doctorz
JF-Expert Member
- Aug 10, 2010
- 916
- 228
Kwanza sifahamu wewe kama ni mvulana au msichana. Vijana wa jinsia zote wanapofikia umri wa kubaleghe huwa wanapitia kufanya hivyo. Kwa hali ya kileo, kufanya hivyo ni bora kuliko kujamiiana bila ya kinga sababu ya AIDS. Ushauri wangu wa kitaalam ni jitahidi kuanza mazoezi kama kucheza mpira kunyanyua vyuma, joging, au tafuta jambo ambalo litakutoa kwenye fikra za ngono. Pili ni tafuta mwenza ambaye ataku timilizia mahitaji yako ya kihisia. Tatu ni fanya safari ya kwenda mji mwingine upatapo likizo. Vyote hivi vitaku ondoshea fikra za kihisia na kukuokoa kutoka tabia mbaya hiyo. Ukizoea saaana kufanya hivyo itakuwa hata ukipata mwenza hutapata raha yeyote hadi ujikimu kwa tendo lako baya hilo. Kwa msaada zaidi nenda psychiatric unit iliyo karibu nawe au nione mie nikupatie msaada.