KUTIMULIWA ZITTO, Dk. Kitila CHASO: Uamuzi wa CC Chadema ni muafaka - Wasomi Mlimani

Hofu ya uchaguzi ndani ya chagadema ndio imeleta haya yote. Mbowe hataki kuachia kiti hata kwa njia a mtutu.bamewapanga vijana ili wawachafue wapinzani wake

cdm inapigania demokrasia ,,wakati hawana demokrasia ndani ya chama
 
Wasomi mbona wanaongea kama wanatumika na Mbo...we? Hizo sura zimedadavua uhalisia wa jambo mpaka kutoa tamko? Now wanafunzi wengi hawajapa bumu, hivyo kutumika kama k.....ya kiume ni rahisi tu. Nadhani buku 5 ilipita kumlinda mtwasi wa
 
CHADEMA YAPASUKA CHUONI DODOMA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA leo kimepata pigo jipya baada ya kupoteza wanachama wake 92 wakiongozwa na katibu wao ndugu Simon Mpandalume...


Mdau wetu toka Dodoma ametuarifu kuwa wanachama hao wamefikia maamuzi ya kurudisha kadi za CHADEMA na kujiunga na CCM kutokana na kukerwa na hatua ya chama hicho kumvua Zitto Kabwe nafasi zote uongozi .

Wamejiunga na CCM baada ya kuhongwa na chama hicho. Haiwezekani watu 92 waone CCM tu ilhali kuna vyama kadha wa kadha vya kisiasa. Kama shida yao ni Zitto kwanini wasijiunge na chama chake cha CHAUMA? Upuuzi mtupu!!!
 
View attachment 124022
Kiongozi Julius Mario wa Shirikisho la Vijana la
Umoja wa Wanavyuo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na
waandishi wa habari kuhusu kuunga mkono kwa Chadema kumvua uongozi Zitto kabwe.


Suala la kutimuliwa kwenye madaraka ya uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zitto Kabwe, na Mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo, sasa limechukua sura mpya.

Shirikisho la wanachama wanafunzi wa Chadema kutoka vyuo vya Elimu ya Juu, mkoa wa Dar es Salaam (Chaso), jana limeibuka na kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu Chadema kuwavua uongozi waliodaiwa kufanya uasi ndani ya chama

Shirikisho hilo pia limewarushia shutuma Mtela Mwampamba, Habib Mchange, Juliana Shonza na Greyson Nyakarungu, waliofukuzwa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), kutengeneza makundi ya kupinga uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu hiyo.

Akisoma tamko lao kwa niaba ya viongozi wenzake, Mratibu Mkuu wa shirikisho hilo, Himida Jackson, alisema mapema wiki hii kikundi cha vijana wanaojiita viongozi wa Chaso, waliibuka na kutoa taarifa ya kupinga maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu Chadema.

Tamko hilo ambalo limesainiwa na mratibu huyo pamoja na Afisa Habari wa shirikisho hilo, Amandus Gomba, limetokana na kikao kilichofanyika juzi Chadema na kufikia uamuzi wa kuliandaa kwa ajili ya umma wa Watanzania.

Alisema taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari wiki hii kuwa Chaso limepinga uamuzi wa kamati kuu siyo za kweli na kwamba waliozitoa hawatambuliki kwenye kumbukumbu za wanachama wao.

Alifafanua kuwa mapema mwaka huu Bavicha liliwafukuza baadhi ya vijana kwa usaliti wao ambapo waliotajwa hapo juu walikimbilia chama tawala.

“Kikundi hicho (waliofukuzwa) kimekuwa kikipita huko mtaani na kukusanya vijana wa CCM wanaojipachika uanachama wa Chadema na kujipatia vyeo vya Chaso kisha kutoa matamko ya kupinga maamuzi ya chama,” alisema.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakijitambulisha ni viongozi wa Chadema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati siyo kweli, huku akitaja majina ya viongozi wanaotambulika kuwa ni Marco Julius ambaye ni mwenyekiti na Daniel Mswelo, katibu.

Aliongeza kuwa, Januari 19, mwaka huu, uongozi wa Chaso Chuo Kikuu cha Ardhi ulisimamishwa kutokana na utendaji mbovu.

Alisema kwa misingi hiyo, vijana hao hawana uhalali wa kufanya shughuli zozote kwa ngazi ya uongozi au chama.

Alisema Jumapili iliyopita vijana hao walifanya jitihada za kushawishi wanafunzi wa vyuo vikuu kuungana nao katika kupinga maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu ingawa hawakufanikiwa katika hilo.

Alisema tamko la Jumatano ya wiki hii walilolitoa watu hao ni mwendelezo wa jitihada hizo walizozikusudia. Kutokana na hilo, amewataka wanachama watambue kuwa, tamko hilo siyo halali huku akisisitiza kuwa msimamo wao unaunga mkono maamuzi yaliyochukuliwa na Kamati Kuu hasa kwa kuhakikisha hakuna mtu yeyote aliye juu ya chama.

“Tunasisitiza chama kisiruhusu mmoja wetu abomoe nyumba hii hata kama alishiriki kuijenga au hatuwezi kuruhusu mtu atoboe mtumbwi tunaosafiria,” alisema.
Akizungumzia kuhusu chama, Jackson alisema ni chenye watu wenye nia ya dhati ya kulikomboa taifa na watu wake ambao wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

“Tunaamini Chadema ndicho chama pekee ambacho ni mbadala Tanzania kilichobeba matumaini ya Watanzania kwa kuwa kinapigania haki za kila mnyonge,” alisema.
Aliwataka wanachama na viongozi kuwa makini na kutosita kuchukua maamuzi dhidi ya mtu yeyote hasa katika kipindi hiki ambacho wamesikia kauli za viongozi wa CCM wanaojiapiza kuwa Chadema haitafika uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa Chadema UDSM, Julius Michael, alisema kuwa yanayoendelea hivi sasa ni propaganda ya CCM kutaka kukihujumu Chadema na kuonyesha yaliyoamuliwa na kamati kuu ni uonevu kwa sababu chama tawala hakijawahi kuchukua maamuzi magumu kama hayo.

