Kusema Rais anashauriwa vibaya ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana akili; naona ni ukosoaji wa kinafiki

Raisi hakosei labda atoke waziwazi akiri kuwa alikosea.

Tofauti na hapo, ikiwa nyeupe ni sifa kwa raisi na ikiwa nyeusi wateule wamempotosha na atawajibika mtia saini/mkuu wa idara/wizara n.k yeye kama yeye binafsi.

Thisi izi Afrika my furendi.
 
Kwema Wakuu!

Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza kutamka nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

Rais kama kakosea sema kakosea. Inatosha. Mambo ya kuanza kumtetea kuwa kashauriwa, sijui washauri wake ni wabaya ni kujaribu kumnasua na Matendo anayoyafanya. Ni kama unajaribu kueleza kuwa Rais Hakosei Jambo ambalo ni Uongo. Hakuna binadamu asiyekosea.

Kusema Rais anashauriwa vibaya kunatoa tafsiri na maana nyingi kama ifuatavyo;

1. Woga na unafiki
Unashindwa kuongea moja Kwa moja kuwa hapa Rais kakosea. Yaani kiufupi unashindwa kuwa mkweli. Watu Wanafiki wanatabia ya kutaka kuongea lakini wakiongea hushindwa kusema Ukweli. Wanakuwa na kiherehere na uchawa au upambe. Huo ni unafiki.
Wakweli wananamna mbili ya kufanya, ni aidha aseme ukweli wote pasipo kufichaficha au kunyamaza Kabisa. Sio kutoa mambo nusunusu.

2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi
Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.

Kwamba yeye akipewa ushauri anaufanya pasipo kufikiri. Kiufupi ni matusi kusema Rais anashauriwa vibaya.
Mbali na hivyo ni kujaribu kusema wapo Watu wanaomdharau Rais na kutokumheshimu(kutokumuogopa) ndio maana wanauwezo WA kumshauri vibaya(kumdanganya). Hiyo sio tuu kumtukana Rais Bali kutukana Taasisi nzima ya Urais.

3. Inamaanisha Rais ni Mbaya na muovu
Yaani waje Watu wakushauri hapo twende tukaibe, au tupige dili alafu ukakubali alafu atokee mtu aseme umeshauriwa vibaya.

Kikawaida washauri hutoa ushauri kulingana na MTU alivyo. Ukiwa Mbaya utapewa ushauri Mbaya. Ukiwa mzuri ni ngumu sana washauri kukupa ushauri Mbaya Kwa sababu wanakujua fika. Tena Kwa nafasi ya Rais ni ngumu MTU akakushauri vibaya ilhali anajua wewe ni Mwema.

Haya unashauriwa vibaya alafu unatenda Ule ushauri Mbaya. Alafu wasingiziwe washauri. Huo ni Uongo.
Kikawaida mtu hujaribiwa Kwa tamaa, matamanio yake. Ubaya wa mtu upo ndani ya MTU na ndio unaojaribiwa. Ubaya siku zote hautoki nje kwenda ndani ya MTU. Bali unatoka ndani ya mtu kwenda nje.
Nazungumzia Kwa Watu wazima.

Uovu au uhalifu mara nyingi haunaga kisingizio. Kama ulivyo Wema nao hauna kisingizio.

Ukiona jitu ni jizi, fisadi, jambazi, Muuaji, mbakaji, na dhambi zingine jua Yale ayafanyayo yanatoka ndani yake na hakuna sababu ya nje inayoweza mfanya MTU kuwa Mtu Mbaya.

Ukiona MTU ni Malaya anafanya ukahaba ili ajipatie fedha, umaskini anaosema ndio Sababu, huo ni Uongo. Ila yeye ndani yake ndio Yuko hivyo. Narurudia, ubaya wa mtu upo ndani yake na kamwe ubaya hautoki nje. Vinavyotokaje ni vichocheo tuu.

Hata hivyo, Mtu huweza kudanganywa na kupotoshwa kuhusu Jambo Fulani. Lakini mpotoshaji, na anayepotoshwa wote wanakuwa katika nafasi Sawa pale watendapo Kosa Hilo. Tena mtendaji anakuwa ndiye mkosaji Square.

