Kupigia kura vivutio vya Tanzania kuingia katika maajabu saba ya dunia

NKANOELI

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
203
61
Ninafikiri ingekuwa jambo la busara kama mitandao ya simu ingeunga mkono hili jambo kwa kufanya utaratibu wa kutuma sms -kupigia kura vivutio vyetu kwa sababu kwa mtandao pekee itakuwa ngumu kushinda kwani walio na acess ya mtandao ni wachache,kama kutakuwa na namba ya sms ninahakika kura zitakuwa nyingi.Nawasilisha na naomba kusahihishwa kama sijaiweka sawa.:A S 465:
 
Nina maana watu waweze kutumia simu zao kupiga kura kwa vivutio vyetu:Serengeti,Mlima kilimanjaro n.k
 
Yan sisi tupige kura wao wasafirishe Twiga wetu na ndege waka wauze!
 
Labda kupiga kura kuwa Tanzania ni nchi ya maajabu saba kwa wizi, umalaya, uongo kwa viongozi, wivu kwa waliokikosa, uoga, kichwa cha mwendawazimu dili za ajabu kama kuuza twiga
 
Samahani kwa waliopitia uzi huu wakitaraji kukuta list ya maajabu ya dunia.
Lengo langu ilikuwa kutafuta majibu ya swali nililojiuliza muda mrefu.
Nimewahi kusikia kipindi fulani watu wakihamasisha wenzao kupiga kura kwa wingi ili kuwesha kitu fulani
kuingia katika kinyang'anyilo cha maajabu 7 ya dunia na hatimaye kushinda katika shindano hilo.
Swali ni hili, kuna haja gani ya kupiga kura ili kuwezesha kitu fulani mfano, mlima Kilimanjaro ili kuingia katika mashindano
wakati mlima uko pale na kama sifa zipo?
Wingi wa kura unawezaje kuathiri maajabu au upekee wa kitu?
Naomba kufahamishwa.
 
Swali lako zuri, lakini ikumbukwe kuwa Greeks ndio waliokuwa wa kwanza kuingiza rekodi za maajabu 7 ya dunia miaka 2000 iliyopita. Na vigezo vilikuwa ni sehemu zilizojengwa wakati huo ndio ziliorodheshwa, baada ya hapo ikawa tukawa tunapiga kura kuchagua maajabu hayo duniani kote. Unaposema mlima Kilimanjaro huo hauwezi kuingia kwenye maajabu ya dunia kwani haukujengwa na binadamu, Bali tunaangalia vilivyojengwa tu. Mwaka 2007 kulikuwa na kura za kuchagua ni yapi maajabu ya dunia na huwa hazivuki saba ingawa kuna mengi ya kuingia katika shindano hilo. Sasa basi mwaka 2007 watu wengi walijitokeza kupiga kura huwezi amini watoto ndio walikuwa wengi zaidi kupigia kura hayo maajabu ingawa sina uhakika Tanzania walichangia wangapi maana walikuwa watu milioni 90 waliopiga kura nafikiri Great pyramids haikuwemo na MACHU PICCHU ilikuwa ya nne. Pia kwa kuongezea tu watu wengi wanachanganya kati wonders of the world na Unesco world heritage sites.
 
Nina maana watu waweze kutumia simu zao kupiga kura kwa vivutio vyetu:Serengeti,Mlima kilimanjaro n.k

Naona hapo unachanganya, maana maajabu ya dunia ni yale yaliyojengwa miaka 2000 iliyopita tu na si vinginevyo. Na kuhusu vivutio ambavyo vinalindwa kitaifa ni tofauti kabisa kwa hiyo unapoongelea Serengeti na Kilimanjaro ni world heritage sites zikiwemo nyingi tu Tanzania ambazo zinalindwa kitaifa ikiwemo pia mji wa mawe Zanzibar
 
Samahani kwa waliopitia uzi huu wakitaraji kukuta list ya maajabu ya dunia.
Lengo langu ilikuwa kutafuta majibu ya swali nililojiuliza muda mrefu.
Nimewahi kusikia kipindi fulani watu wakihamasisha wenzao kupiga kura kwa wingi ili kuwesha kitu fulani
kuingia katika kinyang'anyilo cha maajabu 7 ya dunia na hatimaye kushinda katika shindano hilo.
Swali ni hili, kuna haja gani ya kupiga kura ili kuwezesha kitu fulani mfano, mlima Kilimanjaro ili kuingia katika mashindano
wakati mlima uko pale na kama sifa zipo?
Wingi wa kura unawezaje kuathiri maajabu au upekee wa kitu?
Naomba kufahamishwa.
Hili ni wazo lakini kumbuka uzuri au ubaya wa asili hauboreshwi kwa kupiga kura bali upo kwa asili. Haya sio mambo ya bongo fleva na akina wema.
Ingelikuwa kura zinawezesha kitu kuwa bora basi Nigeria ambayo ina wakaazi karibia 190m na subscribers wengi wa simu ingeliongoza kwa vivutio. Na hivyo vivyo kwa ngazi ya dunia basi china ndio ingeliongoza kila kitu.

Back
Top Bottom