Kutenguliwa kwa Gekul na nakisi ya elimu ya uraia kuhusu haki ya kusikilizwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,362
Baada ya Rais Samia kumtengua naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria, Pauline Gekul ambaye siku tatu kabla ya utenguzi huo kulijaa tuhuma nzito za vitendo viovu dhidi yake kumeibuka watetezi wake mbalimbali wanaodhani hakutendewa haki hasa wakidai hajapewa haki ya kusikilizwa.

Kwanza ni vyema kufahamu nchini Tanzania ukiondoa nafasi za majaji, CAG na gavana wa BoT, Rais anao uwezo kumtengua mtu yeyote aliyemteua katika nafasi nyingine yoyote yeye mwenyewe au aliyeteuliwa na wateule wake bila kulazimika kutoa sababu yoyote.

Tanzania kutenguliwa katika nafasi yako na Rais ni jambo rahisi zaidi kwa sababu bunge huwa hata halihusiki kufanya vetting na kuthibitisha wateule wa nafasi yeyote serikalini, hiyo inamaanisha hakuna hata gharama za mivutano ya kisiasa katika kuteua na kutenguliwa kwa viongozi, tofauti na nchi ambazo Rais anahitajika kupeleka wateule wake bungeni kuthibitishwa.

Pili, ni kelele za haki ya kusikilizwa.
Watu wengi wanaomteta Pauline Gekuli kwa kigezo cha haki ya kusikilizwa wanashindwa kufahamu Pauline Gekul hajahukumiwa wala hajafungwa. Kutenguliwa sio kuhukumiwa na hata barua yenyewe haijasema sababu za utenguzi kwa sababu mamlaka yake hailazimiki kuhitaji sababu kumtengua.

Tatu, haki ya kusikilizwa ni mahususi na muafaka kwa Polisi, Mahakamani na vyombo vilivyo na hali ya umahakama tu katika utendaji kazi wake( quasi-judicial bodies). Raia wa kawaida, umma, vyombo vya habari n.k havilazimiki kumsikiliza mtu ili kumtuhumu au kusema amefanya uovu fulani. Rais haihitaji kusikiliza au sababu yoyote kutengua, hata akiona mteule ni mzigo tu au hana manufaa ya kisiasa kwake anaweza kumtengua.
 
Huyo mama katili kuliko shetani mwenyewe. Kafuatilie alichomfanyia mume wake, ndio utajua ya huyo kijana yalikuwa ni Chamtoto.
 
Mkuu kuna video inayoonesha Gekul akifanya kitendo hicho?
Kwa hiyo unaona anasingiziwa?
Hivi unajua ukiwa kiongoz hutakiwi kuwa na tuhuma za kipumbavu hivo

Huwez kumuingizia binadamu mwenzako chupa matakoni aise

Sasa ataitwa rasmi mama chupa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
CDM inatengeneza watu wa ajabu ajabu, wahuni kama akina Martini, Katambi, yule kichaa wa Tunduma, ndumilakuwili kama ZZK, wavuta bange kama akina Mdude, watu katili kama akina Gekul, walevi kama akina Waitara, wafanyabiashara wa siasa kama akina Mbowe N.K
 
Hakuna aliyepinga Gekui kutenguliwa kwani Haki ya Kuteua na Kutengua anayo Mteuaji

Hapa tunazungumzia Wanasiasa wanaomshambulia kabla hatujasikia Utetezi wake

Uwage unaelewa meku
Katibu mwenezi anagawa haki kama hakimu kwenye majukwaa ya siasa.
 
Baada ya Rais Samia kumtengua naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria, Pauline Gekul ambaye siku tatu kabla ya utenguzi huo kulijaa tuhuma nzito za vitendo viovu dhidi yake kumeibuka watetezi wake mbalimbali wanaodhani hakutendewa haki hasa wakidai hajapewa haki ya kusikilizwa.

