Kutoka Bungeni - Jumamosi 21, Aprili 2012 (Videos)

HIlo Zee Toka Gombe(Wassira) halina tija sijui linamshauri nini Rais, wananchi wa Bunda piga chini hilo zee fukuzieni kwenye hifadhi linakotoka ya GOMBE hahahahahahaha
 
HIlo Zee Toka Gombe(Wassira) halina tija sijui linamshauri nini Rais, wananchi wa Bunda piga chini hilo zee fukuzieni kwenye hifadhi linakotoka ya GOMBE hahahahahahaha

Soma Signature yangu hapo CHini..yeye ameenda kusinzia bungeni bwana! Msimzonge zonge
 
Mbona EL alisimama akasema nimemwandikia Rais barua ya kujiuzuru, yy mbna hakusubr Rais akubali ndo atangaze. Suala hapa ni kuwa tumepigwa changa la macho,na JK ndo mbaya wetu.

Kwangu sioni tatizo la wao kusita kujiuzuru kwa vile ndio wanaendeleza wimbi zuri la upinzani kuchanja mbuga na wananchi kuendeleza hasira zao juu ya CCM na serikali yake. Siasa ya leo ni sayansi na kosa la mwenzake ni kheri kwako.
 
Acheni kukuza mambo.....nchi hii hivi sasa kuna mengi na ya msingi ya kujadili kuliko mambo kama haya....kwa akina siye tunaekutana na maneno kama haya wala hatuwezi kutafsiri vibaya kama ambavyo mnataka kulazimisha na ndio maana sio Mnyika wala Mbowe ambae aliitilia maanani kauli hiyo!! Binafsi hiyo tafsiri yake ni sawa na kusema "jembe lako"

Mbona sasa kaomba msamaha na kuipotezea kiana wewe magamba?
 
Uliposikia kuwa huyu Serukamba ni Nanihino...wa Ma-mvi ulielewa nini? Hujui huko kwenye bandari ndo kuna akina Karamagi marafiki wa Ma-mvi na RA
 
Katika wabunge bogasi huyu ameshika namba!Nasio leo tu,nimuda mrefu sana!We angalia kila anapochangia kitu bungeni ni utumbo tu ulioza!Nakwambia mwisho wake katika siasa zake zakutumwa unakaribia!Kigoma wanahopeless mbunge,Nawapa pole sana.
 
Muda Mfupi uliopita Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kamaliza mazungumzo na Waandihi wa Habari wa Vyombo mbalimbali na kusisitiza kuwa Taarifa kamili kuhusu Mawaziri wanaodaiwa kujiuzuru atazitoa rasmi Jumatatu atakapokuwa akiahirisha kikao cha Bunge.

Maswali ni mengi kwa kila nayeisikia kauli hii:

  1. Nini kimejitokeza hapa
  2. Kuna aliyezuia maamuzi haya yasipate baraka?
  3. PM kashikwa na kigugumizi gani?
  4. Mbona kila jambo katika kiako cha jana yalishafahamika mpaka maazimio?
  5. Kikao cha leo kilikuwa na Agenda gani?
  6. Ni kweli anasubiri baraka za Rais?
  7. Ilikuwa sanaa?
  8. Au ni mchezo gani unataka kufanyika hapa?
  9. Kwa nini Spika kaahirisha Bunge bila kuusoma Muongozo uliohusu ufafanuzi wa Serikali juu ya suala hili?
  10. Kwa nini wameiacha nchi katika sintofahamu kiasi hiki?


Ahadi yake ni Jumatatu

Game limeishia hapo kwa leo, Ila TUPO Dodoma na hakuna cha Mnadani wikiendi hii ni kona hadi kona hata kama yatakuwa maamuzi ya kushtukiza kama jana USIKU ghafla wakaghairi kuwapa niuz wanahabari. WE ARE MONITORING

Tunaendelea kusubiri


ADIOS
 
Hamjamfaham JK kwa kupenda ujiko na kudandia treni.

Anataka atangaze yeye hayo maamuzi ya kuwatoa Waziri ili aweke kumbukumbu ya kufanya maamuzi magumu.

Tuvute subira, ataibuka very soon!
 
Du!
Serikali hii ni ya mambo ya kichinichini sana!
Pinda nilishamsema kuwa hana maamuzi huyu m'baba!
 
GHOST RYDER!

Asante sana mkuu kwa kazi nzuri uliyojitolea kutuhabarisha muda wote wa tukio hili na hayo mengine yatakayojiri.

Shukrani Mkuu!
 
manongo we wa wapi ulidhan wanajiuzulu vp .wanaandika barua kwa baba riz then ndo anaridhia na ndicho kilichofanyika
 
Naomba ieleweke kwamba Mawaziri kadhaa kuandika barua za kujiuzuru uwaziri hazijawa confirmed na aliyewateua. Mpaka pale Rais atakapopokea na kukubali kujiuzuru kwao, vinginevyo wangali kazini. Full Stop. Tusiwe na hali ya kuendekeza zaidi vionjo bali taratibu za ajira na sheria za uajiri zifuate mkondo wake.

Uko sahihi Mkuu na hapa JF kilichowekewa msisitizo ni taarifa za wao kutakiwa (kushauriwa) na kamati ya wabunge wa CCM kupima kama wajiuzulu ama la, na walimuandikia Rais barua jana usiku, kila mmoja anajua alichoandika, japo wapo baadhi ambao hawakujiuzulu bali walieleza kilichotokea na kumwambia Rais aamue kulingana na uzito wa HOJA na kama walikosea wachukuliwe hatua. Baadhi walisema hoja ya wabunge wa CCM kwamba kujiuzulu kwao kutaikoa CCM haina maana kwa kuwa kujiuzulu kwa mawaziri wanane kutoka sekta nyeti ni kuiangusha CCM na si kuiokoa na ni kumuaibisha rais na si kumsaidia, ila kama kuna Waziri amekosea basi Rais asisite kumchukulia hatua haraka na kama kuna watendaji (kama wa TBS) ambao ni wateule wa Rais wameichafua serikali nao wachukuliwe hatua mara moja bila kuchelewa, badala ya kuwahukumu mawaziri wengi kwa kufuata mkumbo. Hapa ndipo pia wamempa JK wakati mgumu kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia ukweli na HAKI na si kufuata upepo, jazba na visasi vya kisiasa vya ndani ya CCM.

Hoja ya mmoja kusema kina Lowassa, na wenzake (Karamagi na Msabaha) walitangaza kujiuzulu ndani ya bunge; hiyo ilikuwa tofauti na ndio maana hadi sasa pia Lowassa mwenyewe anajuta maana hakujua kama amezungukwa na itamsumbua hadi leo, kwa hiyo hakuna atakayerudia makosa ya LOwassa kusema kwamba ameonewa sana halafu anajiuzulu wakati aliambiwa 'apime' kwa hiyo kipimo chake kilikua kuondoka. Pia, wakati ule JK alikua Dodoma na aliridhia walikutana kabla ya kutoa tamko lile, hawa mawaziri hakuna aliyekutana na JK (alikua Brazil) na hata barua wamezituma tu na Mkulo hayupo hata Dodoma kama ni kutuma naye katuma tu hiyo barua, kama ni kujieleza ama kujiuzulu.

Thread kuu ya JF haikusema wamejiuzulu kama baadhi ya magazeti yalivyosema bali ilisema;

"Mawaziri wanane watakiwa kung'oka"
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/254164-mawaziri-wanane-watakiwa-kungoka.html
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom