Kutoka kuwa Kabila dogo la Kayi mpaka kuwa Ottoman Empire na kutawala Dunia

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Huu Uzi Una kilomita nyingi lakini ni Mgodi unaotembea,kazi kwako ukutane nao au upishane nao!

Dola ya Uthmaniya ndio Dola kubwa kabisa na iliyodumu Kwa Mda mrefu zaidi Kati ya Dola zilizo asisiwa na Waturuki. Walianzisha Dola kama ukamilishaji WA Dola za Bani Abbasi,Bani Umayya na Walseljuq. Waligeuka kutoka kabila dogo na kuwa Kati ya wawakilishi WA ustaarabu wa Waislamu. Ilitawala Asia,Ulaya na Afrika na kuwa Dola kuu ya mwisho ya Uislamu.

Dola ya Uthmaniya iliasisiwa Anatolia (Uturuki) na kabila la Kayi ambalo ni Tawi la Waturuki WA Oghuz katikati ya Karne ya 13, walifika Anatolia ili kukwepa shinikizo la kandamizaji wa Wawamongoli, wakaishi katika eneo la Ankara.

Ertugrul Ghazi (ertugrul bey) alikuwa kiongozi WA Kayi aliyekuja Anatolia,alipofariki dunia mwaka 1281, mwanaye Uthman Bey (Osman bey) alishika hatamu za uongozi WA kabila la Kayi ambalo liligeuka kuwa Jimbo dogo. Uthman Bey alipambana dhidi ya makabaila WA Kirumi. Kwa kupata msaada WA watawala WA majimbo ya jirani na viongozi WA Ahi. Kundi ambalo kilikuwa madhubuti katika mambo ya Dini na jamii,alitangaza Uhuru mwaka 1299.

Wakuu wote WA Dola baada ya Uthman Bey walitokana na kizazi chake,ndio maana Dola hii ikaitwa Dola ya Uthmaniya ( Ottoman Empire).

HALI YA KISIASA KIENEO

Dola ya Uthmaniya ilipoundwa ,Dola ya warumi/wabizanti (Rumi ya mashariki) ambayo makao yake yalikuwa Instanbul ilikuwa na changamoto mbali mbali na kupoteza sifa ya kuwa Dola na kubakia kuwa Jimbo Tu. Hii ilitokana na fitna katika kasri na mapigano ya kugombea madaraka na kitu cha utawala,hivyo nguvu zake za kijeshi zilisambaratika. Kulikuwa na falme za Bulgaria na Serbia na majimbo ya maldovia,walachia,bosnia-herzegovina na Albania katika eneo la Balkan.

Yote yaliendelea kupambana na kusababisha changamoto za kisiasa na kidini,Kwa ujumla hapakuwa na umoja WA kisiasa katika eneo Hilo. Katika kipindi Hicho Dola ya Walsejuq ya Anatolia kabla ya Wauthmaniya ilianguka na majimbo yakaa kufanya mambo yake Kwa Uhuru. Wauthmaniya hawakuingilia migogoro iliyo tokea katika majimbo hayo. Badala yake walifuata Sera ya kipekee ya kuelekea upande WA magharibi,eneo la Balkan Kwa lengo la kuimarisha Dola na kueneza mazuri ya Uislamu.

Uthman Bey alifariki dunia mwaka 1326. Kwa mujibu wa taratibu za Dola mwanaye Orhan Bey wakati WA Baba yake alikuwa na jukumu la kutoa maelekezo ya safari za kijeshi na kutekeleza majukumu ya Dola,alishika hatamu za Dola. Wakati WA utawala WA Orhan Bey (1324-1362) Dola iliasisiwa Kwa mifumo ya serikali kuu na jeshi.

Bursa ilivyokuwa Chini ya Warumi ilifunguliwa na kuwa makao makuu ya Dola. Kisha miji ya Iznik,Izmit na Balikesir ilifunguliwa. Moja ya matukio makubwa ya utawala WA Orhan Bey ni kwamba Dola ilifika maeneo ya Balkan na udhibiti WA Waturuki ilianzia huko. Orhan Bey alimtuma mwanaye Suleyman Pasha kwenda Canakkale,hivyo Ngome moja ilipatikana na kisha harakati za ufunguzi WA Thrace na Balkan zikaanza.