Chagua Watu waadilifu, Wema na wapenda HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
You have hit on the nail good. Tuna Raisi goigoi
 
Swali ni hili: Umewahi kumsikia mtu kule Marekani anamwambia Rais anashauriwa vibaya? Ni hapa tu kwa unafiki watu husema ati Rais anashauriwa vibaya. Kule nchi ikienda vibaya moja kwa moja Rais anaambiwa ndiyo mwenye makosa. Au hujamwelewa mleta mda? Rais hata akiwa na advisors akiwa kichwa kitupu kama huyu mama obvious hata washauri wakimshauri ataishia STUPID tu
IMG_4567.jpeg
 
Ma Rais dunia nzima wanategemea ushauri....hakunaga kitu kama Rais mwenye akili...na Rais asie na akili..

Akili ya ma Rais wote hutegemea advisors ndo maana wenzetu wameenda mbali Sana na kuweka washauri rasmi wa Rais Kwa kila kitu...kuanzia siasa Hadi Uchumi...washauri wanatangazwa wanajulikana na CV zao zimeshiba

Wamarekani wameenda mbali zaidi
Mfano kuna mshauri wa uchumi anaelipwa wa Rais. Halafu kuna mshauri wa uchumi anaelipwa wa Makamu wa Rais ...halafu kuna waziri WA fedha na yeye ana mshauri wa uchumi anaelipwa wa waziri WA fedha...bado kuna washauri Tele wa wizara wanalipwa, the list goes on..

So Kwa Wamarekani likija suala la uchumi mezani Kwa Rais ...unakuta kuna PhD kama 10 hivi zimechangia Hilo wazo.....na mapendekezo.

You are only smart if you surround yourself with people who are more smarter than you
Unaweza kushauriwa hata na watu MILIONI 30.

Lakini bado una hiari ya kuchagua ukatae ushauri upi ukuballi upi. Bado kichwa chako ndio kitaamua.

Tena katiba yetu inasema Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

Kwahiyo ukiboronga ni wewe.

Suala la watu kusema, Rais kashauriwa vibaya ni la KINAFIKI, KICHAWA, KUJIKOMBKOMBA na kumuona Rais mungu mtu, hawezi kukosea, akikosea kapotoshwa.
 
Kwema Wakuu!

Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza kutamka nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

Rais kama kakosea sema kakosea. Inatosha. Mambo ya kuanza kumtetea kuwa kashauriwa, sijui washauri wake ni wabaya ni kujaribu kumnasua na Matendo anayoyafanya. Ni kama unajaribu kueleza kuwa Rais Hakosei Jambo ambalo ni Uongo. Hakuna binadamu asiyekosea.

Kusema Rais anashauriwa vibaya kunatoa tafsiri na maana nyingi kama ifuatavyo;

1. Woga na unafiki
Unashindwa kuongea moja Kwa moja kuwa hapa Rais kakosea. Yaani kiufupi unashindwa kuwa mkweli. Watu Wanafiki wanatabia ya kutaka kuongea lakini wakiongea hushindwa kusema Ukweli. Wanakuwa na kiherehere na uchawa au upambe. Huo ni unafiki.
Wakweli wananamna mbili ya kufanya, ni aidha aseme ukweli wote pasipo kufichaficha au kunyamaza Kabisa. Sio kutoa mambo nusunusu.

2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi

Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.

Kwamba yeye akipewa ushauri anaufanya pasipo kufikiri. Kiufupi ni matusi kusema Rais anashauriwa vibaya.
Mbali na hivyo ni kujaribu kusema wapo Watu wanaomdharau Rais na kutokumheshimu(kutokumuogopa) ndio maana wanauwezo WA kumshauri vibaya(kumdanganya). Hiyo sio tuu kumtukana Rais Bali kutukana Taasisi nzima ya Urais.

3. Inamaanisha Rais ni Mbaya na muovu
Yaani waje Watu wakushauri hapo twende tukaibe, au tupige dili alafu ukakubali alafu atokee mtu aseme umeshauriwa vibaya.

Kikawaida washauri hutoa ushauri kulingana na MTU alivyo. Ukiwa Mbaya utapewa ushauri Mbaya. Ukiwa mzuri ni ngumu sana washauri kukupa ushauri Mbaya Kwa sababu wanakujua fika. Tena Kwa nafasi ya Rais ni ngumu MTU akakushauri vibaya ilhali anajua wewe ni Mwema.

Haya unashauriwa vibaya alafu unatenda Ule ushauri Mbaya. Alafu wasingiziwe washauri. Huo ni Uongo.
Kikawaida mtu hujaribiwa Kwa tamaa, matamanio yake. Ubaya wa mtu upo ndani ya MTU na ndio unaojaribiwa. Ubaya siku zote hautoki nje kwenda ndani ya MTU. Bali unatoka ndani ya mtu kwenda nje.
Nazungumzia Kwa Watu wazima.

Uovu au uhalifu mara nyingi haunaga kisingizio. Kama ulivyo Wema nao hauna kisingizio.

Ukiona jitu ni jizi, fisadi, jambazi, Muuaji, mbakaji, na dhambi zingine jua Yale ayafanyayo yanatoka ndani yake na hakuna sababu ya nje inayoweza mfanya MTU kuwa Mtu Mbaya.

Ukiona MTU ni Malaya anafanya ukahaba ili ajipatie fedha, umaskini anaosema ndio Sababu, huo ni Uongo. Ila yeye ndani yake ndio Yuko hivyo. Narurudia, ubaya wa mtu upo ndani yake na kamwe ubaya hautoki nje. Vinavyotokaje ni vichocheo tuu.

Hata hivyo, Mtu huweza kudanganywa na kupotoshwa kuhusu Jambo Fulani. Lakini mpotoshaji, na anayepotoshwa wote wanakuwa katika nafasi Sawa pale watendapo Kosa Hilo. Tena mtendaji anakuwa ndiye mkosaji Square.

Chagua Watu waadilifu, Wema na wapenda HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wewe hapo ungekuwa na Rais na hivyo viakili vyako ungekuwa ndio Mwanasheria,injinia,daktari,mwanausalama nk?

Kuna watu wao ndio wenye hizo kazi Rais anawapa hints na wanampa mrejesho kama Kuna shida sometimes hao ndio wa kuwajibishwa.
 
Ukiangalia habari hii utaona kuna matatizo ya kimfumo yaliyowapita washauri, kiasi cha washauri wengine wanaotaka kutetea mkate wao kuona ni bora wanyamaze tu au washauri kinachotakiwa kusikika na wakubwa lakini si kinachopaswa kusikika.
Dah!... hatari kweli kweli...hapo penye kurekebisha mfumo ndio kipengele.
 
Umenikumbusha juzi wakati mafuta yalipopanda bei baada ya Ukraine war .. serikali ndo ikagundua kuwa wazo la National Oil reserves lipo kwenye makbrasha ...research ilishafanyika imebaki utekelezaji tu since wakati wa Nyerere. Hadi sasa hatuna National Oil reserves....very very strange
Dah!...tuna tatizo kubwa sana hasa kwenye utekelezaji wa tulichopanga nadhani tunahitaji sana kujifunza hapo.
 
Neno washauri limekuwa maarufu sana awamu hii sababu jamii bado inaamini mwanamke hawezi kuongoza nchi hivyo kuna watu nyuma yake kwenye kila kitu.

Ajabu akifanya jambo jema washauri hawatajwi.
 
Rais ndiye muamuzi wa mwisho, anapewa ushauri, lakini halazimiki kuukubali.

Pia, ana nyenzo na taasisi zote, zilizo rasmi na zisizo rasmi, kuhakiki ushauri wowote kabla ya kuukubali.

Kwa hiyo, akikubali ushauri mbaya, lawama ni zake.

Miaka ya 1970s Rais Nyerere alishauriwa na washauri wake rasmi wa uchumi kutaifisha maduka yote Tanzania. Mpaka maduka madogo kabisa ya mitaani.

Rais alikuwa anafikiri sana kuhusu suala hili, washauri wake rasmi walimshauri hivyo, lakini yeye alikuwa na shaka. Akamuita mzee mmoja wa Dar, Tabu Mangala. Huyo mzee hakuwa mchumi, hakuwa msomi, alikuwa ni mzee alwatan wa mjini tu (aliingia kwenye uongozi Yanga). Nyerere akamuuliza Tabu Mangala, akamwambia kuwa kashauriwa na washauri wake kutaifisha maduka yote, mzee Tabu Mangala anaona vipi suala hilo?

Mzee Tabu Mangala akamwambia Mwalimu Nyerere, chonde chonde baba, usifanye hivyo, utatuadhiri vibaya sana watu wa chini. Nyie taifisheni viwanda vikubwa, huku chini haya maduka ya mtaani tuachieni.

Nyerere akaacha ushauri wa washauri wake rasmi, wasomi wa uchumi, akachukua ushauri wa Tabu Mangala.

Habari hii inatufundisha nini?

Washauri hata wakiwa wasomi, wakati mwingine wanakosea.

Si lazima rais akubali ushauri wa washauri rasmi kila wakati.

Rais ana mkono mrefu unaoweza kupata ushauri kutoka sehemu mbalimbali zilizo rasmi na zisizo rasmi.

Hivyo, rais akipokea ushauri mbaya na kuufanyia kazi, of course washauri wana makosa, lakini wajibu wa mwisho ni wa rais, rais ana uwezo wa kupokea au kukataa ushauri wowote.

Rais Harry Truman wa Marekani alikuwa na kibao kwenye meza yake White House.

Kibao kile kiliandikwa "The Buck Stops Here".

Alisema kwamba kazi ya kuongoza nchi ina tatizo la watu kutupiana lawama sana, lakini, lawama zote zinaishia kwake, yeye ndiye anachukua lawama zote.
Hadi nimekumbuka Gibson Sembuli aaaaaaaaa!!!!!!!
 
Kama hiyi habari niyaukweli basi rais Nyerere alikuwa mjinga na Mpumbavu ...huwezi kukapata ushauri kwenye mambo ya straightforward kama hayo.
 
Mbona Nyerere alishauriwa vibaya kuhusu vijiji vya jamaa na watu wakafa na hatukusema Nyerere Hana akili??
No no no Usidanganye. Watu hawakufa kwasababu ya Vijiji vya Ujamaa. Kijiji gani hicho? Kama unayo taarifa kamili weka hapa au tukuite mdanganyifu hapa jamvini.
Kiuhalisia Raisi Julius Nyerere hakushauriwa vibaya kuhusu Ujamaa ila, viongozi walishindwa kuelimisha na kuratibu dhana yake hiyo. Ujamaa Village kwa lugha ya Leo unaweza kuifananisha na Economic zone minus all the jargons- na kwaavile alikuwa katika vita ya Uchumi, mipango mingi ilivurugika na ikavunjika. Wacha kupandikiza uwongo kwa Vijana.
 
Wewe hapo ungekuwa na Rais na hivyo viakili vyako ungekuwa ndio Mwanasheria,injinia,daktari,mwanausalama nk?

Kuna watu wao ndio wenye hizo kazi Rais anawapa hints na wanampa mrejesho kama Kuna shida sometimes hao ndio wa kuwajibishwa.

Hujui maana ya Rais. Itoshe kusema hivyo.
 
Wewe unajua?

Unaweza ukatamka neno alafu usijue maana yake, ndio wewe Sasa.

Ukishakuwa kiongozi au Mtawala jua lolote utakaloshauriwa liwe zuri au Baya. Ukilifanya jua wewe ndio umefanya. Hivyo mkosolewaji wa Kwanza ni wewe kiongozi.

Kama ungejua Maana ya Rais basi ungeelewa kuwa anauwezo, mamlaka, na nguvu ya kuchunguza Jambo(ukweli wake) Kabla hajalifanya.
 
Kila mara vitu vikianza kwenda kombo, swali au maswali tunayojiuliza ni Kwanini? Why?

Kwa kawaida tunasema oh haya mambo yametokea kwa sababu ya A B C au kwa matendo ya mtu, hapa Raisi. Mara nyingi hii ni kweli na athari inaweza kufuatiliwa kwa kurudi nyuma.

Lakini wakati hili ni kweli, hatupaswi kulaumu kila kitu kwa mtu mwingine au hapa kwa washauri tu. Kama agizo maelekezo amri na what have you yametoka juu, tunaweza kurudi juu, meaning from C to A. Na amini kila mtu ana wajibu kwa kile anachochagua kukifanya. Including hawa washauri. Wawajibike au Wawajibishwe.

Anyways, the Buck stops with her.

Nachelea kusema, haya ya kudai anashauriwa vibaya ni woga!
 
Hatuna tatizo la ushauri, tatizo letu ni kwamba nchi inaendeshwa kwa amri kutoka juu, haiendeshwi kwa kusikiliza ushauri wa kitaalamu.

Lawrence Mafuru, a very respected banker, alimshauri Magufuli kuhusu kubana mzunguko wa pesa kwa kasi kutakavyokuja kuharibu uchumi. Akamshauri Magufuli aende polepole. Magufuli alimtoa Mafuru kuwa Registrar wa Hazina, Mafuru basically akawa jobless mpaka Samia alivyomkumbuka baada ya Magufuli kufariki.

Hata kwenye IGA, wanasheria nguli wachache tu wangeweza jutuonesha matatizo makubwa yote. Nchi ina watu milioni zaidi ya sitini hii. Kuna watu kama kina Dr. Nshala wame specialize kwenye mikataba kama hii, wamesoma Harvard and Yale mambo haya, na kufanyia research kubwa. I am sure rais angemuita Dr. Nshala hata kama unofficial advisor aangalie mkataba, Dr. Nshala angemuonesha madudu.

Washauri wa serikali wanaendeshwa kisiasa mpaka wanajistukia, wanakuwa wanasikiliza kinachotakiwa kushauriwa, na wao wanashauri hichohicho.

Hivi nyie hamuelewi wapi?

Mimi nilikuwa na rafiki yangu mmoja, very smart chap, kafanya kwenye NGOs za elimu, kasoma mpaka Harvard, anajua mambo ya mitaani, very well rounded kuanzia kwa watu chini, mpaka Ivy Towers huko Harvard and Yale and Wall St. circles.

Alikuwa mwanaharakati sana mambo ya elimu. Kikwete akamuona huyu anasema sana, ngoja nimchukue nimuoneshe mambo yanavyoenda serikalini.

Akamteua kuwa mshauri wake mambo ya elimu. Jamaa akaona sasa hapa nimepata sikio la rais, nimechaguliwa kuwa mshauri, nitaleta impact, yale mambo yangu yote niliyokuwa nafanya activism sasa nitamwambia rais, tubadili policy serikalini. Nina sikio la rais sasa.

Jamaa akawa anamwambia Kikwete, hapa tufanye hivi na hivi. Kikwete anamjibu, hilo, hilo mbona tunalijua miaka mitano sasa, mfuate fulani wizarani atakupa makabrasha yote, walishafanya study na ripoti anayo.

Jamaa anamwambia Kikwete hapa kwenye elimu ya msingi mitaala tufanye hivi na hivi, Kikwete anamjibu hilo, hilo tushalisoma tangu enzi za Mungai, mfuate Katibu Mkuu Elimu atakupa makabrasha yote, tumefanya study na ripoti tunazo, tena nyingine wamekuja Wazimbabwe ku copy hapa mwaka jana.

Kila jamaa anachoshauri, anaambiwa tushafanya study, matokeo yapo wizarani, nenda kwa fulani utapata ripoti.

Jamaa akajitafakari sana, kama hawa watu wanajua kila kitu nilichofikiri nataka kuwashauri, mimi hapa nafanya kazi gani kama mshauri?

Akaona kumbe ali wa underestimate sana watu wa serikali kwa kufikiri hawajui mambo. Akagundua kwamba serikali ya Tanzania ina taarifa nyingi sana, ripoti nyingi sana, ina ushauri karibu wote inaouhitaji.

Tatizo si ushauri, tatizo ni political will, tatizo ni ulaji wa watu, watu wanaona wakibadili mambo ulaji wao utapotea.

Jamaa akaona kazi yake ya mshauri wa rais haina impact aliyotegemea.

Akaenda New York akachukua kazi ya kuongoza Foundation moja kubwa ya kimataifa. Akawa anafanya kazi za kimataifa huko, anaongoza taasisi yenye bajeti ya mabilioni ya dola.

Siku moja nilikaa naye New York City akanipa story hii mwenyewe.

Ukiangalia habari hii utaona kuna matatizo ya kimfumo yaliyowapita washauri, kiasi cha washauri wengine wanaotaka kutetea mkate wao kuona ni bora wanyamaze tu au washauri kinachotakiwa kusikika na wakubwa lakini si kinachopaswa kusikika.
Ww ndo mafuru ,eti well informed bank
 
Swali ni hili: Umewahi kumsikia mtu kule Marekani anamwambia Rais anashauriwa vibaya? Ni hapa tu kwa unafiki watu husema ati Rais anashauriwa vibaya. Kule nchi ikienda vibaya moja kwa moja Rais anaambiwa ndiyo mwenye makosa. Au hujamwelewa mleta mda? Rais hata akiwa na advisors akiwa kichwa kitupu kama huyu mama obvious hata washauri wakimshauri ataishia STUPID tu
Umemaliza kila kitu mjadala ufungwe
 
Unaweza ukatamka neno alafu usijue maana yake, ndio wewe Sasa.

Ukishakuwa kiongozi au Mtawala jua lolote utakaloshauriwa liwe zuri au Baya. Ukilifanya jua wewe ndio umefanya. Hivyo mkosolewaji wa Kwanza ni wewe kiongozi.

Kama ungejua Maana ya Rais basi ungeelewa kuwa anauwezo, mamlaka, na nguvu ya kuchunguza Jambo(ukweli wake) Kabla hajalifanya.
Hiyo ni tafsiri Yako,sheria zetu zinaweka distinction hasa Kwa ngazi ya Rais
 
Back
Top Bottom