Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Ombaomba limekuwa ni tatizo kubwa katika miji mikubwa kama Dar es salaam. Upitapo maeneo ya Posta mpya, Fire na Magomeni utakutana na kundi kubwa la ombaomba vijana, watoto na wazee na hata watu wa makamo. Idadi yao inaongezeka kila kukicha.
Leo nimepita maeneo ya Magomeni na kukutana na gari ya manispaa ikiwa inawakamata ombaomba. Sikujua wanawapeleka wapi baada ya kuwakamata? Inawezekana wanawakamata na kuwarejesha makwao. Je hii kamata kamata itakuwa endelevu? Au ni nguvu ya soda. Mimi ningeshauri wapelekwe mahali wafundishwe jinsi ya kujitegemea na kazi ngumu ikiwemo kuwafunga. Kwani warudishwapo makwao hawakawii kurudi mijini.