Baada ya hapo Sera ya makazi ilianza na kuwachukua Waturuki WA Anatolia na kuwaleta pale na kuanzisha makazi na kuachana na utaratibu WA kuhama Hama na hivyo watu wakawa katika makazi na hata ukusanyaji WA Kodi ukawa rahisi zaidi.
Wauthmaniya walichukua urithi WA Dola ya Walsejuq ya Anatolia Kwa lengo la kulinda na kueneza Uislamu kama walivyofanya wao. Dola ya Uthmaniya ilipiga hatua kubwa na kuwa Dola moja ya madola ya yaliyo dumu Mda mrefu duniani,ikapanua Sana mipaka yake katika mawanda ya kiutamaduni na ustaarabu. Ilipofika Karne ya 15 na 16 ilifikia hatua ya kuwa Dola yenye nguvu zaidi duniani.

SABABU KUBWA ZA MAFANIKIO YA DOLA YA UTHMANIYA
1. Eneo kijiografia : tangu ikiwa Jimbo haikuvuta umakimi WA majimbo mengine,pamoja na hivyo ilikuwa kwenye njia za biashara na usafirishaji WA biashara.

2. Ilikuwa kwenye mpaka WA Dola dhaifu ya Warumi

3. Eneo hili kilikuwa linafaa Kwa kilimo na ufugaji.

4. Muundo WA Anatolia uligawanyika kisiasa na mafanikio ya Sera ya Wauthmaniya kutumia hali hiyo Kwa faida.

5. Hali ya eneo la Balkan (hawakuweza kupambana na Wauthmaniya kwasababu nguvu zao za kisiasa katika ukanda huo zilikuwa zimedhoofika na kutawanyika).

6. Waliungwa mkono na jumuiya za Ahi ambazo yalikuwa makundi yenye nafasi nzur kisiasa,kidini,kiuchumi na kijamii katika Anatolia.

7. Vita vitukufu vilivyoandaliwa na Wauthmaniya vilikubaliwa kikamilifu na umma WA Anatolia na viongozi.

8. Watu wakubwa WA Turcoman na makamanda waliwaunga mkono Wauthmaniya.

9. Waliutekeleza Kwa mafanikio mfumo WA serikali kuu na uelewa wao WA uadilifu.

10. Walitekeleza kikamilifu Sera Yao ya iskan (makazi).

WOSIA WA SHEIKH EDIBALI KWA UTHMAN GHAZI

Mwanangu?

Wewe ni kiongozi! Kuanzia sasa hasira itatoka kwetu,huruma itatoka kwako! Hisia ya kukosewa itatoka kwetu, tulizo la nafsi litatoka kwako...kulaumu ni kazi yetu,kuvumilia ni kazi yako...Udhaifu na aibu zitatoka kwetu,subira ni kazi yako...migogoro mapigano na mabishano yatatoka kwetu,kutenda haki ni kazi yako....jicho Baya,kutabiri mabaya na tafsiri zisizo kuwa na haki zitatoka kwetu ,msamaha itatoka kwako.

Mwanangu!

Kuanzia sasa kugawanyika ni kazi yetu,kuunganisha ni kazi yako...uvivu ni kazi yetu,kuonya ,kuhamasisha na kuweka mipango ni kazi yako.

Mwanangu!

Wewe ni mzungumzaji imara,mwenye Busara nzuri,lakini kama hujui namna na mahalo pa kuvitumia, utasombwa na upepo WA Kwanza wa asubuhi na nafsi yako. Ndiyo maana daima unatakiwa kuwa mvumilivu,imara na mwenye azma.

Subira ni muhimu Sana,kiongozi anapaswa kuwa na Subira. UA halichanui kabla ya wakati, tunda bichi haliwezi kuliwa, hata kama likiliwa, litakwama kooni mwako. Upanga Bila elimu ni kama tunda bichi.

Mwanangu!
Kuna watu wanao zaliwa alfajir na kufariki wakati WA swala ya jioni
Waheshimu Baba na mama yako! Tambua kwamba baraka zipo pamoja na wazee. Ukipoteza Imani yako hapa duniani,utageuka kuwa jangwa hata kama ukiwa kijana mbichi.

Kuwa mwaminifu! Usilichukulie kila neno Kwa mtazamo binafsi! Unapo shuhudia Jambo usilitangaze,unapojua Jambo usiliseme! Usisimame mara Kwa mara sehemu ambayo unapendwa; vinginevyo upendo na heshima yako vitaumizwa.

Wahuzunikie watu watatu: msomi anayeishi baina ya Wajinga,tajiri aliyefukarika na mheshimiwa anaye poteza heshima ya watu.

Usisahau kuwa wale walio juu hawako salama kama wale walio Chini.

Usiogope kupigania Jambo madamu upo sahihi! Unapaswa kujua kuwa farasi mzuri huitwa bay.shujaa WA mashujaa huitwa deli ( shujaa na jasiri)

Mwanangu!

Yafanye maarifa na elimu ya umma viishi ndani mwako. Usiyageuzie mgongo maarifa na elimu.
Daima sikia uwepo wake. Elimu na maarifa haya ndicho kitu kinachomlinda kiongozi na umma.

KIPINDI CHA MAENDELEO (1360-1453)
Kipindi kunachoanzia wakati WA kifo cha Orhan Bey mpaka kufunguliwa Kwa Instanbul ni kipindi cha MAENDELEO cha Dola ya Uthmaniya,muundo WA Dola uliundwa kikamilifu wakati ikiendelea kujitanua katika maeneo ya Balkan .Viongozi muhimu kipindi hiki ni Murat I,Bayezid,Mehmet na Murat III.

Mafanikio ya haraka katika maeneo ya Balkan yalizifanya nchi za Balkan kuwa na wasiwasi. Kwa uchochezi WA Papa,jeshi la wanamsalaba liliundwa Chini ya uongozi wa Wafalme WA Bulgaria, Hungary na Serbia. Kwakuwa walijiamini Kwa ukubwa WA jeshi Lao hawakuchukua tahadhar za lazima, Kwa kutumia fursa hiyo jeshi la Wauthmaniya Chini ya uongozi wa Haji Ilbey liliwashinda Wanamsalaba Kwa shambulizi moja la usiku. Na hii ilikuwa Vita ya Kwanza ya Wauthmaniya dhidi ya Wanamsalaba.

VITA VYA KWANZA VYA KOSOVO
Nchi za balkan zilijikusanya tena baada ya kuona kuwa Wauthmaniya wameikamata miji kama vile Sofia,Nia na Manastir na kuimarisha udhibiti wao maeneo ya Balkan. Watu WA Hungary,Croatia na Wallachia walijiunga pia katika muungano WA Wanamsalaba ambao uliundwa Chini ya uongozi wa Waserbia. Wauthmaniya Chini ya kiongozi Murat I walishinda Vita,ingawa walishinda lakini Murat I aliuwawa na Askari mmoja wa Serbia anaitwa Milos.

Jeshi sasa na uongozi ulikuwa Chini ya Bayezid I, Wauthmaniya walipanua mipaka katika eneo la Balkan mpaka kwenye lingo za mto Danube,Jambo ambalo liliwaogopesha wahangary. Kwa kutoweza kupambana na Wauthmaniya Peke yake Mfalme WA Hungary Sigismund aliyaita mataifa ya Ulaya kwenye muungano WA kikristo Kwa msaada WA Papa. Hapo jeshi imara likaundwa Kwa kushirikisha nchi kama vile Hungary,Venice,Ujerumani,Ufaransa,Uingereza,Ubelgiji,Switzerland,Uholanzi,Scotland na Wallachia
Wanamsalaba hao walizingira ngome ya Nicopolis kwenye kingo za mto Danube. Wanamsalaba pia walishindwa katika Vita hiyo.

Baada ya kushindwa katika Vita hiyo Wanamsalaba hawakuweza kujiandaa na kuweza kupambana na Wauthmaniya Kwa kipindi cha takribani miaka 50.

Jeshi la wanamsalaba likiongozwa na Wladyslaw III wa Poland lilijikusanya Kwa lengo la kuwaondoa Wauthmaniya katika eneo la Balkan,lakini jeshi la Wauthmaniya Chini ya Sultan Murad II liliwashinda Wanamsalaba hao katika pwani ya Varna. Na Mfalme wao aliuwawa.

KIPINDI CHA UKUAJI (1453-1579)
Masultan WA kipindi cha ukuaji,Mehmed II, Beyazid II,Selim I na Sultan Suleyman I

Matukio Makubwa katika Kipindi cha Ukuaji

1. Ufunguzi WA Istanbul (1453) : Sultan Mehmed II alipoingia madarakani lengo lake ni kutengeneza Dola kuu inayotawala ulimwengu mzima. Jambo la Kwanza ilikuwa ni kuifungua Istanbul na hii ni kwasababu Warumi walikuwa wanaleta Sana chokochoko enelo la Anatolia.

Pili,Istanbul ilikuwa kituo muhimu cha utamaduni na ilikuwa kwenye njia za biashara za nchi kavu na baharini,iliufanya mji huu kuwa eneo muhimu Sana kijiografia.

Aidha Istanbul lilikuwa eneo muhimu kidini. Kila kamanda WA Kiislamu alitamani kuwa mfunguaji WA mji huo aliyesifiwa katika hadith ya Mtukufu WA daraja Mtume Muhammad (s.a.w) aliposema "Hakika Constantinople itafunguliwa. Kamanda aliyebarikiwa ni Yule atakaye ifungua na jeshi lililo barikiwa ni jeshi litakalo ifungua." Ndio maana mji huu ulizingirwa mara nyingi na majaribio mengi ya kuifungua yalifanywa na Waislamu. Kama zama za Bani Abbasi na Bani Umayya ulizingirwa mara nane. Na Zama za Wauthmaniya ulizingirwa mara tatu na haukufunguliwa.

Sultan Mehmed II alipokuwa anafanya maandalizi ya kuifungua Istanbul Warumi waliongeza hatua za ulinzi na kukarabati ukuta WA ngome Yao uliokuwa imeharibika na kuomba msaada WA ulimwengu WA kikristo na kujaribu kuunganisha makanisa ya kikatoliki na kiorthodox na halfa kubwa ilifanyika ndani ya Hagia Sophia Kwa AJILI ya lengo Hilo. Hata hivyo Waorthodox WA Rumi walipinga Hilo. Maneno ya mwinyimkuu WA Wabizanti Loukas Notaras: " Ninapendelea kukiona kilemba cha Wauthmaniya mjini Constantinople kuliko kofia ya Kadinali". Inaonyesha kuwa juhudi za kuwaunganisha madhehebu zilishindikana na watu WA Istanbul waliutamatani uadilifu WA Wauthmaniya.

Baada ya maandalizi,Sultan Mehmed II alituma ujumbe Kwa Mfalme kuwa ajisalimishe lakini mwamba alikataa,unajua mwamba alikataa kwakuwa alikuwa amezungukwa na ngome kubwa Sana hivyo akajiamini kuwa yupo salama,kumbe Sultana alikuwa na mizinga ya kurusha,zaidi ya majahazi sabini (70) yalikokotwa ndani ya usiku mmoja na kuwekwa karibu na pembe ya dhahabu.

Kama haitoshi Sultan Mehmed alimtaka tena Mfalme ajisalimishe lakini mwamba akakataa tena ndipo hapo mashambulizi yalianza na kufanikiwa kuifungua Istanbul mnamo mei 29,1453. Baada ya ufunguzi sultan huyo kijana aliingia na msafara katika kanisa la Hagia Sophia ambalo kilikuwa sehemu muhimu katika historia ya Warumi na Ukristo. Na aliwaambia maelfu ya wakristo waliokuwa wamekusanyika katika eneo Hilo, Aliwaambia kwamba Uhuru wao kimadhehebu na kidini utalindwa,Mali zao hazita chukuliwa na wale walio kimbia wanaruhusiwa kurudi. Mashallah huo ndio Uislamu,siku zote hata tangu enzi za Mtume watu wasio waislamu walipewa haki zao na kuthaminiwa,ni tofauti kabisa na jinsi watu wanavyo uchafua Uislamu na kuupaka matope.

Matokeo ya ufunguzi WA Istanbul ulikuwa na matokeo makubwa na historia ya Wauthmaniya na storia ya dunia. Dola ya warumi ilianguka na tukio hili lilipokewa katika ulimwengu WA kiislamu Kwa furaha kubwa Sana. Istanbul ikaanza kuwa kitovu cha elimu na ustaarabu. Wanazuoni wengi kutoka mashariki na magharibi wakaja Istanbul na kuzalisha kazi mbali mbali Chini ya hifadhi ya Sultan Mehmed II ,ambapo kazi zao ziliuangaza ulimwengu wote.

Kuanguka Kwa Dola ya Warumi kulisababisha huzuni kubwa Sana Ulaya, kwasababu ulisababisha pia kuanguka Kwa matumaini ya ulimwengu WA Kikristo ya kuifikia Jerusalem Kwa nguvu ya Warumi. Walikuwa wamepoteza ngome muhimu Sana, utaalamu WA mizinga iliyotengenezwa na Sultan Mehmed II Kwa AJILI ya kuizingira Istanbul ulithibitisha kuwa kuta za mji huo hazikuwa kizuizi kisichopitika.

