waliotajwa na Dr. Ghassany katika kitabu chake kuwa ndiyo wapangaji wa mapinduzi leo wametolewa katika historia ya mapinduzi.

Jeshi lile lilikuwa katika ardhi ya Tanganyika huru na kiongozi wa Tanganyika anafahamika kuwa niJulius Kambarage Nyerere. Iweje nchini kwake liwepo jeshi ambalo lilivuka mikapa ya nchi yake kwenda kushiriki katika kuvamia nchi jirani. Hapa ndipo unapokutana na Abdallah Kassim Hanga naOscar Kambona. Marafiki hawa wawili ndiyo waliokuwa wapangaji wa mipango ya mapinduzi ya Zanzibar. Kambona wakati ule alikuwa na sauti kubwa katika TANU na serikali yake. Hanga na Kambona hawakuwa peke yao. Vyombo vya dola vya Tanganyika viliwapa kila aina ya msaada ili mpango huu ufanikiwe.

Hapa ndipo unapokutana na Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah viongozi wa ngazi ya juu katika serikali Mkoa wa Tanga wakati wa mapinduzi. Hapa ndipo unapokutana na wahusika wengine wakuu katika mpango ule kama Victor Mkello na Mohamed Omar Mkwawa. Orodha bado ndefu. Wapo wengine katika Tanganyika katika ngazi za juu ndani ya TANU na vyombo vya usalama wote walihusika katika kufanikisha mpango wa mapinduzi na Dr. Ghassany kawataja wote kwa majina yao katika kitabu chake.

CPouovOhcYaMLt-XH13tABXsjyYGOv0Kccjn8IstvFs=w291-h207-p-no
Victor Mkello Nyumbani Kwake Nguvumali, Tanga 2003

41106_152104221469073_3582704_n.jpg
Mohamed Omari Mkwawa Akiwa Nyumbani kwa Mwandishi Barabara ya 14 Tanga

Hanga hakupata kutia mguu Sakura na Kipumbwi lakini Jimmy Ringo alifika Tanga kukagua mipango. Mkono wa Hanga ulikuwa chini ya mkono wa Kambona wakati wote wa kukamilisha mpango wa mapinduzi. Unaweza sasa ukajiuliza mkono wa nani ulikuwa juu ya mkono wa Kambona? Waarabu wana msemo: "Ukiijua sababu huondoka ajabu." Sishangai kuwa hawa wote waliotajwa na Dr. Ghassany katika kitabu chake kuwa ndiyo wapangaji wa mapinduzi leo wametolewa katika historia ya mapinduzi.

Wanamajlis,
Mkasa wa Abdallah Kassim Hanga Sehemu ya Pili.
Katika makala haya kitu muhimu ni wasia alioacha Hanga.

Tujaalie kuwa wasia huu uwe ndiyo dira ya Wazanzibari wote katika kuleta utangamano.
Endelea kusoma...:

Raia Mwema - Yaliyotokea kifo cha Abdallah Kassim Hanga-2

HEBU tumsome Dk. Ghassany ameandika nini katika kitabu chake Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru kuhusu Hanga wakati yuko nyumbani kwa Oscar Kambona anajitayarisha kurejea Tanzania: ''Nnavokumbuka mimi, Oscar akatwambia sikilizeni bwana. Mimi nimekuiteni hapa mje mseme na ndugu yenu na mzee wenu huyu, Hanga, amekuja hapa na anataka kurudi nyumbani.

Hajataja pahala. Na mimi nimemkataza. Nimemwambia huu si wakati mzuri ni bora yeye asiende. Ama angelibaki huko huko West Africa anokotoka kwa mkewe, au abaki hapa London lakini kakataa, anataka lazima arudi. Na mie na hofu maisha yake kuwa akifika kule hatoweza kupata salama. Kwanza kuwa yeye amefikia kwangu, anajulikana yeye na mimi ni rafiki, Nyerere atajua zaidi/uzuri hayo kuwa mimi tangu tuko kule tunasikilizana mimi na ndugu huyu Abdallah. Kwa hali hiyo mimi namwambia. Na yeye Abdallah anasema hana ugomvi na Nyerere.

