Jamani naomba msaada. Maana huwa napiga chafya sana kila ninapohisi kunusa vumbi, mtu akivuta sigara moshi tu ukipita mbele yangu, pia kama natafuta nguo kabatini, nikipulizia pafyumu n.k. Chafya hiyo huambatana na mafua mepesi. Naomba mwenye kujua dawa yake nifanyaje maana hospitali huwa napewa piliton, chengachenga n.k bila mafanikio.