Kushangiliwa kwa Kafulila kwenye Msiba wa Regia kunaashiria nini?

Nimekuwapo kwenye viwanja vya Karimjee katika kumuaga Shujaa wetu Mh. Regia Mtema. Ni viongozi wengi walikuwapo, kuanzia wa Serikali pamoja na Waziri Mkuu ni Makamu wa Rais. Pia Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa Majeshi ya Polisi, n.k n.k.
Kilichonishangaza ni pale yalipokuwa yanasomwa majina ya Wawakilishi wa vyama vya Siasa ambao watalipiwa na Ofisi ya Bunge na kwamba wameteuliwa na Bunge kuwakilisha kwenye Mazishi hayo huko Ifakara. Pamoja na Kutajwa majina ya Wabunge mbalimbali wa CCM na Upinzani, Viwanja viliripuka pale Jina la Kafulila lilipotamkwa kama mmoja wa Wabunge watakaoiwakilisha NCCR Mageuzi kwenye Maziko hayo.
Bado najiuliza, Je kushangiliwa kwa Mh. Kafulila, kulikuwa kunatoa Ujumbe gani kwa akina
James Mbatia ambaye tulikuwa nae pale viwanjani?

Mwenye Macho haambiwi Ona!
Kwa sababu ulikua na mbatia eneo la tukio, ingependeza sana ungemuuliza kuwa ni ujumbe gani kaupata kwa hilo lililojiri.
 
"..Wananchi bado wanamkubali kutokana na michango yake bungeni ambapo mara nyingi alijali maslahi ya Umma kuliko matakwa ya chama chake.."
 
Kushangiliwa huko kuna maana kwamba, JAMII YA WATANZANIA bado inamtambua Mh. Kafulila kama mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hata mimi na wewe tunatambua hivyo.
 
..Ofisi ya Bunge wamepotoka ktk suala hili.

..sidhani kama wanaweza kufanya hivyo kwa wabunge wa CCM.
 
Back
Top Bottom