Kusitisha Mikataba Mikubwa (Mining Moratorium); Magufuli Asipoteze Nafasi Hii

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,490
40,020
Na. M. M. Mwanakijiji

Kati ya mambo mengi ambayo Watanzania wameyalalamikia sana kwani athari zake na matokeo yake yanajulikana sana ni mikataba mikubwa ya madini. Wengi tumelalamikia masuala haya kwa karibu miongo miwili sasa kwani tumekuwa tukiamini kabisa kuwa tungeweza kuwa na mikataba mizuri kabisa ya madini ambayo kweli ingekuwa inanufaisha taifa lakini pia inawanufaisha wawekezaji. Kwamba, tumekuwa tukitaka mikataba yeyote ile iwe mwisho wa siku ni ya manufaa kwa taifa na manufaa hayo yaonekane.

Hivyo, sakata la "makanikia" limetoa fursa ya pekee kwa Taifa kujichunguza na kuchunguza kama katika weledi na ujuzi wetu wote hapa ndipo tumefikia kikomo. Kwamba, mikataba tuliyoingia ndio tumepata 'the best deal' au tungejadiliana vizuri labda tungepata dili nzuri zaidi.

Ni kwa sababu hiyo binafsi ninaamini nafasi hii ya kupitia sheria na mambo mbalimbali kuhusiana na sekta ya madini si ya kuipoteza. Vyovyote vile itakavyokuwa katika ripoti itakayowasilishwa muda si mrefu ujao ni jukumu letu kuhakikisha kuwa haturudi na kuacha hali iendelee kuwa ilivyokuwa - the status quo should not be maintained. Hivyo basi, ni maombi yangu kwa Rais Magufuli hasa kutokana uthubutu ambao ameshauonesha na jinsi ambavyo ameonesha kuwa yuko tayari kufanya kile kinacholazimika basi afanye kile kinachopaswa.

1. Kutangaza usitishwaji wa muda wa uchimbaji wa madini kupitia makampuni makubwa ya kigeni (temporary moratorium in mining). Usitishaji huu uwe wa angalau (minimum) miezi sita ili kupisha:

a. Upitiaji wa sera na sheria ya madini ya Tanzania kuangalia mapungufu yake na pamoja na hizo kuangalia sera na sheria nyingine zinazoingilia na sekta hii ili kuzioanisha na kuhakikisha kuwa zinasahihishwa ili kuondoa mianya mbalimbali na mapungufu mbalimbali ambayo tayari yanajulikana au ambayo yatajulikana ndani ya muda huo.

b. Kutoa nafasi kuweza kupitia mikataba yote mikubwa na kuweza kuona mapungufu yaliyomo lakini vile vile kuanzisha mazungumzo mapya na makampuni hayo chini ya mwanga wa mabadiliko ya sera na sheria ya madini. Ni vizuri kuweka ushawishi ili makampuni haya yatambue kuwa tunataka wafanikiwe lakini kufanikiwa kwao kuwe ni kufanikiwa kwa taifa kwa ujumla lakini pia kufanikiwa kwa jamii ambayo inazunguka migodi hiyo.

2. Kusitisha kwa muda utafutaji wa mafuta ili kupitia sheria na sera husika ili kuweza kuweka mazingira yanayofaa kisheria na kisera kwa sekta hiyo. Lengo ni kuhakikisha kuwa wakati uchimbaji wa mafuta utakapoanza baadhi ya matatizo ambayo tumeyaona kwenye nchi nyingine yasije kutokea kwetu kwani tutakuwa tumeyatarajia na kuyashughulikia.

3. Kusaini mikataba mipya chini ya sheria mpya madini - Ni jambo muhimu kuhakikisha kuwa makampuni makubwa yanaingia katika majadiliano mapya (renegotiation) ya mikataba au baadhi ya vipengele vya mikataba hiyo chini ya mwanga wa sheria mpya ambayo itapitishwa katika muda huu wa miezi sita ya moratorium.

Endapo hili litafanikiwa nina uhakika tutakuwa tumeepusha matatizo mengi ya mbeleni lakini pia tutakuwa tumeonesha nia njema ya kuweza kushirikiana na wawekezaji katika kushughulikia matatizo haya ili kuepuka migongano isiyo ya lazima huko mbeleni.

4. Kwa vile suala hili linahusiana na utajiri wa nchi wa asili; ni vizuri kabisa na ni lazima ielezwe na ieleweke na wawekezaji wote (wa ndani na wa nje) utajiri wetu huu wa asili hauozi. Endapo makampuni makubwa yataona kuwa hayako tayari kufanya majadiliano upya kwa sababu yeyote ile au kwa madai ya kutaka mikataba ya sasa (hata kama ina mapungufu mengi) iheshimiwe basi iwekwe wazi kabisa kuwa kama taifa tunaweza kujitoa kwenye instruments zozote za kimataifa ambazo zinatufunga ili kuhakikisha kuwa tunalinda utajiri huu wa asili kwani mwisho wa siku ni sisi wa kizazi hiki tutakaolaumiwa na watoto wetu endapo watakuta mashimo ya yaliyokuwa machimbo ya madini na wao hawaoni tofauti yeyote.

Kama kwenye nchi za Kiarabu zimeweza kutumia mafuta yao kujenga mataifa yao na kutengeneza mifuko mikubwa ya utajiri wa nchi (sovereign wealth funds). Na sisi tunaweza kufanya hivyo na ninaamini tunaweza kufanya hivyo si kwa madini tu bali pia kwenye utajiri mwingine wa asili ukiwemo utalii.

Ni maombi yangu kuwa nafasi hii ni kama penati ya kuamua nani anashinda kombe la dunia katika dakika za nyongeza. Si nafasi ya kuipoteza lakini pia ni nafasi ambayo inahitaji hekima, busara, weledi, uthubutu, maono na uongozi usioyumbishwa. Naamini Magufuli anaweza kufanya hili na kuipa Tanzania nafasi yake ya kufanikiwa kwa kutumia utajiri wake.

Kwa vile tayari yeye ameshaonesha kuchoshwa na hali ya kuwa ombaomba hata kwa malori ya takataka ni wakati sasa kuonesha ni jinsi gani tunaweza kutumia utajiri wetu kujenga nchi yetu na kuona fahari kufanya hivyo.

MMM
 
All that shit said, law does not operate retrospectively!
 
Nakubaliana nawe MMJ. Hapo ndipo tutakapojua kama wazungu wanajali au la, utawaona tu. Nchi hii ilifika pabaya. Mtu anasaini mikataba utadhani wajukuu zake hawataishi nchi hii. Urais mtamu, uongozi mtamu, ufisadi mtamu, hela tamu, wananchi mtajijua wenyewe.

Ngoja tuone mapendekezo ya report ya leo.
 
Lakini wakati inasainiwa mbona tuliunga mkono leo tumegeuka ukinyonga wetu ni hatari zaidi katika mustakabali wa maendeleo, tatizo letu huwa hatufanyi tafiti ila tunaamini viongozi ndo wako sahihi hata Leo ukiambiwa hatuibiwi naamini utageuka na kuamini hivyo
 
Na. M. M. Mwanakijiji

1. Kutangaza usitishwaji wa muda wa uchimbaji wa madini kupitia makampuni makubwa ya kigeni (temporary moratorium in mining). Usitishaji huu uwe wa angalau (minimum) miezi sita ili kupisha:

ni nafasi ambayo inahitaji hekima, busara, weledi, uthubutu, maono na uongozi usioyumbishwa. Naamini Magufuli anaweza kufanya hili na kuipa Tanzania nafasi yake ya kufanikiwa kwa kutumia utajiri wake.

Kwa vile tayari yeye ameshaonesha kuchoshwa na hali ya kuwa ombaomba hata kwa malori ya takataka ni wakati sasa kuonesha ni jinsi gani tunaweza kutumia utajiri wetu kujenga nchi yetu na kuona fahari kufanya hivyo.

MMM
Mzee Mwanakijiji,
I salute bandiko hili nimelipenda haswa ile closing ya kutokubali kuwa omba omba hadi wa magari ya taka.

Nimeipenda hoja ya re negotiations ili tupate a win win situation na sio hii iliyopo ya win lose situation.

La mikataba naliunga mkono na kwenye gesi nimewahi kutoa angalizo hili
Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Hata hivyo nina maswali machache
1. Hii temporary moratorium, ni moja ya vipengele kwenye mikataba yao? ,au unamaanisha tuivunje kwanza mikataba yote kwa kuisitisha kisha tutengeneze mikataba mipya?. Kufanya chochote ambacho sio part of contract ni kuvunja mkataba, sasa kwa vile umeishamjua Magufuli hili analiweza kutokana na hulka yake, hivyo unamchagiza avunje tuu, jee Tanzania iko tayari to pay the consequences ya kujitoa kwenye instruments zote za kimataifa tulizoridhia na kusaini?.
2. Hii hekima, busara, weledi, uthubutu, maono na uongozi usioyumbishwa tunayo?

All the best, let's wait and see, kiukweli miongoni mwa vitu ninavyovipenda kwenye hotuba za raisi Magufuli ni jinsi anavyosemaga ni jinsi gani hana time ya kusoma mitandao ya kijamii lakini huzijibu hoja zilizoibuliwa humu jf, mfano leo nina uhakika pia kuna mahali atazungumzia hoja hii kwa kuikanusha any possibility ya a compromise.

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli?

Paskali
 
Nimeandika kuwa ameandika "shit" akakasirikia! Nimempa na sababu... he can no longer be trusted!
Huyu bwana sijui bibi anacheza mchezo mbaya sana. Anapiga U-turn highway. Bahati mbaya sana watu kama hawa wana wafuasi wengi sana.
 
Back
Top Bottom