2. Matukio katika Maeneo ya Balkan
Ufunguzi WA Istanbul huko Ulaya ulipokelewa Kwa hisia tofauti,jamii za Wabalkan zilifurahishwa na Sera za kuvumiliana za Waturuki. Hata hivyo Papa,Wafalme na viongozi WA kikabaila walikuwa na mtazamo tofauti
Hawakuachana na tamaa Yao kuwaondoa Waturuki maeneo ya Balkan,ufunguzi mpya WA Istanbul uliwasha upya tamaa hiyo. Papa aliyatolea wito mataifa ya Ulaya kujikusanya tena na kubeba harakati za bendera ya Msalaba.

Sultan Mehmed II ambaye alikuwa anafuatilia hayo matukio hayo Kwa ukaribu alichukua hatua Bila kuwapa nafasi ya kujikusanya. Aliharibu mipango Yao Kwa kuimata Serbia mwaka 1459,Morea mwaka 1460,Moldavia na Wallachia mwaka 1476. Mamlaka ya Wauthmaniya katika eneo la Balkan yalifika mpaka bahari ya Adriatic.

Wabosnia walikuwa wamechoshwa na shinikizo la Wakatoliki na wakasikia kuhusu heshima kubwa ya Wauthmaniya kwenye Uhuru WA Dini,walisalimu amri Bila kuonyesha upinzani wowote. Upendo WA watu Kwa Waturuki waislamu ulikuwa mkubwa Sana kiasi kwamba wanaume wote waliokuwa na uwezo wa kutumia silaha waliungana na jeshi Hilo. Baada ya Muda mfupi wabosnia waliingia katika Uislamu.

3. Matukio katika Eneo la Anatolia na Baharini

Wakati WA Wauthmaniya wakiendeleza harakati zao za ufunguzi kuelekea upande wa magharibi ili kufikisha Ujumbe WA Uislamu ndani ya Ulaya,baadhi ya Waturuki huko nyuma Anatolia walikula njama na maadui na kuwashambulia Wauthmaniya Kwa nyuma. Majimbo yaliyokuwa mbele katika hujuma hiyo ni Isfendiyar,beyligi huko sinop,Karamanogullari katikati mwa Anatolia na Akkoyunlu upande wa mashariki. Safari za kijeshi zilifanywa kwenda kutuliza uhasi huo.

Baada ya Wauthmaniya kuiweka Anatolia Chini ya uthibiti wao,harakati za kijeshi baharini zilifanyika ili kuhahakisha usalama kwenye milango ya bahari ya Bosporus na Dardanelles na Pwani zake. Visiwa vingi katika bahari ya Aegea vilikamatwa na hivyo tahadhari zikachukuliwa dhidi ya hatar ambazo zingetokea baharini.

4. Safari za Misri na Ukhalifa WA Wauthmaniya
Ukhalifa ambao ulianza na Abu Bakar (r.a) baada ya kifo cha mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w) na ilikuwa na umuhimu mkubwa kidini na kisiasa Kwa ulimwengu WA kiislamu ulikuwa mikononi mwa Mamaliki WA Kituruki ambao walikuwa wameanzisha Dola huko Misri. Mamaliki (mamluk) walitawala eneo ambalo Leo linajumuisha Misri na Syria. Miji Mitukufu ya Makka na Madina ilikuwa Chini ya mamlaka Yao. Kutokana na Miji hiyo kuwa Chini Yao walikuwa na kauli katika ulimwengu WA kiislamu. Sio Tu kwamba walikuwa wakiingilia mambo ya ndani ya Dola ya Wauthmaniya,Bali pia walikuwa wakishirikiana na Mashia dhidi ya Dola ya Wauthmaniya . Kwa kuifungua Misri njia ya kiunganishi ingewekwa Chini ya udhibiti na Kwa namna hii madhara ambayo mabaria WA Kireno walikuwa wakiyatoa Kwa Waislamu katika Bahari ya Hindi yangezuiliwa.

Sultan Selim I alikuwa na fikra kwamba nguvu ya kisiasa katika ulimwengu WA kiislamu inatakiwa kuunganishwa na kuwekwa Chini ya mkono mmoja. Baada ya kuitokomeza hatar ya Washia, Sultan Selim aliamua kwenda Kwa Mamluk. Kwanza alitaka kujua mtazamo WA wanazuoni namna ya kuamiliana na mtawala WA Mamluk ambaye pia alikuwa muislamu. Wanazuoni walisema ilikuwa halali kwenda kwenye safari ya kijeshi. Na Safar hiyo ilifanywa baada ya kupata idhini hii.