Kwanza ni vyema kufahamu nchini Tanzania ukiondoa nafasi za majaji, CAG na gavana wa BoT, Rais anao uwezo kumtengua mtu yeyote aliyemteua katika nafasi nyingine yoyote yeye mwenyewe au aliyeteuliwa na wateule wake bila kulazimika kutoa sababu yoyote.

Tanzania kutenguliwa katika nafasi yako na Rais ni jambo rahisi zaidi kwa sababu bunge huwa hata halihusiki kufanya vetting na kuthibitisha wateule wa nafasi yeyote serikalini, hiyo inamaanisha hakuna hata gharama za mivutano ya kisiasa katika kuteua na kutenguliwa kwa viongozi, tofauti na nchi ambazo Rais anahitajika kupeleka wateule wake bungeni kuthibitishwa.

Pili, ni kelele za haki ya kusikilizwa.
Watu wengi wanaomteta Pauline Gekuli kwa kigezo cha haki ya kusikilizwa wanashindwa kufahamu Pauline Gekul hajahukumiwa wala hajafungwa. Kutenguliwa sio kuhukumiwa na hata barua yenyewe haijasema sababu za utenguzi kwa sababu mamlaka yake hailazimiki kuhitaji sababu kumtengua.

Tatu, haki ya kusikilizwa ni mahususi na muafaka kwa Polisi, Mahakamani na vyombo vilivyo na hali ya umahakama tu katika utendaji kazi wake( quasi-judicial bodies). Raia wa kawaida, umma, vyombo vya habari n.k havilazimiki kumsikiliza mtu ili kumtuhumu au kusema amefanya uovu fulani. Rais haihitaji kusikiliza au sababu yoyote kutengua, hata akiona mteule ni mzigo tu au hana manufaa ya kisiasa kwake anaweza kumtengua.
Kwenye siasa hakuna kinachoitwa Haki ya kusikilizwa,hiyo ipo Mahakamani huko.

Ungefangiwa wewe harafu aliyekufanya apewe Haki ya kusikilizwa
 
Alihitaji kusikilizwa kwa sababu tayari kulikuwa na tuhuma juu yake. Kwanini hakutenguliwa kabla ya tuhuma hizo?
 
Inaonekana ni rahisi sana kuwajibishwa kwa mwanasiasa wa kanda ya Kaskazini katika utawala huu wa awamu ya sita kuliko wanasiasa kutoka pande zingine. Mara kibao wanasiasa wamekuwa na tuhuma lkn hawakuwajibishwa haraka haraka kama ilivyotokea kwa Pauline Gekul.
 
Alihitaji kusikilizwa kwa sababu tayari kulikuwa na tuhuma juu yake. Kwanini hakutenguliwa kabla ya tuhuma hizo?
Rais akikuona hata ni mzigo au hauna faida kisiasa kwake anaweza kuketengua, wala hahiitaji tuhuma au uwe umefanya kosa lolote na wala hahitajiki kukusikiliza au kutoa sababu.
 
CDM inatengeneza watu wa ajabu ajabu, wahuni kama akina Martini, Katambi, yule kichaa wa Tunduma, ndumilakuwili kama ZZK, wavuta bange kama akina Mdude, watu katili kama akina Gekul, walevi kama akina Waitara, wafanyabiashara wa siasa kama akina Mbowe N.K
Sasa ccm yenye Serikali na vyombo vyote, Tiss wakiwemo, wanakuwa wamelala usingizi? Hivi unatumia nini kufikiri kabla hujaanika upumbavu wa kiwango hiki!! Uone mlivyo wazembe na wajinga, hao mliowaiba kwa kuwahonga, mlidhani Mungu amelala!! Kama mlimuona Pauline anawafaa bila shaka anafanana na nyie ccm, mmemchukua 2018, na 2020 mkahakikisha mnaharibu uchaguzi ili abaki leo mnalia!!! Shindwa pepo mchafu.
 
Back
Top Bottom