Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,952
- 46,713
Baada ya Rais Samia kumtengua naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria, Pauline Gekul ambaye siku tatu kabla ya utenguzi huo kulijaa tuhuma nzito za vitendo viovu dhidi yake kumeibuka watetezi wake mbalimbali wanaodhani hakutendewa haki hasa wakidai hajapewa haki ya kusikilizwa.
Kwanza ni vyema kufahamu nchini Tanzania ukiondoa nafasi za majaji, CAG na gavana wa BoT, Rais anao uwezo kumtengua mtu yeyote aliyemteua katika nafasi nyingine yoyote yeye mwenyewe au aliyeteuliwa na wateule wake bila kulazimika kutoa sababu yoyote.
Tanzania kutenguliwa katika nafasi yako na Rais ni jambo rahisi zaidi kwa sababu bunge huwa hata halihusiki kufanya vetting na kuthibitisha wateule wa nafasi yeyote serikalini, hiyo inamaanisha hakuna hata gharama za mivutano ya kisiasa katika kuteua na kutenguliwa kwa viongozi, tofauti na nchi ambazo Rais anahitajika kupeleka wateule wake bungeni kuthibitishwa.
Pili, ni kelele za haki ya kusikilizwa.
Watu wengi wanaomteta Pauline Gekuli kwa kigezo cha haki ya kusikilizwa wanashindwa kufahamu Pauline Gekul hajahukumiwa wala hajafungwa. Kutenguliwa sio kuhukumiwa na hata barua yenyewe haijasema sababu za utenguzi kwa sababu mamlaka yake hailazimiki kuhitaji sababu kumtengua.
Tatu, haki ya kusikilizwa ni mahususi na muafaka kwa Polisi, Mahakamani na vyombo vilivyo na hali ya umahakama tu katika utendaji kazi wake( quasi-judicial bodies). Raia wa kawaida, umma, vyombo vya habari n.k havilazimiki kumsikiliza mtu ili kumtuhumu au kusema amefanya uovu fulani. Rais haihitaji kusikiliza au sababu yoyote kutengua, hata akiona mteule ni mzigo tu au hana manufaa ya kisiasa kwake anaweza kumtengua.