Kwanza Mamluk walishindwa walishindwa katika ilivyotokea katika eneo la wazi la Marji Dabiq lililopo karibu na Aleppo. Syria, Lebanon na Palestina ziliunganishwa katika kwenye Dola ya Wauthmaniya na hivyo njia ya kwenda Misri ikawa wazi. Sultan Selim alituma ujumbe kwenda Kwa mtawala WA Mamluk ,Tuman Bey II na kumtaka ayatambue mamlaka yake. Tuman Bey II sio Tu kwamba alikataa kutambua mamlaka yake Bali alimuua mjumbe aliyetumwa. Daah huyu mwamba Noma,Kwa kawaida Mjumbe hauwawi Ila yeye akaamua kumuua! Vita vilipiganwa na Tuman bey alikamatwa mateka na kuuwawa.

Sharifu WA Makka alikabidhi funguo za Makka na Madina Kwa Sultan Selem I. Kwa namna hii alipata cheo cha Khadim al- Haramain (mtumishi WA haram mbili). Ushindi huu ulizaa baadhi ya matukio muhimu kama ifuatavyo.
  • Ukhalifa uliamia Kwa Wauthmaniya
  • Dola ya Mamluk ilifikia kikomo na mamlaka ya Miji miwili Mitukufu ya Makka na Madina iliwekwa Chini ya mamlaka ya Wauthmaniya.
  • Njia ya kiungo ambayo ilianzia bandari za bahari ya Hindi mpaka Meditereniani kupitia nchi kavu na baharini iliwekwa Chini ya udhibiti ya Wauthmaniya .
  • Dola ya Wauthmaniya ulifanikiwa kuwa Dola kubwa kabisa yenye nguvu katika ulimwengu WA kiislamu.
  • Amana tukufu zililetwa Istanbul na kuwekwa katika Kasri la Topkapi. Amana hizo ,ambazo ni vitu vya kale,bado vimehifadhiwa katika Kasri mpaka Leo.

5. Matukio Mbali Mbali wakati WA Sultan Suleyman I

Alifanya Dola ya Wauthmaniya kuwa Dola yenye nguvu barani Ulaya na katika ulimwengu WA kiislamu na kumwachia mwanaye hazina iliyojaa. Kipindi ambacho Dola ya Wauthmaniya ilikuwa na nguvu katika mawanda ya kisiasa na kijeshi Kwa mashariki na magharibi. Watu WA Ulaya walimwita Sultan Mkuu (sultan Al adhim) na Waturuki wakamuita Qanuni (muweka sheria).

Dola ya Warumi Ujerumani ambayo ilidhibiti sehemu kubwa ya Ulaya na Mfalme wake Charles V . Hungary ambayo ilikuwa ikiungwa mkono na Mfalme huyu ilikuwa ikipanga kufanya Vita vya Msalaba dhidi ya Wauthmaniya . Baada ya mjumbe WA Qanuni kuuwawa aliyetumwa na Wauthmaniya ,kufuatia tukio hili Sultan alituma jeshi na kuikamata Belgrade (1521). Wakati huo huo Mfalme WA Ufaransa alichukuliwa mateka na Mfalme WA Hungary, ikabidi mama yake aombe msaada Kwa Sultan Suleyman I amkomboe mwanae na mwamba alifanya hivyo.

Kuanzia wakati uhusiano na wafaransa uliimarika na Kwa ombi la Mfalme Francis I makubaliano yalifanywa ya kuitenga Ufaransa na muungano WA Wanamsalaba,mkataba huo WA kusalimu amri Kwa Ufaransa Chini ya Wauthmaniya uliitwa ahitname na wafaransa waliuita "kusalimu amri" ulisainiwa Kati ya mataifa hayo mawili.

Huko baharini nako Wauthmaniya walikamata mawanda ya huko na mapambano makubwa yalifanyika bahari ya Hindi na Meditereniani dhidi ya mataifa ya Ulaya. Sultan aliweka umakini katika jeshi la wanamaji. Na maeneo yote hayo yalidhibitiwa vizuri Sana.

WAUTHMANIYA BARANI AFRIKA
Baada ya ufunguzi WA Misri 1517,udhibiti WA Wauthmaniya ulianza barani Afrika,nchi hii muhimu ambayo ndio ilikuwa ya Kwanza kuweka Chini ya mamlaka ya Wauthmaniya iliendelea kuwa Chini ya Dola ya Wauthmaniya barani Afrika mpaka mwaka 1882 baada ya Waingereza kuivamial Misri.

Ufunguzi WA Algeria (1533) . Baada ya Wahispania kuidhibit Algeria kutoka Kwa waislamu (1510) walimwaga damu nyingi katika eneo Hilo na katika Bahari ya Meditereniani Kwa unyama wao. Ndugu wawili Oruc Reis na Hizir Reis ambao walikuwa wakishughulika katika Bahari ya Meditereniani waliirejesha Algeria mikononi mwa Wahispania.

Sultan Suleyman I alimteua Hiriz Reis kuwa kiongozi WA jeshi la wanamaji la Wauthmaniya. Kwa njia hiyo Algeria iliunganishwa katika Dola ya Wauthmaniya.

Ufunguzi WA Tripoli : mwaka 1552 baharia WA Kituruki Turgut Reis (dragut) aliichukua Tripoli kutoka wapanda farasi WA wakikristo kutoka Malta. Mwaka 1911 eneo Hilo lilivamiwa na Italia.Tripoli ndio kipande cha mwisho cha ardhi ambacho Wauthmaniya walikipoteza barani Afrika.

Tunisia ilikuwa Chini ya Wauthmaniya kati ya Mwaka 1573 - 1881,nchi hii ilivamiwa na kunyonywa na Wafaransa. Leo kuna misikiti 20 na madrasa 11 nchini humo zilizo achwa tokea enzi za Wauthmaniya.

Ufunguzi WA Morocco, nayo iliingizwa katik Dola ya Wauthmaniya. Mamlaka ya Wauthmaniya ilitanuka mpaka kwenye jangwa la Sahara wakati Hassan Pasha gavana WA Algeria.

Ozdemiroglu Suleyman Pasha alianzisha Hebesh Eyalet (Jimbo la uhabeshi) mwaka 1554 ambalo liliendelea kuwepo mpaka mwaka 1916. Baadhi ya nchinza Afrika Leo Kama vile Sudan, Eritrea, Djibut, Somalia, Ethiopia, Niger, Chad, Kenya na Uganda wakati Fulani katika historia zao ziliingia Chini ya utawala wenye uadilifu WA Wauthmaniya .

KIPINDI CHA MDORORO (1579-1699)
Kipindi kinachoanza wakati WA kifo cha Wazir Mkuu Sokullu Mehmet Pasha (1579) mpaka makataba WA Karlowitz (1699) kinaitwa kipindi cha MDORORO WA Wauthmaniya. Japokuwa Dola ilikuwa na nguvu lakini ilikuwa ikikabiliana na migogoro mingi ndani na nje. Usultan WA watoto wadogo,shahzade na mama zao (valide sultan) kuingilia mambo ya Dola, mawazir ambao hawakuungwa mkono na jeshi,na uasi dhidi ya Masultani vilizuia matatizo hayo kutopatiwa ufumbuzi.

Baada ya Wahispani kuingiza kiwango Kikubwa cha dhahabu na fedha huko Ulaya wakati WA misafara mipya ya kibiashara na baadhi ya dhahabu na fedha hiyo kuingizwa katika ardhi ya Wauthmaniya Kwa njia isiyokuwa ya halali ulisababisha sarafu ya kiuthmaniya kushuka thamani na kuongeza gharama za Maisha. MAENDELEO ya kiufundi ya majeshi ya Ulaya yalisababisha majeshi ya Wauthmaniya kushindwa katika Vita mbali mbali.

Wakati WA kipindi cha MDORORO Vita vya ndani vilizuka,wanakijiji walikuwa wamehelemewa na mzigo mkubwa WA Kodi,viongozi ambao hawakuwa na furaha na serikali kuu,na wahitimu WA shule ambao hawakuwa na ajira walijiunga katika uasi. Uasi ulizimwa na jeshi lakini vyanzo vya matatizo hayo havikuchunguzwa. Ndio Imani ya watu Kwa Dola ilidhoofu.

KIPINDI CHA KUSHUKA NA KUANGUKA (1699-1922)

Kwa mujibu wa wanahistoria ,Dola ya Uthmaniya iliingia katika kipindi cha kushuka baada ya kusaini mkataba WA Karlowitz na mataifa ya Ustralia,Lehistan,Venice na Urusi mwaka 1699.

Kuanza Kwa mapinduzi ya viwanda Ulaya ,vuguvugu na itikadi za utaifa zilizo ibuka baada ya mapinduzi ya Ufaransa ni mambo yaliyo athiri Dola ya Wauthmaniya . Ukuaji na ustawi WA Dola vilidumaa katika Karne ya 18.
Karne ya 18 Dola ya Wauthmaniya iliingia vitani na Urusi,Austria na Venice. Na Urusi ndio nchi iliyosababisha matatizo makubwa Sana Kwa Wauthmaniya kuliko nchi nyingine.

Dola ya Urusi iliwachochea watu WA Serbia na Ugiriki kujitenga na Dola ya Wauthmaniya. Iliwapatia kila Aina ya msaada.

Kwakutumi haki za Wakristo WA kiorthodox,mara Kwa mara iliingia mambo ya ndani ya Dola ya Wauthmaniya .
Ilifuta Sera ya uvamizi kupitia eneo la Balkan Kwa kuyaweka mataifa huko Chini ya udhibiti wake.

Iliwachochea Waarmenia dhidi ya Dola Wauthmaniya. Ilisababisha kuibuka Kwa "swala la Waarmenia" ambapo Waarmenia walikuwa wakiishi vizur na waislamu Kwa Karne nyingi.Suala la Armenia ambayo liliibuka baada ya uchochezi WA Urusi na mataifa mengine halikuweza kutatuliwa.

Lakini hata mataifa ya Ulaya hayakupenda Dola ya Wauthmaniya iwe Chini ya Urusi hivyo waliungana kupambana na Urusi,hapa tunaona kwamba Urusi toka zamani ilikuwa na ubabe Sana na haikupendwa na mataifa mengine kama ambavyo tunaona Leo America na washirika wake wameunga nguvu kupambana na Urusi dhidi ya Ukraine,daah kumbe Putin hafanyi mambo mapya Bali anaendeleza mambo ya wazee wake.

Kwa kumalizia ni kwamba ilitokea baadae fitina kubwa kutoka katika mataifa ya Ulaya dhidi ya Dola ya Wauthmaniya,kumbuka Dola hii ndio ilikuwa kimbilio la wakimbizi wengi wa kiasia katika mataifa mbali mbali,hivyo baadae mataifa ya Ulaya yakaanzisha fitina Kwa kuwachochea waislamu na wasio kuwa waislamu kuanza uasi dhidi ya Dola hii,hata wale ambao walikirimiwa na kuhifadhiwa kama wakimbizi nao walianza chokochoko ili mradi fitina ilikuwa kubwa Sana dhidi ya Dola ya Wauthmaniya.

Huku Afrika nako mataifa ya Ulaya yakaanza kuvamia ngome za Wauthmaniya na kuchukua au kugawana maeneo ambayo yalikuwa Chini ya Dola ya wauthmaniya. Kwahiyo kifupi mambo yalikuwa mengi Kwa Dola kuweza kupambana nayo.

Mambo ni mengi na Mda ni mchache,kwani kuna matukio mengi ilibidi nisiyaweke hapa kutokana na kukosa Mda WA kuandika na vile vile kuogopea Uzi usizidi kuwa na kilomita nyingi Sana.

Mpaka wakati mwingine.

Ni hayo Tu!
 
Hakunaga dola ya haki. Hao unasema walikuwa na uhuru wa kidini lakini walipora huo msikiti wa Hagia Sofia na hadi leo ni msikiti. Mara tu walipoangusha utawala wa byzantine wakabadili kanisa hilo kuwa msikiti. Wameua mamilioni ya waarmenia. Nk nk. Hakunaga empire nzuri. Hao waturuki walikimbizwa na wamongoli kutoka central Asia. Wakakaribishwa na Wakurd na Waarmenia hapo mashariki ya kati. Baadaye kwa kuwa ni watu wa vita, wakaanza kuwatawala wenyeji na kuwachinja hadi leo.
 
Kila empire ilikuwa na Athari Fulani katika jamii husika,hata hao Warumi nao utakuta walikuwa na Athari zao

Lakini

Wauthmaniya walikuwa na ustaarabu uliotukuka kiasi kwamba hata wasio waislamu walipendezwa na Utawala wao.

Kumbuka Waorthodox walikuwa tayar kutawaliwa na Sultan na kuona kilemba chake kuliko kuona kofia ya Kadinali,inamaana wakristo wenzao walikuwa sio ndio maana walikuwa radhi kuwa Chini ya Ottoman empire
 
Shetani mdogo(Lesser evil) lakini bado shetani.
 
Kilindia Ottoman Inaingia Ilikuwa Misri ikiwa na Watu wa Jamii gani ?
Algeria Jamii gani ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom