Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Mara nyingi tunasikia viongozi wakisema “nendeni mkafanye”. Hiyo haitoshi kuleta utekelezaji. Lazima kutoa KPI (Key Performance Indicator) na kufuatilia utekelezaji wake.
Kilicholeta maendeleo ya haraka China ni hivi: kila mtendaji anapangiwa KPI zake na wa juu yake anafuatilia. Ufanisi unapimwa, ukiwa umefanikisha unasonga mbele la sivyo unapisha nafasi. No stories, no excuses, just get it done.
Nimeona Makamu wa Rais amelalamika kwamba tunaagiza biskuti na sabuni nje. Akasema hilo ni kutumia fedha vibaya na kuwanyima Watanzania nafasi za kazi. Badala ya kuwapangia mawaziri husika KPI yeye akasema “nendeni mkalifanyie hilo kazi”. Those are not effective words. Nothing will happen.
Kuna hizi fedha za Uviko ambazo zimeelekezwa kwenye kujenga madarasa na vituo vya afya. Kutaja idadi ni mwanzo mzuri. Idadi halafu “nendeni mkalifanyie kazi” haitoshi. Rais na Waziri Mkuu wangepashwa kuagiza ma RC walete work plan za kila mkoa kufikia tarehe….. Na ma RC waagize DC kuleta GantChart ya utekelezaji wa ujenzi wa hayo madarasa 70 ya kila Jimbo kufikia tarehe…… na ma DC waagize kuletewa building plans za kila darasa na Watendaji kufikia tarehe…. etc.
Maneno ya kificho cha uvivu na uzembe (kama "mpango mkakati unaendelea" na "mchakato wa mpango mkakati" yakatazwe). Jiwe alikuwa na mapungufu yake lakini neno lake la “hapa kazi tu lilikuwa spot on”
Tumevurunda vya kutosha, sasa tuache maneno. Kama Makamu wa Rais anataka tuwe na viwanda vya biskuti na sabuni aache neno jepesi la “kalifanyieni kazi”. Aanze yeye kulifanyia kazi. Atoe DIRECTIVE nini hasa kifanyike na ni nani akifanye na kikamilike lini. Kila asiyeweza kufanikisha KPI zake aondoke tu, maana hakuna namna.
Maneno yangekuwa yanaleta maendeleo basi Waswahili wangekuwa wameendelea sana.
Naomba kumalizia kwa kuuliza: kuna mtu amewahi kuona GantChart ya ujenzi wa SGR au Bwabwa la Stiegler Gorge? Vinamalizika lini? Yaani hata Dar to Dodoma SGR bado treni haitembei? Si kuna umeme wake tayari, na sio kusubiri Stiegler Gorge? Tumechoka kuisikia hiyo SGR, sasa tunataka tuone treni ikitembea.