Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #21
Uzuri wa sera ya ccm kuhusu elimu ya msingi ni nini?
Uzuri wa sera ya ccm kuhusu elimu ya msingi ni nini?
chanzo cha umaskini wa watanzania sio sera bali ni WATANZANIA wenyewe...period......watu wa TZ na viongozi wao ndio chanzo cha matatizo yao......sera hazijitekelezi zenyewe bali zinatekelezwa na watu.......na pia sera hazijitungi zenyewe bali hutungwa na watu........Sijasema kushindwa kwa "utekelezaji" wa sera; bali kushindwa kwa 'sera" zenyewe. Yaani, ni 'substantial failure" ya sera za CCM ndio chanzo hasa cha umaskini wa Watanzania.
Siyo kukosekana kwa raslimali, siyo kukosekana kwa uwezo, fedha, mipango au hata raslimali watu; bali ni uwepo wa sera ambazo zimeshindwa kuyainua maisha ya WAtanzania. Kwamba hakuna sera hata moja ya CCM ambayo imefanikiwa na ikasifiwa kwa kufanya vizuri na kuinua maisha ya watu wetu. NONE.
Siyo Sera ya Elimu
Siyo sera ya Maji
Siyo sera ya Ajira
Siyo sera ya kodi/uchumi
Siyo sera ya uwekezaji
Siyo sera ya ubinafsishaji
Siyo sera ya ulinzi na usalama (kwanza hii haipo technically)
Siyo sera ya utawala bora
Siyo sera ya madini
Siyo sera ya nishati
Siyo sera ya mazingira
Siyo sera ya Utalii
Siyo sera ya "kilimo"
Siyo sera ya afya
Sera zote zimeshindwa.
Sasa sijasema hazijajaribiwa au kwamba hazijawahi kuwa na mafanikio madogomadogo ya hapa na pale la hasha nitakuwa si msema kweli. Shule zimejengwa, vyuo vimejengwa, barabara zimejengwa n.k Lakini ukizichukua sera zote na kuziweka kwenye mizani ya kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu wetu utaona kuwa sera hizo zimefeli. Ukishatambua hili ni rahisi kuona kuwa wanaojaribu kufanya CCM waboreshe sera zilizoshindwa wanafanya zoezi litakaloshindwa.
Hutaki?
Mwanakijiji,
Wadau wamechangia mengi yote yaliyosemwa yana ukweli mkubwa sana, wengi wameilaumu serikali, mimi naamini pamoja na serikali sisi wenyewe watanzania tunapaswa kubeba lawama kubwa; wananchi ndiyo wanayoipa changamoto serikali; kama unakumbuka wakati wa utawala wa Mwalimu kulikuwa na sera za maendeleo; kilimo kilipewa kipaumbele ili kuleta ajira na hatimaye maendeleo ya kiuchumi; yote hayo yalipotea baada ya utawala wa Mwalimu; kumbuka kilimo kinaajiri zaidi 60% kwa nchi zilizo kusini ya Sahara (sub Sahara countries); wakati nchi nyingi za sub Sahara zinawekeza kwa makusudi kwenye kilimo ili kuondoa umasikini uliokithiri; Tanzania iliacha matokeo yake ni haya ya umasikini, viwanda hatuna ajira zitatoka wapi? Sisi watanzania tumekuwa vigeugeu na ndiyo sababu tunachezewa na wanasiasa; tatizo sio sera za CCM ni watanzania wenyewe. Hata ikiingia Chadema madarakani kama watanzania hawatabadilika hakuna kitakachofanyika. Umegusia kupoteza dira, tatizo hatujui hata huko tunakoelekea, na hii ndiyo inayofanya tusijue kama tmepoteza dira.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Uzuri wa sera kwenye makaratasi unasaidia nini?
Chama,
Katika sera alizotoa Mwanakijiji nitajie moja ambayo Mwalimu alifanikiwa katika utawala wake? Mafanikio ni pale unapomkabidhi anayekufuatia kitu kilicho kamili. Na mwalimu hakufanikiwa katika hilo na mwenyewe alikiri.
Umezungumzia kilimo. Ukweli wa mambo, watanzania pamoja na elimu yao ndogo walikuwa wazalishaji wazuri wa chakula cha kujitosheleza wenyewe.
Sera moja iliyoharibu kilimo ilikuwa ni ya vijiji vya ujamaa. Na mwandisi wa sera hiyo ni JKN.
Chama,
Katika sera alizotoa Mwanakijiji nitajie moja ambayo Mwalimu alifanikiwa katika utawala wake? Mafanikio ni pale unapomkabidhi anayekufuatia kitu kilicho kamili. Na mwalimu hakufanikiwa katika hilo na mwenyewe alikiri.
Umezungumzia kilimo. Ukweli wa mambo, watanzania pamoja na elimu yao ndogo walikuwa wazalishaji wazuri wa chakula cha kujitosheleza wenyewe.Sera moja iliyoharibu kilimo ilikuwa ni ya vijiji vya ujamaa. Na mwandisi wa sera hiyo ni JKN.
...... Zakumi kinachojadiliwa ni sera za Chama na si mtu.Mzee Mwanakijiji: Re: Mdahalo: Kushindwa kwa sera za CCM ndio chanzo cha umaskini wa Watanzania!
Mwanakijiji,
Ukweli wa mambo. Napiga mabox hapa US na naona kuwa excellence inarithishwa. Utamaduni wa sera za kwenye makaratasi ulianza zamani, na mambo yanayofanyika sasa hivi ni wajukuu.
Hivi kuna sera zaidi ya hizo za CCM?
Nope! sera pekee zinazofanya kazi nchini ni za chama tawala; vyama vingine vinazo sera zao lakini havitawali na hivyo sera zao hazitekelezwi.
Ha ha ha,Sasa wapi mmefanikiwa ndugu KIKWETE,Ambapo hakuna any other Changamoto?
Mwanakijiji
Ni kweli zinaotumika ni sera ni za chama tawala kabla hujalaumu hicho chama tawala hebu jiulize je hao watawala waliopewa dhamana wanazifuata? Ndio sababu binafsi ziwezi kulaumu CCM kama chama; naamini kabisa sera za CCM kama zitafuatwa zitaondoa kero nyingi; wakulaumiwa ni watanzania wenyewe; wanachama wa CCM hawafiki hata mil.8 kwa mantiki hiyo serikali hii ilichaguliwa na watanzania, ni sisi tu wananchi wa kawaida ndio wenye uwezo wa kuishinikiza serikali, kama walivyofanya madaktari ipo siku watanzania wataweza.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Mwanakijiji,
Kwa muono wangu, tumeathiriwa sana na uamuzi wa wakubwa kuliweka pembeni azimio la Arusha. Kibaya zaidi, sioni hata kwenye vyama vingine kama kuna atakayekuja kutukomboa. Mazungumzo ya Mbowe na watanzania waishio Marekani miezi michache iliyopita yalinivunja moyo. Huwezi kuondokana na umaskini wakati mali na nyenzo nyingine ambazo zingekutoa kwenye umaskini umewapatia wengine kwa kisingizio cha kukosa mtaji kuvuna rasilimali hizo.