Kutimiza Ahadi

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Una mpenzi/mume/mke wako na imani iliyoko katika mahusiano ya mapenzi ni kwamba wapendanao hawatakiwi kufichana mambo yanayowahusu. Kwa upande mwingine kila mmoja anao marafiki wake binafsi kulingana na kazi, ujirani, shule, n.k. Chukulia inatokea katika kuongea na mmoja wa rafiki yako kukawa na suala fulani mmeliongea, suala hilo likawa linamhusu mwenzi wako kwa namna moja ama nyingine, na rafiki yako akakuomba liwe siri kati yako na yeye tu( usimwambie hata mwenza wako). Kwa upande mwingi Mwenza wako akabahatika kulifahamu suala hilo na wakati akijaribu kukuelezea ikaonekana wewe ulilifahamu kabla. Hali hiyo inamfanya mwenza wako kuudhika.


Je utakuwa umemtendea kosa mwenza wako kwa kutomwambia suala ambalo mlikubaliana na rafiki yako (ambaye siyo mwenza wako) kwamba liwe siri kati yenu. Au kwa maneno mengine, tunalazimika kuvunja ahadi zetu za usiri tunazoweka ili kuloinda uaminifu, uwazi na mapenzi kati ya wawili wapendanao?
 
and where is 'the two shall become one' thing?
Kama ni jambo la kwenu pekee yenu na halimhusu sawa.
 
Back
Top Bottom