Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Dr Slaani jembe na huwezi kumlinganisha na Mh Zitto
1/ Dr Slaa ni mzoefu wa mapambano na mafisadi
2/ Dr Slaa ni mzalendo ei aliwaorodhesha Mafisadi ambao mpaka leo wanawasumbua CCM kujivua GAMBA mpaka kesho.
3/ Dr Slaa hatumiwi na CCM kama ambavyo kijana hutumiwa nyakati fulani na Mafisadi kuchanganya na kuvuruga
mustakabali wa chama na mtasikia ripoti ya mafisadi wa madini mtasikia
4/Dr Slaa harubuniki/hana historia ya kuasi chama chake(chadema alishindana na CCM Akahama) kama kijana alivyorubuniwa kwenye misimamo ya chama kule bungeni alipojificha kwenye issue ya kupambana na DHAIFU.:israel:
 
nimepiga kura yangu si kwamba nafurahia uzi huu, bali ni kuonesha kuwa huwezi kulinganisha mlima na kichuguu.
pili si wakati muafaka wa kujadili mambo kama haya. huyu dogo (nyepesi)nimeanza kumtilia mashaka kama hajanunuliwa na magamba.
 
Ukweli wa mambo Zitto anakosa sifa moja tu ya umri, Dr Slaa anayo sifa ya umri unaoruhusiwa na katiba inayoelekea ukingoni zilizobaki wote wanazo, kuna mambo mengine sioni kama yana uhusiano sana na urais, uzinzi, uasherati na umalaya ni tabia karibu za wanaume wote, hekima na busara nyie wenyewe mnajua, uwezo wa kujenga hoja mjengoni wengi tumekuwa mashahidi kwenye hili, tuliona zama za slaa tukaona zama za kabwe, hawa jamaa wote ni majembe, kusema nani bora wengi wenu mnaangukia kwenye chuki za udini na ukabila camooon watanzania wapi mnaelekea huko?
 
1.mwenye busara,mkweli
2.asiyenunulika na kujitenga na rushwa
3.anayeamini chama ni zaidi yake
4.hana visasi achilia mbali kauli zinazohujumu chama
 
Kumlinganishsa zitto na slaa ni kumdharirisha Dr. Slaa maana huyu jamaa anakubalika na umma wa watanzania walio wengi.
 
Ukweli wa mambo zitto anakosa sifa moja tu ya umri, dr slaa anayo sifa ya umri unaoruhusiwa na katiba inayoelekea ukingoni zilizobaki wote wanazo, kuna mambo mengine sioni kama yana uhusiano sana na urais, uzinzi, uasherati na umalaya ni tabia karibu za wanaume wote, hekima na busara nyie wenyewe mnajua, uwezo wa kujenga hoja mjengoni wengi tumekuwa mashahidi kwenye hili, tuliona zama za slaa tukaona zama za kabwe, hawa jamaa wote ni majembe, kusema nani bora wengi wenu mnaangukia kwenye chuki za udini na ukabila camooon watanzania wapi mnaelekea huko?

Ninavyoona hapo kwenye results,japo ni mapema kusema, nadhani mashaka yako ya udini na ukabila yanaanza kupungua
 
nimepiga kura yangu si kwamba nafurahia uzi huu, bali ni kuonesha kuwa huwezi kulinganisha mlima na kichuguu.
pili si wakati muafaka wa kujadili mambo kama haya. huyu dogo (nyepesi)nimeanza kumtilia mashaka kama hajanunuliwa na magamba.
si ajabu ndo kaanzisha uzi huu
 
1. Zito Kabwe, haamiiki. Ni kigeugeu. Hajiamii pia. Ndio maana mara nyingi hufanya mambo ambayo huleta hali ya wasiwasi kwa wenzake ktk chamam chama chake.
Huweszi kumwamini zito.
Mtu anayeambataa a Wema Sepetu, si dhani kama anaweza kuomgoza Taifa. Anachotamani Zito ni kama tu Kikwete. U-celebrity. Mengi anayofanya - huwa ni kwa ajaili ya kujenga jina na heshima yake. Hafai kwa raisi. Too much Pride in him. He lacks humility.
 
Kwani CDM hawana mchakato ambao uko defined na unaeleweka wa kuwapata wagombea urais? Mi naona mada hii lengo lake ni kuleta vurugu ndani ya CDM. CDM kaeni macho . . .
 
Dr. Slaa kwanza ni mtu (mzee) hasiendeshwa na hisia, ana udhubutu na uhodari kuliko Zitto, Zitto anaonyesha anaweza kurubuniwa kirahisi (SUALA LA NISHATI & MADINI), na Dr. Slaa ni mzalendo wa kweli (rejea kauli yako baada ya uchaguzi 2010...siko tayari kuingia ikulu kwa damu ya mtanzania kumwagika) kitu ambacho naamini Zitto hawezi.
 
Mimi siwezi kutoa maoni.....kumuweka dr.slaa na zitto kishoka nadhani ni dharau sana......zitto hajafika hata robo ya dr.slaa kwa hiyo kura ya maoni ni dharau kwa kiongozi mwenye heshima km dr.slaa.....sijui labda zitto umshindanishe na shibuda ingefaa kwani hata kwa mnyika au lema haingii

tuacheni dharau kwa rais wetu

Haya a mengineyo yote ni maoni ,ila naomba msome hii!! hivi ni nini kiini cha wazo la huyu mtoa mda kwa mtazamo wako? kwa kiini hicho, katika wakati huu tete, unadhani ni vema kwa watu wapevu kisiasa kulianzisha hili?

vile vile ukijiona wewe ni mchanga ktk uchambuzi na utambuzi wa mada fulani, ili usimuudhi hata MUNGU, usithubutu kuinua mada nyeti kama udini mahali hapa na wakati kama huu, tena kwa staili kama hizi watoto mnazo kurupuka nazo!

hivi kunaugumu kujua ni akina nani wanaubeba udini Tanzania hata uanze kuwasukumia mada/kosa wasiohusika kwa kiwango kikubwa. Kila uchao tunaona matendo ya ubaguzi na ushabiki wa kidini kwa watu fulani (nasisiiza kila uchao) sasa akitoke mtu anajifanya haoni hayo unatafuta kuwapachika wengine zigo hilo, anajichoresha kwani hatukawii kumwona mzushi na mpotosha uhalisi...kumbuka sifa moja imara ya ukweli huwa haukubali kudharauliwa hutafuta kwa bidii kujidhihilisha, hapo ndipo mzushi ataumbuka.

wewe uliyeanzisha mada
unatakiwa kuwa na uwezo wa kupima kabla inaweza kwenda wapi?

na wewe unaye ingiza udini kwa watu wasiouasisi
unajidhalilisha kwa kuonyesha udhaifu wako, huwezi tafuta mchanga ufukweni!!!!!?? utauona bila kuutafuta, tumia japo kiduchu akili uliyopewa na Mungu muumba wa mbingu na nchi.

kwa watu wote! tutazame mambo kwa uhalisi, kama haki ingetendeka sote twajua heshima ambayo W.Slaa angepashwa kuwanayo leo, hivyo tusimchukulie poa, tuache nazi iwe nazi na kichwa kuwa kichwa.
 
Mtoa mada kuwa makini kwa mada kama hii,kamwe huwezi hata kidogo kumpambanisha Dr W.P.Slaa na Zito Z. Kabwe, Zito hata hafikii hata nusu thelusi kwa Dr W.P Slaa so hii hata ukumuuliza mtoto wa darasa la kwanza atakuambia Dr Slaa hanaa mpinzani kwa nchi hii sema kwa kuchakachua kura watamweza.Mie nakubaliana na mchangiaji mmoja kasema Zito anaweza kupambanishwa na J. Shibuda kwani hata kwa Mnyika na Lema hajafikia bado.

Tatizo la Mh Zito mapepe na yule Zito wa miaka ile siye huyu wa leo ona kila leo anavyochachatika mara kule mara huku so mtu kama huyu hatumuelewi kiivyo maake ni kama kigeugeu. Kila zali yumo Lol. Mh Zito sie watu wako tunaomba urudishe mambo yako yale ya miaka 2 iliyopita we need you man.
 
huu ni wehu CHADEMA tumesha washtukia njama zao hakuna Kabwe wala Slaa. hawapati kura hata mmoja nawajipanga maana jimbo la Iringa mjini washa lipoteza tayari kwasababu za udini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom