TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Wabunge Wote 394
Wabunge waliopiga kura 369
Akidi ya wabunge wanaotakiwa 184
Wabunge Waliopo na kupiga kura 351
Kura Zilizoharibika 0
Magdalena Sakaya 101(28%)
Dr Tulia 250(71.2%)
Kinachoendelea kwa sasa na wagombea wanaogombea nafasi ya unaibu spika wanaomba kura na kwa sasa ni Magdalena Sakaya kupitia CUF, amesema ana uzoefu wa uongozi kwa miaka 20, kati ya hio miaka 10 ndani ya bunge. Sakaya akijibu swali la Kairuki kuhusu kufanya kazi na spika asie wa chama chake. Amesema kila mbunge anafanya kazi kwa ajili ya watanzania kuhakikisha matarajio ya watanzania yanafikiwa bila kuangalia chama.
Gekul: Umekuwa mbunge kwa awamu tatu, mawazo katika bunge hili hayatekelezwi na serikali, utatumiaje uzoefu wako kuunganisha bunge na serikali.
Sakaya: Tunatambua na awamu mpya ya awamu ya tano, tuna sura mpya za wabunge wengu, spika na tutakuwa na sura mpya ya naibu spika. Naamini sote tukiwa imara tunaenda kuyafikia matarajio ya wananchi.
Anaefata sasa ni Tulia Ackson kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
Tulia: Kwa taaluma mimi ni mwanasheria na nimefanya hiyo kazi kwa miaka 14, nilishiriki kutengeneza kanuni zilizoendesha bunge la katiba. Nagombea nafasi kwa sababu najiamini na nina uwezo.
Matiko: Tunatambua alikuwa naibu mwanasheria mkuu na hakupaswa kuwa mwananchama wa chama chochote, leo unaomba nafasi ya unaibu spika, ukiwa mtendaji lakini tayari unachukua upande wa CCM. Unatuaminisha vipi hautaegemea upande!
Tulia: Nilichukua fomu za kugombania uspika nikiwa naibu mwanasheria, kwa ibara ya 67(ii) na 72, anashikilia nafasi mpaka awe candidate na kuwa candidate ni mpaka upite mchakato.
Katiba nimeisoma, kanuni nimezisoma na yapo makundi matatu matatu yanakatazwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa ikiwemo wanajeshi!
Spika anamruhusu akakae baada ya baadhi ya wabunge kumtaka ajibu swali badala ya kuzunguka na kutokea sintofahamu.