Sasa mimi nimekwiteni mzungumze naye, mseme naye. Akatuchukua akatupeleka kwenye chumba akasema; "Abdallah, hebu zungumza nao hawa jamaa wamekuja kukuamkia." Tukaingia sie chumbani akatuacha mimi na Ahmed [Rajab] na Abdallah. Peke yetu watu watatu. Ndivyo ninavyokumbuka mie na ndivyo anavyokumbuka Ahmed [Rajab].

VHGyYMFxfg1Fo8iDvoLJma9iM3FyVdv9NKC10z07KWSo=w415-h553-no

Ahmed Rajab Akiwa na Mwandishi Katika Ofisi Yake London
ya Jarida Africa Analysis Mwaka wa 1991

Mimi sikumbuki ile nilikwenda railway station. Kile mimi sijakumbuka. Kama ulivyosema, mimi nyumba nilikuwa naijua, sina haja ya Kasembe kunpeleka. Lakini inaweza kuwa nimekwenda mimi na Kasembe kumpokea Ahmed Rajab. Yeye Ahmed kafkiri tu na mie ni mgeni. Hajajua kuwa mimi na Kambona tunajuana na jirani, na nyumba yangu mie na yake si mbali.

Ahmed Rajab ndiye anasema, tumefika aliyefungua mlango ni Oscar Kambona, na akatuonyesha chumba. Hajaeleza nini Kambona katuambia. Lakini mimi nakumbuka Kambona katuambia kwanza, "semeni naye." Yeye kazungumza moja kwa moja, sisi tumekaribishwa tumekwenda kwa Abdallah. Yeye Ahmed amekumbuka mambo mimi sijayakumbuka. Kwa sababu, kasema tulipofika Abdallah Hanga katuambia sikilizeni: nyinyi ni vijana, watoto kwa sasa, lakini kesho nyie ndio mtakuwa viongozi. Nina maneno ninataka kukwambieni. Tukawa sasa tumekaa tunamsikiliza nini atasema.

Anasema nataka kukwambieni juu ya habari ya mapinduzi yetu ya Zanzibar. Kuna mabaya ambayo tuliyafanya na kabla sijasema lolote ninakutakeni jambo moja muhimu mlikumbuke. Msije mkakubali kufuata siasa za ukabila. Siasa za ukabila ndizo zinazotuletea matatizo na ndizo zitakazozidi kutuletea matatizo. Hilo ni jambo la mwanzo ambaye yeye Hanga katuambia.

Akasema mimi (Hanga) nilivyoondoka Zanzibar kupelekwa Dar es Salaam, kuwa Waziri wa kule, badala ya kuwa Vice-President [Makamu wa Rais] huku na Mzee Karume, alivyopelekwa bara, anasema jambo moja katika mambo aliyoyafanya ni kuwasaidia Wazanzibari waliokimbia kutoka Zanzibar wakakaa pale, wale ambao wataalamu, kuwatafutia kazi. Akataja majina. Akamtaja Maalim Salim Sanura, na akawataja wengine, mimi siwakumbuki. Kuwatafutia kazi na wakapewa kazi serikalini. Hata ikafika akaanza kusemwa, akalaumiwa, kuwa Abdalla, mbona unakwenda kinyume sasa? Hawa si ndiyo tuliowapindua, mbona wewe sasa hapa unawasaidia? Unawapokea? Akasema bwana, hapa mimi naona ni Mzanzibari tu hapa. Hawa wote ni Wazanzibari bwana. Na hawako nchi nyingine. Wako na sisi pamoja hapa. Kwa hali hiyo yeye anasema ule ndiyo uzi anataka sisi tuufate. Tusibaguane.
Jambo la pili akasema, sisi Mungu atusamehe, tumefanya mambo mengi ambayo mabaya, tumedhulumu, tumechukua watoto na wake za watu, na Mwenye Enzi Mungu ndiye anaojua. Basi mimi namuomba Mwenye Enzi Mungu anisamehe na ninajuta kwa haya niliyoyafanya. Ahmed Rajab akamuuliza suala. Akamwambia, mzee, lakini wewe na Janab [Babu] mnasikilizana vipi kisiasa? Akamwambia, mimi na Babu sote wawili ni Marxists lakini Babu si tishio kwa Karume. Mimi ndio tishio. Mimi ndio ni tishio juu ya Karume, lakini Babu is not [si tishio]. Hiyo tafauti yangu mimi na Babu, anasema. Kwa Unguja. Sasa ndio tukamuuliza, vipi ikawa wewe ndo tishio? Yeye Ahmed Rajab ndiye aliyemuuliza.

Rome ilijaribu kuingia kati katika ugomvi wa Oscar na Nyerere na ilishindwa. Kambona alinieleza. Hata makanisa yamejaribu. Ugomvi ulikuwa mkubwa na hiyo akijua yeye zaidi Kambona ndio maana akahofu Abdallah asirudi. Ile imani yake ilikuwa kubwa
kuwa Nyerere hatamdhuru. Na yeye akiona watu wangapi wamepotea lakini hajafikiria atakuja kuwa yeye.

Tukasema naye tukamwambia kweli hayo maneno anayoyasema Oscar inaonyesha ni bora usirudi kwa sasa. Akasema hapa kuna mambo mawili. Moja, kuna kutosikilizana baina ya Oscar Kambona na Nyerere, Rais Nyerere. Sasa huyu bwana akisema mimi nisirudi anazungumzia kule kutosikilizana baina yake yeye na Rais Nyerere. Sasa anahisi mie nikirudi labda kwa sababu mimi nimefikia kwake au ni rafiki yake Nyerere, anaweza akachukua hatua. Mimi nimeshafanya kazi na Nyerere na namjua vizuri mzee Nyerere, mimi na yeye hatuna ugomvi wowote. Abdallah Kassim Hanga anasema kuwa yeye na Nyerere hawana ugomvi. Na yeye ikiwa anarudi harejei Zanzibar. Atarudi anakwenda zake akakae nyumbani Dar es Salaam. La pili alisema, kuna ukweli wa kuwa mimi na Mzee Abeid Amani Karume kuwa hatusikilizani na kusema kweli si makosa yangu. Akasema Abdallah, jambo dogo sana limemfanya Mzee Abeid anichukie mimi hata ikawa mimi nikienda Zanzibar sasa siwezi kukaa nikalala Zanzibar. Lazima siku ile ile nirudi Dar es Salaam.

Na hili jambo anasema, mimi nilivyokuwa niko Tanzania Bara na Dar es Salaam ni mmoja katika mawaziri, nilikuwa ninakwenda Zanzibar mara kwa mara. Na nikienda nikifia katika nyumba iliyoko Migombani ambayo niliwahi kukaa nilivyokuwa Makamu wa Rais. Wakati mmoja nafikiri baada ya mapinduzi, President wa Zanzibar alikuwa ni Karume na Makamu alikuwa Hanga. Sasa ile nyumba ya Migombani ikawa yeye bado Hanga hajairejesha serikalini kila akienda Zanzibar anafikia pale. Siku katika siku alizokuweko pale anasema yeye kaja kafikia nyumbani pale Migombani na kila akienda watu wakipata habari kuwa Abdallah kaja, watu, jamaa, ndugu na marafiki, walikuwa wanakwenda kumuona na kuzungumza naye, na wengineo wanakuwa nayo mahitaji yao wanakwenda kumuomba awasaidie. Sasa siku moja hiyo Mzee Karume anatokea njia ya uwanja wa ndege kwenda zake mjini akapita pale Migombani akaona magari, akauliza. Kuna nini hapa, mbona magari mengi? Akaambiwa basi lazima Mzee Abdalla Kassim Hanga kaja. "Ala, sasa yeye kila akija lazima iwe namna hii?" Akaambiwa, yeye akija watu wanakuja hapa kumuamkia na kuonana naye. Basi jambo hilo anavyosema Abdalla Kassim Hanga ndilo liloanzisha ugomvi baina yake na Mzee Karume. Karume akawa hataki tena na ikawa na yeye Abdallah akienda Zanzibar hafikii tena katika nyumba ile. Akakataa kabisa.

Lakini inasikitisha kuwa tangu wakati ule yeye yupo pale London habari zishafika Cairo. Walioko Cairo ma-ambassador wa pale wameshapeleka habari Tanzania kwa Mzee Nyerere. Ikawa serikali ninavyosikia wamekaa wakimngojea arejee tu. Yeye Hanga hajajua, wala sisi hatujajua.''

Ukimsoma Dk. Ghassany anavyoeleza jinsi Hanga alivyoonywa asirejee Tanzania na yeye akakaidi unaweza kusema kuwa kifo kilikuwa kinamwita. Hebu sikiliza na kisa hiki kilichotokea Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam siku Hanga alipotua kutoka London kwa Egypt Air. Mpashaji habari wangu anasema:

''Wakati ule mimi nilikuwa meneja wa shirika moja la ndege. Nilikuwa uwanjani nikamuona Bi. Mkubwa. Huyu alikuwa mkewe Hanga, mwanamke wa Kingazija. Nikamuuliza mbona yuko pale akaniambia kuwa alikuwa amekuja kumpokea Hanga. Nilishtuka sana. Mimi ni Mzanzibari na nilijuana na Hanga kwa miaka mingi na nilikuwa nasikia mengi. Hanga alipofika nilikwenda kumlaki na tukatoka sote nje ya uwanja na hapo nikamualika yeye na mkewe chakula cha mchana hapo hapo uwanja wa ndege.

Wakati tunatoka nje ya uwanja nilimuuliza Hanga iweje karejea nchini wakati kama ule. Hanga akanijibu kuwa hapana kitu. Mimi sikuridhika. Tulipomaliza kula na tukawa tanazungumza nilitaka kwa mara nyingine niufungue moyo wangu kwa Hanga. Sikumbuki nilifanya nini lakini niliweza kumtoa mkewe pale mezani tukabaki sie wawili, mimi na Hanga. Hapo nikamwambia Hanga kuwa ni vyema kama akirejea London na ndege ile ile aliyokuja nayo.

Hanga hakunisikiliza.

Jioni mimi nikamtafuta Ali Nabwa wakati ule anafanya kazi Tanganyika Standard. Nikampa habari kuwa Hanga yuko mjini. Tulimtafuta mji mzima mwisho tukampata Oyster Bay kumbe kafikia kwenye nyumba ya Kambona. Tukaja hadi Magomeni kwa Maalim Matar tukafanya dua.

Ali Nabwa kumbe alikuwa amewaambia Tanganyika Standard wasubiri habari muhimu wachelewe kidogo kuchapa gazeti. Siku ya pili Tanganyika Standard ikachapa habari ukurasa wa mbele kuwa Hanga amerejea nchini. Haikuchukua siku Hanga akakamatwa."

5456767778_1bc5ba67f8_o.jpg

Ali Nabwa

IMG-20140520-WA0001.jpg

Maalim Mohamed Matar

Khabari nzito hizi.

Maalim Faiza,
Huyo mpashaji habari wangu wa uwanja wa ndege Dar es Salaam ndiyo
alinishangaza.

Huyu bwana ni mtu mzima.

Yeye alinisikia nikizungumza kuhusu historia ya Zanzibar katika radio na
akaweka azma ya kunitafuta.

Siku tulipokutana ndiyo akanipa kisa hicho kilichofunga makala yangu.
 
Huyu bwana na mtu mzima.

Yeye alinisikia nikizungumza kuhusu historia ya Zanzibar katika radio na
akaweka azma ya kunitafuta.

Siku tulipokutana ndiyo akanipa kisa hicho kilichofunga makala yangu.

Hakika mikasa hii Ya Mapinduzi na Nyerere yanahitaji Movie , kama ile ya Rise and Fall Of Idd Amin....hakika itakuwa ni movie itakayo zoa oscars zote...ni historia ya ukweli ilojaa ukatili
 
Crabat,
Historia ya African Association, TANU na historia nzima ya kudai uhuru wa
Tanganyika ina mashujaa wake halikadhalika ina wengine ambao ingawa
hawakuwa katikati ya jukwaa lakini walikuwa washiriki katika nafasi ile ya
utazamaji.

Siku chache zilizopita baada ya Yericko kuzungumza kuhusu nafasi ya rais
katika TAA hili lilinifanya nifikiri na ndipo yakanijia majina ya wazalendo
wengi ambao ingawa hawakuwa na nafasi ya uongozi kama uongozi hivi
leo unavyotambulikana lakini walifanya makubwa katika kuijenga TANU na
katika kupigani uhuru wa Tanganyika.

