Kura ya Hapana yazidi kupaa CHADEMA , Humphrey Polepole, Prof. Lwaitama na Askofu

Hawakukosea mwisho wake ungekuwa mbaya interahamwe maccm yangefanya mabaya zaidi kinachotakiwa kupiga kura ya HAPA NA
 
Bila mahakama ya KADHI nasema hapana.Naungana na waislamu katika hili.Zile ahadi za Pinda waislamu msiziamini kabisa.
 
Wakuu,

Bila kwenda vijijini kuwaeleza maana ya HAPANA yetu...haya maccm yatapita. Bila kujiandaa kulinda kura haya maccm yataiba kura zetu za HAPANA. Kazi kwetu...yapo yanachungulia kwa makini sana.
 
Hivi kweli mtu akishajua kusoma na kuandika awe mbunge then Waziri tutegemee mikataba ya aina gani????ni wendawazimu tu watakaoipigia kura ya ndiyo katiba ya 6 na vijisenti
Kwenye uwaziri wamesema lazima awe na degree, mbunge ruksa kuwa std seven ila waziri lazima aanzie degree!!! Kweli kuwa mtanzania ni majanga tena sio madogo!!!
 
'''''''''''''''''''''
nasema hapana ina maana gani , kwani hutaki hata haki ya kuishi , kuabudu , kusoma , kuishi , kuenzi muungano , kuilinda Tanzania kwa gharama yoyote , Demokrasia , haki za binadamu kwa ujumla ,n.k. Naomba unieleweshe ili ikae vizuri . Na , tusaidie vipi ambavyo ni hapana kwenye katiba iliyopendekezwa ili tusije tukabatizwa hapana kw kila kitu tuakaonekana ni wehu kitaani .Please nieleweshe.

haya yangewekwa kwenye nchi husika, ni upuuzi kuizika Tanganyika wakati iko hai na siyo hoi
 
Mkuu kama hujaelewa wewe piga unavyoona.KUMBUKA samaki mmoja akioza tenga zima limeoza. Mimi na familia yangu wakiwemo wake 6 na watoto wenye uwezo wa kupiga kura 35 tutapiga kura ya HAPANA

duh! duh!
 
Mambo niliyopendekeza kwa mzee warioba yote hakuna nilimwambi sioni umuhimu wa mkuu wa wilaya sipendi mtu aliyelitumikia Taifa akastaafu alafu eti anateuliwa na mtu mmoja kuwa mkuu wa mkoa nilitaka tanyanyika nami nifurahi kama wanavyofura ndugu zetu zanzibar nilitaka waziri asichaguliwe na mwenye nchi apeleke sifa zake bungen ndipo wabunge wamchague nilitaka kiongozi ameisababishia hasara nchi ashtakiwe nakufungwa kama wezi wakuku wanavyohukumiwa na sikujiuzuru nakuachwa kama wanavyofanya sasa kwakua hayo hakuna nitakuwa muwazi nakusema mimi HAPANAAAA.
 
Katiba hii pendekezwa ni mbaya kwa sababu;-

1. Tanzania upande wa Zanzibar kazi yao ni kutoa makamo wa rais , urais wenyewe Ngo`ooooo.

2. Maadili ya viongozi yaliyopendekezwa na tume ya kukusanya maoni yamefutwa, madhara yake mtumishi wa umma atataka kupata kiti tu na meza kwenye ofisi za umma hata asipopewa mshahara ndani ya mwaka mmoja tu wa ajira atakuwa amajenga nyumba , amenunua gari , amafanya harusi kubwa hadi kuchinja ngamia.

3. Madaraka ya rais kupunguzwa kama ilivyopendekeza tume ya Warioba imefutwa madhara yake,mashemeji wa mke wa rais, marafiki wa mtoto wa rais , mahawala wa mke wa raisi kabla hajaolewa na rais, waliokataliwa na wanainchi kwenye chaguzi kuu, waliofungwa wakatoka jela kwa msamaha wa rais woteee watapata vyeo kama ukurugenzi, ukuuwa wilaya na mkoa na vyeo vingine. Wanye kustahili na sifa za kutosha watakosa.

4. Ubunge au udiwani wawe na Elimu ingalao kidato cha nne imefutwa madhara yake, hii italeta madhara makubwa sana sana kwenye halimashuri kwa sababu wasimamizi ambao ni madiwani watazidiwa sana ki-elimu na watendaji wa halimashauri ambao ni mkurugenzi na wakuu wake wa idara. Fedha za kodi hukusanywa na TRA na zote hupelekwa hazina,kule hazina fedha hizo hurudishwa kwenye halmashauri ambako kuna watu kwa ajili ya kutekelezwa miradi mbali mbali ya maendeleo. Sasa kwa kuwa wasimamizi (madiwani) ambao wengi wao ni darasa la saba watashindwa kuzisimamia fedha hizo kutokana na umbumbu wao, watendaji(mkurugenzi na mkuu wake wa idara) watatumia mwanya huo watawaibia fedha zote mwisho wa siku miradi haitakamilika. Mfano hai halmashauri ya wilaya ya Mtwara chini ya mbunge Hawa Ghasia ina madiwani mambumbu tupu. Idara ya afya tulikula fedha zote za Semina za ukimwi, tulitengeneza semina hewa kwa maana waliohuzudhuria walikuwa ni hewa, attendance registar ilikuwa ni hewa, payment vocha tuliandika majina hewa na tukatia sahihi zao hao watu hewa na tukuchukua mshiko wote shs 60,000,000/= madiwani husika walitia sahihi zao kwenye ripoti tuliyowapelekea HAWAKUJUA CHOCHOTE MASKINI. Huu ni mfano wa halmashauri moja tu na zingine ni hivyo hivyo lakini kama madiwani wangekua na elimu ya kutosha kwa maana wangafanya monitoring kule site wangeangalia majina na kuwafuata wahusika lazima tungekamatwa.

5. 50 kwa 50 katika vyombo vya maamuzi wanawake na wanaume hii ina madhara makubwa sana kwa sababu muumba mwenyewe aliliona hili akaweka viwango na kila mtu anajua mungu alimpa mamlaka nani, hata hivyo hilo la 50 kwa 50 likitekelezwa kwenye majeshi, inchi itatekwa, Majambaji yatakuwa kila siku yanakimbia, Takukuru hawawezi kuwakamata wanaopokea hela za moto maana mala zote watuhumiwa watawashinda nguvu watakimbia na hela za moto zitapotea serikali itakula hasara.

Hii ni mifano michache tu ya ubovu wa katiba pendekezwa ya wabunge wa CCM,ILE YA WARIOBA ILIKUWA BOMBA WATU KAMA AKINA RAGE wasingepata uongozi tena ndani ya katiba ya tume ya Warioba.

Wale waliokuwa wanaitwa UKAWA walifanya makosa makubwa sana kususia wangebaki mule mule ila wakomae na rasimu ya WARIOBA, waliwaachia nyani shamba la mahindi.

Ikija KATIBA hiyo wanainchi tuikatae kabisa.

UKAWA na wanaharakati watetezi wa rasimu ya pili ya katiba watengeneze jedwali (Matrix) la kuonyesha vifungu katika rasimu ya 2 vilivyoachwa au kurekebishwa sambamba na jinsi vilivyo katika katiba pendekezwa na mwisho kwa kila kifungu waweke madhara (effects) za kuachwa ama kurekebishwa kwa kila kifungu.

Kwa kuwa wananchi wengi ni wavivu wa kusoma, nina hakika andiko hilo halitakuwa kubwa hivyo likiwekwa kwa aina ya vijalida hata wale wavivu wa kusoma wataweza kusoma.

Vijalida hivyo vinaweza kusambazwa bure kwenye mikutano ya hadhara, sehemu za mikusanyiko ya watu, kwenye foleni za magari na mahali pengine ambapo ni rahisi kusambaza.
 
Nasema hapana

HAPANA Kwasababu .Wameondoa Kipengele Cha 1.Ukomo Wa Ubunge 2.Kiwango Cha Elimu Cha Mbunge Kilichopendekezwa Na Warioba.3.Kumwajibisha Mbunge Mtoro Kabla Ya Uchaguzi Mkuu.4.Wabunge Kutokuwa Mawaziri Wao Wamekiondoa Na Kuacha Kile Chazamani Kiendelee.5.Zanzibar Kutunyonya Wakati Tanganyika Haipo. KWAHOJA HZ NA ZINGINE NYINGI.NASEMA H A P A N A.
 
Kura ya hapana imezidi kupata wafuasi na vyama vya siasa baada ya CHADEMA kutangaza wazi kuunga mkono kura ya HAPANA na ufunguzi kufanyika tarehe 14 kwa kongamano.

Kongamano litaoongozwa na viongozi wa CHADEMA , Profesa Lwaitama na mjumbe wa kamati ya kukusanya maoni Humphrey polepole.

Na hii imefanya watu waliojitoa waziwazi kuunga kura ya hapana kuongezeka baada ya askofu wa jimbo la rulenge askofu niwe mgizi kutangaza waziwazi.

Mtihani mkubwa bado hupo kwa baadhi ya vyama vilivyokaa kimya . Cuf na nccr katika umoja UKAWA.

Ambavyo havijasema lolote kama watashiriki au la

mimi nnachokiona n hv,
ccm wanatafta kuja za ndyo, nahc watafanya mchezo mchafu, km huu, Wanavyokwenda kwa wananchi wanatoa ya Warioba, wananchi wanapga ndyooo,
zen kwenye majumuisho watasema katiba ya Chenge + 6 ndyo ilipgiwa ndyo, so itapitishwa hyohyo, hawa watu wanawezafanya hvyo,
My take: WANANCHI KUWENI MAKIN PALE MTAKAPOLETEWA KATIBA PENDEKEZWA NI IP IL UPIGAPO KUJA UJUE UMEPGIA IP,
Nawasilisha:
 
Back
Top Bottom