Alisema baadhi ya vyombo vya habari (bila kuvitaja), vimenunuliwa na vimekuwa vikiripoti uamuzi huo wa kamati kuu tofauti.

Mjumbe wa Chaso, Gwamaka Mbughi alisema baadhi ya magazeti yaliandika bila uhalisia hivyo kupotosha umma.

Alisema kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama chao, Chaso hakina mamlaka ya kupinga maamuzi yaliyofikiwa. Mwenyekiti wa Chaso kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Musa Ndile, alisema maamuzi ya kamati ni halali hivyo inapotokea mtu ameenda kinyume bila kujali anakubalika kwa kiasi gani, hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa katiba yao.

Naaam,

Hawa wasomi halisi wa CHADEMA wamejitambulisha wanatoka vyuo gani.

Wale wasomi mamluki wangesema basi wanatakoa vyuo gani!

Hawa wasomi original wamesema kabisaa kwamba ni kifungu gani kimekiukwa kwenye katiba ya CHADEMA

Mbona wale wasomi wachumia tumbo walikua wanapiga porojo tu kama waokota makopo huko mitaani?
 
Dhambi hizi mbaya sana na Mh. Lema aliongeleza zaidi hii ya kwanza:
1. Dhambi ya woga imewagharimu ccm na sasa badala ya kujenga chama chao wanaangalia kudhoofisha upinzani.
2. Dhambi ya usaliti nayo ilikuwa haijaelezwa sana lakini sasa tutaweza kushuhudia jinsi inavyotafuna wahusika.


Hata wakipambana vipi ukashinda lakini ukishaandika historia ya usaliti huwezi kuishi kwa amani, ZZK na wenzake hawataweza kuwa na Amani mioyoni mwao maisha yao yote.
 
Ndani ya Katiba ya Chadema toleo la 2006. Katika Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama. Sura ya 10, Ibara ya ix, imeandikwa: "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya Uongozi wa Chama au Wanachama wake."

Na katika Katiba hiyo hiyo Sura ya 7 kuhusu kazi za Kamati Kuu, Ibara ya 7, Ibara ndogo t, imeandikwa: "Kufanya uamuzi juu ya mapendekezo ya kufukuza Mwanachama." Na Ibara ndogo v, imeandikwa: "Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, Kanuni na Maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake."

Hata wakipambana vipi ukashinda lakini ukishaandika historia ya usaliti huwezi kuishi kwa amani, ZZK na wenzake hawataweza kuwa na Amani mioyoni mwao maisha yao yote.
 
Usitumie kichwa kufuga tu nywele ww, ccm imeingiaje hapa? Mnauwa watu kwa sumu na tindikali, mnang'ang'ania madaraka, mnakula ruzuku na mahawara zenu mkihojiwa mnaanza kuweweseka. Jinga

Msaliti atabaki kuwa msaliti hata akitetewa vipi ile dhambi ya usaliti haifutiki kamwe.
 
Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu

Je, CCM ni chama cha kiislamu?
 
Hao pia ni mamluki na swali dogo mbona vyama vingine hapa jamani hamna eti kila aneondoka anaenda ccm kulikoni hapa?
 
"ZZK naye si alikuwa kiongozi tena ngazi ya juu sana, kwa nini alikimbilia kwenye vyombo vya Habari kabla ya kutoa taarifa kwenye vikao??? Anatafuta personal attention.. ---- yule..
 
Nguvu za Mh. Zitto na crew yake ndani na nje ya CHADEMA tutazifahamu siku ambayo atapokonywa kadi ya CHADEMA na kuamua kupambana kihoja katika majukwaa ya kisiasa na kwenye vyombo vya sheria.

Kinachoendelea kwa saa ni kama mazoezi huku pande zote zikirushiana maneno katika mpambano unaosubiriwa kwa hamu sana na wananchi wanaofuatilia siasa za Tanzania.
 
Nguvu za Mh. Zitto na crew yake ndani na nje ya CHADEMA tutazifahamu siku ambayo atapokonywa kadi ya CHADEMA na kuamua kupambana kihoja katika majukwaa ya kisiasa.
Nguvu ya Mh. Zitto na crew? Je, baada ya kupokonywa kadi, hayo majukwaa ya kisiasa atakapoamua kupambana kihoja ni yapi? la CCM? la CUF? la TLP au la NCCR Mageuzi?
na kwenye vyombo vya sheria.
Alaa kumbe! Yale yale ya Mbunge wa Jimbo la Wawi, Mhe. Hamad Rashid Mohamed vs CUF au Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mwanza, Mh. Henry Matata vs Chadema ...kaazi kweli kweli.
Kinachoendelea kwa saa ni kama mazoezi huku pande zote zikirushiana maneno katika mpambano unaosubiriwa kwa hamu sana na wananchi wanaofuatilia siasa za Tanzania.
Pande zote? Unachekesha kweli ndugu yangu, mpambano upi unasubiriwa, CCM vs Chadema? Serikali vs upinzani au vyombo vya dola vs raia wema? Ng'wamapalala, see how ridiculous all this sounds?
 
Back
Top Bottom