Plot4Sale Kusudio la kuuza kiwanja chenye ukubwa 1.48 hectres = sqm2 14,800 Dodoma eneo la Mwangaza

Papaa pedeshee

JF-Expert Member
Nov 7, 2021
234
337
Ndugu wana JF habari ya majukumu?

Napenda kutoa taarifa juu ya kusudio la kuuza kiwanja namba 10 D-centre Mwangaza lililopo Dodoma mara tu baada ya kukamilisha upatikanaji wa Hati ya eneo hilo ifikapo mwakani mwezi Januari au Februari kwakuwa eneo lilikuwa limetwaliwa na wenye nguvu almaarufu vigogo tena wakiwa Serikalini lakini bahati nzuri MUNGU wetu wa familia amekuwa juu yetu na mambo yanakwenda vizuri sana.

Kiufupi eneo hilo lilikuwa lina offer na likimilikiwa na aliyekuwa bingwa wa magonjwa ya Moyo nchini na mmiliki wa Taasisi ya magonjwa ya moyo (THI) Dr. Masau aliyefariki 2013, hivyo eneo linatambulika kwa jina la Dr. Ferdinard Masau Heart Institute company ltd.

Eneo hilo limetenganishwa na barabara ya lami iendayo kisasa hadi UDOM huku linapakana na nyumba 300 wanazokaa watumishi wa serikali, upande mwingine magharibi linapakana na kigango cha kanisa katoliki na sambamba pia na shule ya Raisei primary English medium school kwa upande mwingine.

Halikadhalika upande wa juu yake kuna apartment na makazi ya watu, huku ukiangalia SGR ikipita na kukiwa na kituo chake umbali kadhaa tokea eneo la kiwanja.

Hivyo kiwanja kilitolewa kwa ajili ya Taasisi na hivyo tunakusudia kubadilisha matumizi yake hapo baadaye.

Kuhusu bei; eneo linakadiriwa kubwa na thamani isiyopungua 300M. Hata hivyo tathmini itafanyika kabla ya kuuza eneo hilo.

Kwa leo sitaweka picha kutokana na simu yangu kupata shida kidogo lakini wakati ukifika nitaweka kila kilicho muhimu kuwepo, hivyo kwa leo pokeeni kama taarifa tu wana JF.

Nb. Eneo linafaa pia kwa matumizi ya petro station na majengo ya kibiashara.

Naomba kuwasilisha.
 
Ndugu wana JF habari ya majukumu?

Napenda kutoa taarifa juu ya kusudio la kuuza kiwanja namba 10 D-centre Mwangaza lililopo Dodoma mara tu baada ya kukamilisha upatikanaji wa Hati ya eneo hilo ifikapo mwakani mwezi januari au februari kwakuwa eneo lilikuwa limetwaliwa na wenye nguvu almaarufu vigogo tena wakiwa serikalini lakini bahati nzuri MUNGU wetu wa familia amekuwa juu yetu na mambo yanakwenda vizuri sana.

Kiufupi eneo hilo lilikuwa lina offer na likimilikiwa na aliyekuwa bingwa wa magonjwa ya Moyo nchini Dr.Masau aliyefariki 2013 baada ya kufilisiwa taasisi yake ya magonjwa ya moyo nchini (THI), eneo liko kwa jina la Dr.Ferdinard Masau Heart Institute company ltd.

Eneo hilo linapakana limetengeneshwa na barabara ya lami iendayo kisasa hadi UDOM huku linapakana na nyumba 300 wanazokaa watumishi wa serikali, upande mwingine mashariki linapakana na kigango cha kanisa katoliki na sambamba pia na shule ya Raisei primary English medium school.

Halikadhalika upande wa juu yake kuna apartment na makazi ya watu, huku ukiangalia SGR ikipita na kukiwa na kituo chake umbali kadhaa tokea eneo la kiwanja.

Hivyo kiwanja kilitolewa kwa ajili ya Taasisi na hivyo kukusudia kubadilisha matumizi yake na bei yake haitapungua 300M. Hata hivyo tathmini itafanyika kabla ya kuuza eneo hilo.

Kwa leo zitaweka picha kutokana na simu yangu kupata shida kidogo.
300m Dodoma ilisha shuka bei mwendazake aliwapa matumaini makubwa sana, kwasasa hivi hata ikiwa nusu ya hiyo bei bado kubwa.
 
300m Dodoma ilisha shuka bei mwendazake aliwapa matumaini makubwa sana, kwasasa hivi hata ikiwa nusu ya hiyo bei bado kubwa.
Natambua hilo lakini tathmini itaamua vema maana eneo liko pazuri sana na ikishindikana litabaki likipumua tu kamanda,ardhi haiozi na ni mali.
 
Natambua hilo lakini tathmini itaamua vema maana eneo liko pazuri sana na ikishindikana litabaki likipumua tu kamanda,ardhi haiozi na ni mali.
Kumbe hauku serious una jaribu kuchek soko liko je ila kwa 300m kwa Tz ya sasa sio rahisi labda uuzie hao majirani zako kabisa au shule,
 
Kumbe hauku serious una jaribu kuchek soko liko je ila kwa 300m kwa Tz ya sasa sio rahisi labda uuzie hao majirani zako kabisa au shule,
Ni serious lakini ni vema kupima kama kitu hicho au jambo fulani lina manufaa unayokusudia au Lah! Na siyo kuuza kwa sababu umetangaza hivyo na mara kadha watz wakiona unauza kitu,fikira za kwanza ni kuona mtu huyo anashida na hivyo kukudidimiza. Kwa hapa muda utaamua mkuu.
 
Jaribu kuongea na kanisa walinunue wakigoma jenga msikiti watu wafanye ibada!
 
300m Dodoma ilisha shuka bei mwendazake aliwapa matumaini makubwa sana, kwasasa hivi hata ikiwa nusu ya hiyo bei bado kubwa.
Usinitoneshe kidonda nilinunua ekari kadhaa Chato now nimemwachia mungu.
 
Usinitoneshe kidonda nilinunua ekari kadhaa Chato now nimemwachia mungu.
Duh! Pole sana mkuu, kila maisha ya mtu yana historia yake. Endelea kuitunza pengine itakuja kukulipa baadaye japo Chato iko pembeni sana kimazingira tofauti na ingekuwa Mwanza au morogoro.jipe muda mkuu.
 
Back
Top Bottom