Mathalan Sheikh Hassan bin Amir au Hamza Mwapachu.

Ndipo katika bandiko langu kumjibu Yericko nikamueleza habari za Hamza
Mwapachu.

Mwapachu hakuwa na nafasi katika TAA pale Makao Makuu New Street wala
jina lake halipo katika wale waasisi 17 wa TANU lakini hayo yote kwa hakika
yasingepatikana bila ya mchango wake wa fikra kuanzia miaka ya mwishoni
1940.

Sasa watu kama Yericko wako wengi sana ambao hawaijui historia ya uhuru
na kwa hakika hatuwezi kuwalaumu watu kama hawa kwani wataijuaje historia
hii ikiwa haikuandikwa?

Tutawalaumu pale tu watakaposomeshwa historia ya kweli na wao wakafanya
ukaidi.

Turudi kwa kisa hiki cha Abdallah Kassim Hanga.

Waliokuwa karibu ya Mwalimu Nyerere wanasema kuwa baada ya kupata
taarifa za kuuliwa Hanga, Nyerere alihuzunika sana.

Inasemekana haikumptikia kabisa Nyerere kuwa Hanga atauliwa.

Bado iko nafasi kubwa sana kwa wanahistoria hasa wazalendo kutafiti na
kuandika historia ya Tanzania kama inavyostahili kuandikwa.

In Sha Allah ukipatikana wasaa na sababu nitamueleza Maalim Mohamed
Matar.

Nini kiliwafanya Hanga, Nabwa na yule mpashaji habari wangu waende kwake
kumuomba amombee Mungu Hanga?

Baada ya kukamatwa kwa Hanga haukupita muda mrefu Maalim Matar
alikamatwa na kuwekwa kizuizini Ukonga Prison lakini kukamatwa kwake
hakukuwa na uhusiano wowote na mkasa wa Hanga.
 
Kwanza nikupongeze kwakuwa mmoja ya waswahili wanaopigania uswahili wao uheshimiwe,

Japo ni mzee wa ngano lakini hilo halikuondolei heshima ya kupewa hongera na mimi msomi wa nera za ubwa
 
Mohamed Said, Naomba sasa utufunulie ni nini kiliwafanya Nabwa na Mpashaji wa uwanja wa ndege kwenda kwa Maalim Matar kumuombea dua!!
Jazaakallah!
 
Mohamed Said,
Naomba sasa utufunulie ni nini kiliwafanya Nabwa na Mpashaji wa uwanja wa ndege kwenda kwa Maalim Matar kumuombea dua!!
Jazaakallah!
MchukiaUonevu,
Kwanza,
Maalim Matar
alikuwa mtu Mcha Mungu hapa kifano chake.

Alifungwa Zanzibar na kuteswa sana na Mandera lakini siku
alipokutananae Dar es Salaam alimkaribisha kwake na kula
pamoja.

Wakati huo Karume keshafariki na Mandera na wenzake wako
hoi wanapigwa na maisha.

Hakuishia hapo tu bali katika ugonjwa wa Mandera, Maalim
Matar
akimzuru na kumsomea dua kadhaa.

Kila aliyesikia haya alihakikisha hakika Maalim Matar ni walii.

Mwenyewe akiwausia wanae waliokuwa wakimlaumu kwa hilo
kuwa lipa ubaya kwa wema.

Sasa Nabwa na Hanga waliamua kwenda nyumbani kwa Maalim
Matar
ili awanyanyulie mikono kwa Allah ipatikane nusra kwa
Hanga.

Pili.

Mke wa Hanga alikuwa na udugu na Maalim Matar ikawa ni awla
wende kwa Maalim Matar.

Taarifa kutoka Zanzibar kuhusu Hanga zilikuwa zimezagaa katika jamii
ya Kiunguja iliyokuwa Dar es Salaam ni bahati mbaya sana Hanga
alikuwa mkaidi hakutaka kuonyeka.

Kadar.

Kalamu ya Allah ilikuwa ishaandika na wino kukauka.
Hivi ndivyo Hanga alivyopotea.
 
Maalim Faiza,
Huyo mpashaji habari wangu wa uwanja wa ndege Dar es Salaam ndiyo
alinishangaza.

Huyu bwana ni mtu mzima.

Yeye alinisikia nikizungumza kuhusu historia ya Zanzibar katika radio na
akaweka azma ya kunitafuta.

Siku tulipokutana ndiyo akanipa kisa hicho kilichofunga makala yangu.

Nnamkumbuka mzee mmoja wa Kiunguja kwa sasa marehemu, Mohamed Shafi, nikikutana nae sana London akija mara kwa mara kutokea Dar kwa biashara zake baada ya kustaafu BOAC hapo Dar. Sijapatapo kumsikia akiongelea siasa hata mara moja ila nnajuwa kuwa yeye ni katika wangazija waliofukuzwa / kimbia siasa za ubaguzi za Abeid Aman Karume na kuhamishia makazi yao Dar.

Jee, inaweza kuwa mpashaji wako ni huyo?
 
Huyo ni Ahmed Saleh Yahya na yu hai.
Allah amjaalie umri tawil.

Kumsikia kuongea siasa kwake ni tabu lakini mimi akinipa
kazi nyingi za uandishi katika Africa Events kuandika siasa
za Tanzania.

Liangalie gazeti lilivyokuwa.

Hili liliandika habari kubwa sana katika siasa za CCM na
khasa Zanzibar bila kuweka ''byline.''

Sababu zinaeleweka.
Kama upo London unaweza kupata nakala maktaba ya SOAS.

blt-yTZ_QGsAXw84fV3_iBgU3k4LXGVZHvLVjaD8OcErmo9ca_Lb6RT81bmLP501mBvtUw=w442-h567-no

Africa Events Vol. 3 No. 11 November 1987

20160417_181118.jpg

VHGyYMFxfg1Fo8iDvoLJma9iM3FyVdv9NKC10z07KWSo=w415-h553-no

Mwandishi na Ahmed Rajab London 1991
 
Alama

Sipo London kwa sasa.

Nipo Shungubweni Mkuranga, huku Alama kuna Masjid kubwa sana na nzuri sana ambayo Al Habib Ramadhan Dau alitusimamia kuipata, AlhamduliLlah.

Tunauita msikiti wa Dau. Ajeeb.

Shukran.
 
Maalim,
Huku watu wanakasikrika daraja kuitwa Daraja la Dau.
Huko jina la Dau linapewa nyumba ya Allah!

Subhanallah!
 
Mohamed Said,
Tunanufaika sana na elimu hii adhimu unayoitoa hapa jamvini, Mola akutie nguvu ili historia hii iliyofichika iwafikie waTanzania walio wengi.

Kwa sisi tulioijua Dar es salaam miaka ya tisini, ukiunganisha na historia ya wapigania Uhuru Tanganyika na Zanzibar, hakika kuna mengi ya kujifunza.
Historia ya Kassim Hanga unavyoisimulia na mwisho wake alivyotwaliwa roho yake, kila nikisoma nalengwalengwa na machozi.

Lakini ipo siku kila aliyedhulumu nafsi ya mtu mwingine hatanyanyua unyayo wake mahali hapo mpaka ajibu swali hili, mbele ya Hakimu muadilifu.
 
Uwa nasikia kuwa kilicho fanya Nyerere amkamate Hanga ilichangiwa na Hanga mwenyewe kuweka urafiki na Kambona ambaye kwa mida huo Nyerere alimuona ni kama mhaini

Je hilo lina weza kuwa kweli ndugu Mohamed Said!!?
 
Ahsante sana mzee wangu mohamed said...kwa kutupasha habari nzito hizi Mungu akujalie umri mrefu ...historia ya kuuawa hanga inanihuzunisha..sana apa nafuta machozi hayakauki
 
Escotter,
Watu wengi hunipa mimi pongezi kwa kisa cha Hanga.

Ukweli wa mambo ni kuwa kisa kizima cha kifo cha Abdallah
Kassim Hanga kimeandikwa kwa kirefu katika kitabu maarufu
cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Ninayoeleza mimi ni yale niliyoyasoma kutoka katika kitabu hicho.
 
Back
Top Bottom