Zanzibar ni dola kamili na mihimili yake yote mitatu, Mahakama, Serikali na Bunge. Hivi wao sasa wanalalama nini, bara ndio waliokuwa hawana kitu. Nafikiri Zanzibar wangeshughulikia serikali ya Tanganyika, Badala ya kuzungumzia kuvunja muungano.
Fredrick Sanga
Kuna uzi huu https://www.jamiiforums.com/habari-...hati-za-muungano-ndio-hizi-2.html#post3971657
Huyu jamaa ametoa wazo la Tanganyika (Tanzania bara) ikubali kuwa dola kamili. Hili wazo likitekelezwa huenda Muungano akaimarika.
Wazo lake, anataka Tanganyika iwe dola kamili kama Zanzibar kwa miaka 48 ili ipate faida ya Muungano. Pia anashauri Zanzibar ifutike,ipotee kama ilivyopotea Tanganyika badala yake iwe ndio Tanzania.
Mimi nilipolisoma wazo lake nilipata tabasamu, nilielewa na kutanabahi kuwa kero za Muungano zinaweza kupatiwa suluhisho na njia za kuuenzi Muungano wa Tz zipo na pande zote za Muungano zitafurahia Muungano na kuona faida ya Muungano.
Hii ni hoja nzito sana, Kama hata JK 1st aliona hiyo basi.
Changamoto ndio imetolewa hiyo, tuwahimize wabunge wetu makini akina Zitto, Mnyika, Mbowe, Shibuda , na hata wale wa CCM wanaotaka kuuenzi Muungano walifanyie kazi wazo hili (changamoto iliyotolewa).
Mzee Mwanakijiji juzi ametangaza rasmi kuwa kero za Muungano hazitatuliki, nafikiri alikurupuka. Katika watu wote wanaotetea Muungano. Mzee mwenzangu juzi alimwaga manyanga, alitamka Muungano uvunjwe.
Mwalimu alitoa rai kuwa itakapoanzishwa tena jumuiya ya Afrika Mashariki basi Tanzania iwe na serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar
(Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11 .link ya kitabu hii Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere) )
Lakini hii rai ya mdau nafikiri ni bora kuliko rai ya Mwalimu. Kuna msemo wa kiswahili usemao, "Mchawi, mpe mtoto alee". Tuwabebeshe dhamana Zanzibar kwa miaka hata 20 tu sio 48 ili na wao waone ugumu na raha za kulea Muungano.
Kuuvunja muungano ni sawa na kula sumu. Hii siikubali kabisa
Mimi nina ndugu kabisa huko zanzibari, na wadogo zangu wameoa huko. Sioni haja ya kuvunja muungano, ila kuujadili na kuuimarisha. Hii mambo ya Muamusho ni hovyo kabisa.
hapo hata mimi nakubali hatuwezi kujadili Muungano huku tumeizika Tanganyika!
Watu kama nyie mko wachache, mnaelewa mambo haya vizuri. Wengine wamekazania gharama tu. Je gharama za kukosa Tanganyika?
Zanzibar ni dola kamili na mihimili yake yote mitatu, Mahakama, Serikali na Bunge. Hivi wao sasa wanalalama nini, bara ndio waliokuwa hawana kitu. Nafikiri Zanzibar wangeshughulikia serikali ya Tanganyika, Badala ya kuzungumzia kuvunja muungano.
Mimi nina ndugu kabisa huko zanzibari, na wadogo zangu wameoa huko. Sioni haja ya kuvunja muungano, ila kuujadili na kuuimarisha. Hii mambo ya Muamusho ni hovyo kabisa.
Kuuvunja muungano ni sawa na kula sumu. Hii siikubali kabisa
Kwani lazima wanandoa wote wawe wa nchi moja? mbona kuna watanzania wengi tu wameoa au kuolewa na wasio watanzania? Muungano ukivunjika ni wajibu wa waliooana kuamua wawe upande upi wa nchi? kama mtu unaipenda nchi kuliko ndoa yako au familia yako basi waache uwe raia wa upande unaoupenda.
Maisha popote Watanyika walioko Zanzibar wanaweza kurudi Tanganyika na wakaendelea tu na maisha. Au wakabaki Zanzibar na kuishi kama wahamiaji.
Mimi nina ndugu kabisa huko zanzibari, na wadogo zangu wameoa huko. Sioni haja ya kuvunja muungano, ila kuujadili na kuuimarisha. Hii mambo ya Muamusho ni hovyo kabisa.
unajua kuwa Mombasa ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar mpaka 1963 , na kuna watu wengi wa huko walioana na wazanzibari ?? jee mbona huo muungano haupo ?? Karume ni mzaliwa wa Nyasa na amekuwa Rais Zanzibar na ameowa Zanzibar mbona
huo muungano haupo ??? kuna wajaluo Kenya na Wajaluo Tanganyika mbona hamuungani?? kuna wamasai Kenya na Tanganyika mbona huo muungano hamuungani huko ??